Wednesday, June 24, 2015

NCHINI ZANZIBAR MAWAZIRI WA CHAMA CHA CUF WASUSIA BAJETI

Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Ahmed Nassor Mazrui, akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habarai katika Ofisi za CUF Vuga baada ya Mawaziri wote wa CUF na wajumbe wa Baraza la wawakilishi kupitia Chama hicho kususia kupitisha bajeti Kuu ya serikali. Kutoka ni   Waziri wa Sheria na Katiba, Abubakary Khamis, Waziri wa Mifungo na Uvuvi, Abdillah Jihadi, Waziri wa Miundo Mbinu na Mawasiliano, Juma Duni Haji, Waziri wa Habari, Utamaduni Utalii na Michezo said ali Mbarouk na Waziri wa Nchi Ofisi ya makamo wa Kwanza wa Rais, Fatma Fereji.
Nchini Zanzibar kasheshe zinaendelea. Mawaziri wa Serikali 
ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na Wawakilishi kutoka chama cha 
CUF jana walitoka kwenye kikao cha bajeti cha Baraza la 
Wawakilishi, wakipinga urasimu katika utoaji vitambulisho 
vya ukazi wa nchi ya Zanzibar na uandikishaji 
wapigakura. Muda  mfupi baada ya tukio hilo, Serikali ya 
Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ilitoa taarifa yake ikisema 
kitendo cha mawaziri wa CUF kutoka kwenye kikao cha bajeti 
ni kuvunja katiba, kwa kuwa wameshindwa kuheshimu 
kiapo cha utii katika utekelezaji wa majukumu yao, kwa 
mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
Mawaziri hao walitoka nje ya kikao hicho muda mfupi baada 
ya Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Juma Duni Haji 
kusimama na kutoa malalamiko ya kutoridhishwa na utendaji 
wa SUK katika kusajili na kutoa vitambulisho hivyo 
vinavyotumika katika kuandikisha wananchi kwenye Daftari 
la Wapigakura. Wakati wawakilishi hao wanaondoka ndani 
ya ukumbi, wenzao wa CCM walikuwa wakipiga makofi huku 
wakiimba “CCM, CCM, CCM”, na baadaye baraza 
kuendelea na muswada wa kupitisha mapato na matumizi ya 
bajeti ya mwaka 2015/2016. Mawaziri waliohudhuria 
mkutano huo ni Abubakar Khamis Bakar ambaye ni Waziri 
wa Sheria na Katiba, Fatma Abdulhabib (Nchi, Ofisi ya 
Makamu wa Kwanza wa Rais), Abdilahi Jihadi Hassan 
(Mifugo na Uvuvi) na Haji Mwadini Makame (Ardhi, 
Makazi, Maji na Nishati).
“Tumeamua kutoka ndani baada ya kuona wenzetu 
tuliowaamini, wametubadilikia. Hawana nia njema ya 
kuendesha serikali ya pamoja,” alisema makamu 
mwenyekiti wa CUF, Juma Duni Haji alipoongea na 
waandishi baada ya kutoka kwenye ukumbi 
huo. “Wameanzisha Serikali ndani ya Serikali na sasa 
wanawanyima haki wananchi kinyume na 
katiba.” Juma Duni alisema kwa miaka mingi wananchi 
wamekuwa wakizungushwa kusajiliwa na kupewa 
vitambulisho vya ukazi, hali inayowaweka katika hatari ya 
kupoteza haki zao za kijamii, ikiwa ni pamoja na fursa ya 
kushiriki Uchaguzi Mkuu. Hata hivyo, alisema uamuzi wao 
haujavunja katiba ya nchi ya Zanzibar na kwa hiyo 
wataendelea na shughuli za Serikali kama kawaida.
Alisema kuwa kazi ya uandikishaji wapigakura kwenye 
Wilaya  ya Magharibi, Unguja imetawaliwa na vitisho na 
kwamba watu wasiojulikana wamekuwa wakionekana 
wakiwa na silaha za moto na kujifunika vitambaa usoni 
mithili ya maninja na wengine kuvaa vinyago. “Katika 
maisha yangu sijawahi kuona askari anayekwenda 
kulinda akificha uso na huu ni mkasa mpya duniani. 
Huwezi kumlinda raia kwa silaha za moto wakati yeye 
hana chochote zaidi ya mikono yake,” alisema Juma 
Duni. Naibu katibu mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui 
alisema kuna vijana wame kwama kuandikishwa na 
kuitaka Serikali kuondoa urasimu katika upatikanaji wa 
vitambulisho vya ukazi.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment