Thursday, June 4, 2015

VIDEO-SITTA ATII NA YEYE AMETANGAZA RASMI KUGOMBEA URAIS WA NCHI YA TANGANYIKA DUUUUUUU!!!!


SITTA UNAIKUMBUKA SIKU HII AU USHAISAHAU....????

SITTA UNAIKUMBUKA SIKU HII AU USHAISAHAU....????
WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta atii na yeye ametangaza rasmi nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya wa Tanganyika kupitia CCM na kusema atii ana ari, uwezo na utayari wa kuiimarisha nchi na kwamba kipindi kimoja tu cha miaka mitano kinamtosha. Mbali na hilo, Sitta amesema akifanikiwa kupata nafasi ya kuongoza nchi atahakikisha anatenganisha masuala ya siasa na biashara, kwa sababu ndiyo chanzo cha rushwa kubwa na kufikiwa kwa mikataba mibovu.((mbona huku mwambiya kikwete miaka kumu umo madarakani na kikwete mbona hukumuambia hayo..??)) Alitangaza nia yake hiyo jana kwenye eneo la Itetemia (Ikulu) mkoani Tabora ambako kulikuwa na makao makuu ya mashujaa wa Unyanyembe wakiwemo Isike na Kiyungi walioendesha harakati dhidi ya dhuluma na unyanyasaji wa wakoloni.((nyinyi wenyewe wakoloni weusi tanganyika))
Pia, neno ‘Ikulu’ asili yake ni Itetemia baada ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ilipofika mwaka 1961 kuamua kulitumia neno hilo la Kinyamwezi liwe mbadala wa maneno ya kikoloni ya ‘State House’ kwa ofisi na makazi ya mkuu wa nchi ambayo kwa sasa yapo eneo la Magogoni, Dar es Salaam nchini Tanganyika. “Uimara wangu kiuongozi nitajumuisha nguvu na maarifa ya wananchi ili tuvuke salama na pia tutekeleze kazi za maendeleo kwa ufanisi na tija zaidi. ...nakuja kwenu Watanganyika kuomba niwatumikie katika nafasi hii ya juu ya uongozi.((wananchi wananchi sindio ulio walazimisha walikubali katiba lako ulilo tengeneza wewe na rafiki yako chenge na mijuha wenzio CCM na kuyatupilia mbalini maoni ya hao hao wananchi unao wataja sasa mpumbavu wewe.)) Ninayo ari, ninao uwezo na utayari wa kuiimarisha nchi yetu katika kipindi cha miaka mitano ijayo ya utawala,” alisema Sitta. Katika hotuba yake hiyo, Sitta aliainisha baadhi ya vipaumbele na kuwa kimojawapo ni kupambana kwa nguvu zote na vitendo vya rushwa kiasi kwamba akifanikiwa kuingia madarakani atatenganisha masuala ya siasa na biashara.((wewe mwenyewe mla rushwa utaitegenisha vipi hiyo rushwa na wewe ndio chakula chako...??))
Akifafanua kuhusu hilo, Sitta ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanganyika alisema rushwa kubwa zimekuwa na athari mbaya kwa uchumi wa nchi yetu ambapo mikataba mibovu ya huduma na mauzo, manunuzi hewa, manunuzi yaliyojaa unyonyaji, uteuzi wa wazabuni kwa rushwa na hata rushwa katika ajira, vimesababisha hasara ya matrilioni ya fedha kwa taifa.((sasa wewe siulikuwa madarakani miaka kumi na kikwete kwenye hiyo hiyo mirushwa namikataba mibovu nini umesema bungeni kuhusu hilo..? kimya unakula ukinenepa sasa ndio unajidai kuwadanganya wananchi...?)) “Uchumi unakosa afya kutokana na kubanwa na rushwa ambayo sasa imeenea mijini na hata vijijini...kwa hatua ya kwanza hatuna budi kutenganisha biashara na uongozi.((sasa kwa nini hukumshauri kikwete kutenganisha biashara na uongozi...? mpaka leo unataka kuwa raisi ndio unakuja na ahadi hii....? "Mtu achague kimoja; biashara au uongozi wa siasa. ((hahahaahaha bora nicheke kwanza hahahahaha yani huyu sitta anaona watu wajinga kweli kweli.)) Ikiwa mfanyabiashara atataka kuingia katika uongozi wa siasa itabidi akabidhi mali na biashara zake kwa mdhamini atakayeendesha biashara hizo wakati mhusika anatumikia Umma,” alisema Sitta.
Aliongeza kuwa kwa sasa baadhi ya wanasiasa na watumishi waandamizi serikalini wanatumia nafasi zao kujitajirisha kupitia kujipendelea na kuwa jambo hilo lina athari zake ikiwemo; kuchochea rushwa na usumbufu kwa wananchi; kupunguza ari ya wafanyabiashara wa dhati na kudumaza uwekezaji. Sitta alitaja hatua nyingine katika kukabiliana na rushwa kuwa ni kutunga sheria mpya zilizo kali na ambazo zitakuwa na matokeo ya kumzuia mtu asitamani kusaka rushwa, mali za viongozi zitamkwe kwa uwazi, mali isiyolingana na kipato na kukosa maelezo ya kutosheleza itaifishwe, kesi za rushwa ziwe na utaratibu wenye uwazi na tume inayoshughulikia maadili ya viongozi ipewe nguvu kubwa za uchunguzi na ufuatiliaji wa mali za viongozi bila kuzuiwa na mamlaka yeyote. “Sambamba na kupiga vita rushwa, hatuna budi kuchukua hatua kali dhidi ya hujuma za uporaji wa maliasili za nchi na rasilimali zake. "Madini, misitu, vyanzo vya maji, bahari, maziwa namito ni rasilimali ambazo zisipotunzwa zitatishia uendelevu wa uchumi kwa vizazi vijavyo, kwa hivyo uhalifu dhidi ya maliasili na rasilimali za nchi itabidi uwekewe sheria na taratibu kali,” alionya Sitta. ((huna lolote umeka madarakani miaka mingapi lini ulisimama bungeni ukasema kuhusu madini yawafaewananchi munaiba nyinyi mukijitajirisha nyinyi na familia zenu.))
Akieleza kuhusu vipaumbele vyake vingine, Sitta alisema kwa maoni yake kipindi cha miaka mitano ijayo kina mwelekeo wa mifarakano katika masuala ya Muungano, kutetereka kwa mshikamano kunakotokana na chokochoko za siasa za ushindani, udini na kupanuka kwa tofauti ya kipato na ongezeko la kundi kubwa hususani la vijana mijini lisilo na uhakika wa ajira.
wewe na fitina zako usio juwa lolote zaidi ya fitina na ubaguzi kisha uwe raisi utauwa kila mtu
Kutokana na hali hiyo, alisema atatumia mchanganyiko wa uzoefu wa uongozi kutanzua changamoto hizo ikiwemo ya Muungano feki. Kuhusu hilo la Muungano feki alisema kwa sasa zinajitokeza kauli na vitendo ambavyo vinaashiria kutaka nchi mbili zilizoungana zitengane. “Kutoka Zanzibar, tunashuhudia wanasiasa wanaodai kuwa Zanzibar itanufaika zaidi ikirejea kuwa na uhuru kamili bila kuwa ni sehemu ya Muungano.((Ni kweli maana miaka 50 ya muungano nchi ya Zanzibar imenufaika na nini...? baa,madisco,pombe,mauwaji,wamasai,dawa za kulia mende na panya,wauza jugu,wezi,majambazi,rushwa,malaya,omba omba,madawa ya kulevya,kubakwa,magesti house ya kufanya ulanisi, n.k. "Baadhi ya wabara ((usiseme wabara sema watanganyika unaona haya nini kutamka jina tanganyika)) nao wanawatazama ndugu zao wa Zanzibar kuwa ni wakorofi wasioridhika na chochote kitakachofanywa na Muungano na wanahisi kuwa mfumo wa Muungano uliopo unaipendelea Zanzibar ili hali baadhi ya Wazanzibari nao wanadai kuwa Bara inapendelewa.”  ((usiseme wabara wala bara sema watanganyika unaona haya nini kutamka jina tanganyika))
Sitta alijinadi na kujidai kuwa kiongozi anayeweza kuzileta pamoja kambi hizi na kuuokoa Muungano hana budi kuwa na ufahamu mzuri wa kutosha wa asili, misingi na manufaa ya Muungano.“Ushiriki wangu katika serikali yetu tangu awamu ya kwanza ya uongozi wa nchi yetu unaniweka katika nafasi nzuri ya kuongoza mchakato utakaowezesha kuzijadili na kuzipatia ufumbuzi changamoto za Muungano.” Kipaumbele kingine alitaja ni kuhusu mchakato wa Katiba ambapo alisema licha ya mwafaka kamili kuhusu katiba mpya kutofikiwa, lakini Katiba Inayopendekezwa ina maeneo mengi ya msingi ambayo yanaweza kutuleta karibu ikiwa ni hatua ya awali inayowezesha kusonga mbele kwa amani.((yagujuuuuuu)) Jingine atakalolipa kipaumbele ni kujenga mfumo wenye motisha kwa wote ili kuchochea uchumi endelevu na wa viwanda kukuza uchumi wa nchi kwa kasi inayopunguza umasikini kwa haraka. Aliongeza kuwa wafanyabiashara wakubwa wa ndani hawawekezi vya kutosha ndani ya nchi ili kuleta maendeleo ya haraka ya huduma, viwanda, kilimo na biashara na kuwa baadhi yao baada ya kuchuma fedha wanazihamishia nje ya nchi huku watendaji serikalini wakiwatazama wafanyabiashara hawa kuwa hawana uzalendo na ni wakwepa kodi na wana mazoea ya kutoa rushwa.((unajisema mwenyewe maana wewe ni moja katika walio kuwa katika serekali kwa hiyo umekula marushwa na kujiwekea fedha za kutosha ili uwarubuni watanganyika katika kampeni hizi za kuwa raisi sio...??))
Sitta anakuwa mwanasiasa wa kumi kutangaza nia ya kuwania urais huku baadhi yao wameshachukua fomu za kuwania urais kwa tiketi ya CCM. Waliotangaza nia na kuchukua fomu ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri wa Kilimo, Chakula la Ushirika, Stephen Wassira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya, Mbunge wa Afrika Mashariki, Charles Makongoro Nyerere na mwanadiplomasia mkongwe ambaye kwa sasa ni Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) katika Marekani, Amina Salum Ali. Wengine waliotangaza nia ni Balozi mstaafu, Ali Abeid Karume, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo escrow, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba,mpaka kamasi na gaga la puwa yake mtanganyika mwenzake Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi Kigwangallah.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment