Friday, June 26, 2015

VUAI ALI VUAI AJIVUA NGUWO MWENYEWE NA KUBAKI UCHII ((TUACHIWEEEE TUPUMUWEEEE WAZANZIBARI))


Pamoja na mchanganyiko wa wageni kutoka nchi mbali mbali wanaoishi katika nchi ya Zanzibar, bado inabakia kwamba ukimkuta mtu anaejinasibu kwamba yeye ni Mzanzibar akiwa amevaa nguo nusu uchi ama zinazo onyesha sehemu zake za siri basi kwa jamii ya Kizanzibari iliyomzunguka basi hiyo huwa ni laana kwake ambayo amejisababishia mwenye.
Nasema hivyo kwa kuwa jana tarehe 24/06/2015, nilimsikia kwa mbali Vuai Ali Vuai ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi nchini Zanzibar akijivua nguo mwenyewe hadharani na kujisukumizia laana yeye mwenyewe, tukio hilo lilitokea pale alipo zungumza na waandishi wa habari kuhusiana na baada ya Mawaziri wanaounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutoka upande wa chama cha CUF pamoja na Wawakilishi wote wa Chama hicho kuamua kutoka katika baraza la wawakilishi, baraza ambalo ndio kitovu ama chombo kinachotumika kutunga sheria za nchi pamoja na kujadili mambo yanayowahusu wananchi.
Kitendo alichokifanya Vuai cha kuzungumza na waandishi wa habari na kuwaambia kwamba analaani kitendo walichokifanya Mawaziri na Wawakilishi wa CUF akimaanisha kutoka kwao katika baraza la wawakilishi mimi nasema ni laana, mimi nasema hapa Vuai anajivua nguo na kujilaa nishaa mwenyewe, ukichukulia suala hili ukalivalisha mfano wa imani zetu za kidini, iwapo wewe ni baba mzazi ndani ya nyumba yako una watoto, na ukaamua kutowashughulikia watoto wale ilhali mungu amekupa uwezo wa kuwahudumia, basi watoto wale watanyonga roho zao na hapo huenda ukapata laana kwa tendo lile, nimetoa mfano huo kwa kuwa Vuai na chama chake CCM ingawa CUF ni mshirika katika Serikali lakini yeye hapa ndiye baba wa nyumba hii ya Zanzibar, na kwenye baraza la Wawakilishi ndio matatizo ya wananchi yanapojadiliwa, sasa anaposema kwamba pale hapakuwa pahala pa kujadili matatizo wanayoyapata wananchi katika zoezi zima la uandikishwaji wa wapiga kura wapya, madhila wanayoyapata na kero mbali mbali sasa wapi likajadiliwe......???
Bado naendelea kusema kwamba Vuai amejivua nguo hadharani mwenyewe na hapa sikosei, kwa Mzanzibar mwenye upeo mdogo wa kupambanua mambo basi hapati shida ya kulitafakari hili na atathibitisha kwamba ni kweli Vuai amefanya hivyo, alisikika akisema kwamba, “Sisi CCM tuligundua mapema mpango uliopangwa na CUF wa kuwazuilia wafuasi wa CCM wasiandikishe badala yake wahakikishe wao CUF wanaandikisha kwa wingi”, sasa hapa pana suala la kujiuliza ikiwa wewe ni chama unaeshika dola, wewe ndiye mwenye kutoa maamuzi ya juu katika nchi hii, kama uliligundua hili kwa nini usilizungumze kabla ya zoezi kuanza.....??  ingekuwa busara kama wangelifanya mkutano wa pamoja na wenzao wa CUF kuwaeleza kugundulika kwa mpango huo, au hata wangezungumza na waandishi wa habari kama wenzao wa CUF wanavyofanya mara wanapogundua jambo lolote linalowakwaza, lakini kwa kauli kama hii bado narudia kwamba amejivua nguo mwenyewe na asubiri laana, kwani kama kweli mpango huo ulikuwa unafanyika na CUF wa kuwazuia wafuasi wa CCM wasijiandikishe, basi wawakilishi wa CCM kule barazani walitakiwa waunge mkono ile hoja ya dharura iliyowasilishwa barazani ijadiliwe, kwa kuwa pande zote zilikuwa zina lawama zinazofanana, hapo tungesema kweli tumewatendea haki wananchi kwa kuwa tumejadili kuhusiana na kero wanazo zipata katika uandikishwaji na kutatua kero zao hizo.
Malalamiko waliyoyatoa CUF katika chombo cha kutunga sheria za nchi hii yaani Baraza la Wawakilishi na kudharauliwa na Kiongozi wa Baraza Hilo Spika Pandu Ameir Kificho, mimi nasema ni madai ya msingi na yenye ukweli kwa asilimia nyingi, kwa kuwa CUF hawajaanza leo kudai malalamiko hayo, kwa kauli ya Katibu Mkuu wa CUF ambaye pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad, malalamiko hayo yalishapelekwa katika Baraza la Mapinduzi, yalishawasilishwa kwa Shein ambaye yeye katika utawala wake ni kukaa kimya hata katika mambo muhimu ya nchi, yalishazungumzwa mara kadhaa katika mikutano ya hadhara ili kuwatanabahisha wananchi.
Na kama haitoshi Maalim Seif Shariff Hamad kwa kuonyesha wasiwasi wake juu ya hili aliona ni busara akauhutubia ulimwengu siku ya tarehe 10/05/2015 pale katika ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel Dar-Es-Salaam nchini Tanganyika, pale alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kadhia hiyo hiyo, ambayo CCM iliwakera sana, ndipo Vuai huyu huyu akasimama katika mkutano wa hadhara uliokuwa na wafuasi si zaidi ya 50 kwa mikoa mitatu kwa mikoa mitatu ya Unguja kujibu hoja za Maalim Seif Shariff Hamad na kumlamu kwa nini akafanya hivyo na kutoa rai mbadala kwamba, alitakiwa awasilishe malalamiko hayo kwao kwa kuwa wao ni washirika katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa jambo ambalo Maalim Seif Shariff Hamad alipohojiwa na Mohammed Abdurahman wa Sauti ya Ujerumani kwa kuwa Maalim Seif Shariff Hamad yuko juu Kisisiasa kama mlima kilimanjaro kumzidi Vuai Ali Vuai aliyekichuguu alisema kwamba hatua hizo alishazipita na hakuna muafaka uliofikiwa.
Haikuishia hapo nayo tume ya Uchaguzi ya ZEC, kupitia Mkurugenzi wake Salim Kassim Ali tarehe 11/06/2015, akajariibu na yeye pia atii kujibu hoja za Maalim Seif Shariff Hamad na alikataa yote ambayo aliyazungumza Maalim Seif Shariff Hamad wa CUF kama alivyokataa Vuai katika mkutano wa hadhara na ule wa waandishi wa habari mara baada Maalim Seif Shariff Hamad kutoa malalamiko yake mbele ya waandishi wa habari.“Kama kweli ana ushahidi wa kile anachokizungumza, kwa nini haleti malalamiko yake ZEC badala yake analalamika kwenye vyombo vya habari.....??” nukuu hii ilitolewa na ndugu Salim Kassim Ali siku ya tarehe 11/05/2015, na mfano wa nukuu kama hii ilitolewa na huyu Vuai Ali Vuai katika mkutano wake katika viwanja vya kwa Mabata, sasa kama CUF kupitia kwa wawakilishi wake waliamini kwamba Baraza la Wawakilishi ndipo miongozi mwa vikao vya Serikali hufanyika, ZEC nayo ni miongozi mwa taasisi za Serikali ambayo ZEC imekabidhiwa jukumu la kuendesha shughuli zote za Uchaguzi wa nchi ya Zanzibar, na katika nchi kuna malalamiko yanayoihusu Serikali kupitia ZEC, hivyo hakukuwa na ajabu wala aibu wala sababu ya kulaani kuwasilishwa kwa hoja binafsi inayohusu malalamiko juu ya Uandikishwaji, kwani ZEC ni taasisi ya Serikali na Baraza la Wawakilishi ni Sehemu ambayo matatizo ya Wananchi hujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi pamoja na kutungiwa Sheria.
Rai yangu, kama Vuai atakuwa ni mkweli aligundua njama alizozisema juu ya CUF pale aliposema kwamba wao waligundua mapema mpango wa CUF wa kuwazuilia wafuasi wa CCM wasijiandikishe, na CUF walishalalamikia mara kadhaa, hadi juzi kuamua kuliancha Baraza la Wawakilishi likiwa na wajumbe wa upande mmoja kitendo kilichichafua nchi ya Zanzibar na Serikali ya Shein, kitendo ambacho kwa mara ya pili kinatokea katika serikali ya Shein, ambapo hakijawahi kutokea katika awamu zilizopita, ni vyema Shein aakhirishe ufungaji wa baraza siku ya 26/06/2015, badala yake aunde Tume ya Muda mfupi kuchunguza tuhuma hii, ikiwa litafanyika hili nililoshauri basi tutakuwa tunaitengenezea jina na hadhi mpya ya nchi yetu ya Zanzibar. Lakini hili nililoshauri likifanyika ama lisifanyike bado Vuai ataendelea kujivua nguo mwenyewe hadharani na kujilaani hadi atakapoamua kuzivaa.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment