Saturday, June 27, 2015

VIDEO-WAZIRI OMAR SHARI AKIZUNGUMZA NA WANA HABARI KUHUSU UWEKAJI CAMERA


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha mradi mkubwa wa kiulinzi  katika maeneo mbali mbali ya Miji na mitaa nchini Zanzibar katika kukabiliana na vitendo  atii vya uhalifu vinavyoendelea kuongezeka kila siku. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum Haji Omar Kheir ameeleza hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Vuga Mjini  nchini Zanzibar.

Alisema katika siku za karibuni hapa nchini Zanzibar tumeshuhudia vitendo vya uhalifu ikiwemo ujambazi, uporaji, hujuma, kuwamwagia watu tindikali pamoja na matokeo ya uchomaji moto mali za umma, taasisi na watu binafsi. Hali hiyo imeleta wasi wasi mkubwa atii kwa wananchi na wageni wanaoitembelea nchini Zanzibar  kitu ambacho kinaweza kuathiri biashara ya Utalii inayoingiza fedha nyingi za kigeni.((fedha nyingi za kigeni mbona hatuzioni kujengea nchi badala yake mnajitajirisha nyinyi ni wazi munalinda matumbo yenu tu))

Alieleza kuwa mradi huo utahusisha uwekaji wa Kamera za kiulinzi katika maeneo yote ya Mji Mkongwe na baadhi ya maeneo ya kuingiilia mji wa nchi ya Zanzibar na maeneo yenye taa za kuongezea magari. Alizitaja Kampuni ya Raviltalco ya Romania na Rome Solutions iliyosajiliwa Zanzibar kuwa wamepewa kazi hiyo na zaidi ya kamera 900 zitafungwa katika maeneo hayo.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment