Sunday, August 30, 2015

POMBE MAGUFULI ASEMA MKICHAGUWA UKAWA NCHI TANGANYIKA ((TZ)) ZANZIBAR ITAGEUKA LIBYA-CCM POLENI SANA ASIYEKUBALI KUSHINDWA SIO MSHINDANI


Kauli za fujo na uchochezi zinaendelea kutolewa kupitia viongozi wa chama cha mapinduzi,mgombea urais wa Tiket ya CCM Ndugu John Pombe Magufuli kwa mara nyengine amesema kuwa ,wananchi wasifanye maamuzi magumu kuichagua ukawa ifikapo October badala yake waichague CCM au nchi itageuka kama Libya na wa Tanzania watageuka wakimbizi ndani ya nchi yao.
Hii ni mara ya Pili kutoa kauli hiyo katika kampeni zake za uchaguzi,akiripotiwa na televisheni ya ITV.
Kauli hii ni mfululizo wa kauli za viongozi wa juu wa CCM akiwemo Rais Kikwete na Lukuvi waliponukuliwa kuwa Jeshi litachukua nchi ikiwa wapinzani watashinda.
Baadhi ya wananchi waliohojiwa wameeleza masikitiko yao kwamba hakuna kiongozi yoyote aliekemea kauli hiyo ya uchochezi na wanaamini kuwa CCM wamekusudia kuharibu amani kwa njia yoyote endapo watashindwa katika uchaguzi..
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Wednesday, August 26, 2015

SASA TUMEMUELEWA MKAPA KUITA VIONGOZI WA UKAWA WAPUMBAVU NA MALOFAA KUMBE WAPUMBAVU NA MALOFA NI SISI TULIO IWACHA CCM KUTAWALA KWA MIAKA 50 BILA YA MAENDELEO YOYOTE

Kumbeeeeeee….!!!
sasa nimemfahamu Bwana Ben Mkapa alivyowaita wanaotaka mabadiliko kuwa “wapumbavu” na “malofa”,
1. Mkapa aliondoka dola inauzwa 650, leo hii anatakiwa amnadi Magufuli dola ikiwa inauzwa 2000+, si upumbavu huo na ulofa...???
2. Mkapa aliondoka akaacha sarafu za shilingi 5, 10, 20, leo anamnadi Magufuli hizo hazipo tena kuna sarafu ya jero (500), si upumbavu na ulofa huo...???
3. Mkapa aliondoka nauli ya dala dala Tsh. 250, leo anamnadi Magufuli nauli Tsh.450, si upumbavu na ulofa huo...???
4. Mkapa aliondoka kilo ya sukari ni Tsh. 400 tu, leo anamnadi Magufuli kilo ya sukari Tsh.2000, si upumbavu na ulofa huo...???
5. Mkapa aliondoka fungu la nyanya au tomato ni Tsh. 100 tu, leo anamnadai Magufuli fungu la nyanya ni Tsh. 500-1000, si upumbavu huo na ulofa...???
6. Mkapa anaondoka kilo ya mchele Tsh. 800 tu, leo anamnadi Magufuli kilo ya mchele Tsh. 1800, si upumbavu na ulofa huo???KIBANDA MAITI NCHINI ZANZIBAR MKUTANO WA CCMsasa kama tumevumilia hali hii kwa miaka 10 ya JK, leo vipi tukatae mitano mengine ya Magufuli...??? kama huo si upumbavu na ulofa ni nini...??? kwanini tusikatae tokea mitano yapili ya JK...???Mipumbavu nyie na Milofa!!! MKUTANO WA CCM JANGANI JIJINI DAR ES SALAAM NCHINI TANGANYIKA.Wenzenu Marekani Uwengereza au nchi za Ulaya hawakai na chama miaka 20 hata kiwe kizuri vipi, wao Matajiri wana kila kitu nchi zao nzuri ile mbaya zimejengwa zikajengeka, nyinyi mnakaa na chama miaka 50 umasikini upo pale pale, bado chama hicho kinakuja na ilani na ahadi....???pumbaaaaaaav na malofaaa
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

LOWASSA NA DUNI WAAMUWA KUWATEMBELEA WAPUMBAVU NA MALOFA WENZAO KILA MAHALI KWENYE DALADALA MPAKA MITAANI


WAKATI mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, akizindua kampeni zake juzi jijini Dar es Salaam kwa mkutano wa hadhara, mpinzani wake mkubwa ambaye ni mgombea wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, ameanza kwa mtindo wa aina yake wa kuwafuata wananchi mitaani. Katika hali ambayo haijazoeleka katika siasa za Tanzania, jana Lowassa alifika kwenye kituo cha daladala kili-chopo eneo la Gongo la Mboto, Ilala jijini Dar es Salaam saa 1:50 asubuhi, na kusalimia wasafiri na wafanya-biashara mbalimbali wanaofanya shughuli zao eneo hilo. Takribani dakika 21 ambazo Lowassa alizitumia kwenye eneo hilo, zilitosha kujaza mamia ya wananchi kila mmo-ja akitaka kumsalimia.
Lowassa anayewania nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aliwasili kituoni hapo akiwa na gari aina ya Noah yenye namba T 607 DDR. Mara baada ya gari hilo kusimama kituoni hapo na Lowassa kushuka, baadhi ya watu waliokuwa eneo hilo walionekana kupata mshangao kutokana na ziara hiyo ya kushtukiza, wakiwa hawaamini wanachokiona, huku wengine wakishangilia. Muda mfupi baada ya Lowassa kufika akiwa na mgombea mwenza, Juma Duni Haji, baadhi ya watu waliacha shughuli zao na kufurika kwenye eneo hilo. Kwa madereva wa bodaboda na daladala, walisitisha shughuli zao na kusogea eneo hilo huku wakishangilia kwa kusema ‘rais… rais… Lowassa… Lowasssa’ na kupiga miluzi.
Kadiri Lowassa alivyokaa kwenye eneo hilo, watu waliendelea kufurika huku baadhi yao wakisema tangu taifa hili lipate uhuru, hawajawahi kushuhudia kiongozi mkubwa akiwatembelea kwenye maeneo yao. “Hata waziri mwenyewe hajawahi kuja huku,” alisikika mmoja wa wananchi wa eneo hilo akisema na kuongeza: “Baba wewe ndiye unafaa, na miaka yote tulikuwa tunamhitaji mtu wa aina yako.” Pia baadhi ya wananchi walisikika wakimweleza kwamba akifanikiwa kuwa rais, wanaitaka Katiba ya Jaji Joseph Warioba. Katika hali ya kushangaza, mwanafunzi mmoja aliibuka na kumfuata Lowassa, huku akimwambia kuwa anacho kichinjio – kitambulisho cha kupigia kura.
Ilipotimia saa 2:11 asubuhi, Lowassa alipanda daladala yenye namba za usajili T 917 CWS inayofanya safari zake kati ya Buguruni na Nzasa na kwenda nayo hadi eneo la Pugu Shule ambako alifika saa 2:24 asubuhi. Wakati anapanda ndani ya daladala hiyo, wananchi walijazana eneo hilo walizidi kupatwa na mshangao, wengine wakisema hawaamini wanachokishuhudia. Kitendo hicho kilisababisha baadhi wa wananchi kuvamia daladala hiyo na kupanda, huku wengine wakipitia madirishani kutokana na msongamano wa kugombania ulivyokuwa mlangoni.
Wananchi hao walijaa kwenye daladala hiyo hadi wengine wakaning’inia mlangoni na kisha kuanza safari yake kuelekea Pugu. Kitendo cha daladala hiyo kuondoka eneo hilo, vijana waendesha bodaboda walianza kuifuata kwa nyuma na wengine wakitangulia mbele yake. Baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye kituo hicho, nao waliifuata daladala hiyo wakikimbia hadi Pugu, takribani umbali wa mita 400. Akiwa ndani ya daladala hiyo, Lowassa aliyekuwa ameketi kiti kimoja na mwanafunzi, alitoa Sh 2,000 kwa ajili ya nauli yake na abiria waliokuwa karibu naye. Baada ya kufika katika eneo hilo la Pugu Shule, Lowassa alishuka na kupanda kwenye gari lake ambapo msafara uliendelea hadi Mbagala Rangi Tatu.
DEREVA WA DALADALA ANENA
Akizungumza na MTANZANIA, dereva wa daladala hiyo, Steven Zunga, alisema amefurahi sana kwa kitendo cha mgombea huyo wa Ukawa kupanda gari lake. “Furaha niliyonayo siwezi kuelezea, nimefurahi sana… sijui kama leo nitalala, sikutegemea kama siku moja ningemwendesha Edward Ngoyai Lowassa. Imeingia katika historia yangu na nitaiandika kwenye kumbukumbu zangu,” alisema dereva huyo.
AWASILI MBAGALA RANGI TATU
Lowassa ambaye pia aliongozana na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja, aliyeku-wa Mbunge wa Arumeru Magharibi, Gudluck Ole Medeye na Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanza-nia, Sheikh Rajab Katimba, aliwasili katika eneo la Mbagala Rangi tatu saa 4:06 asubuhi. Kabla ya kuwasili Lowassa, eneo hilo lilijaa umati wa watu kutokana na madereva wa bodaboda ambao walikuwa wakiwasiliana na wenzao kwamba waziri mkuu huyo wa zamani atafika katika eneo hilo.
Baadhi ya wananchi walimwomba Lowassa ashuke kwenye gari angalau aseme neno moja tu waridhike na baada ya kelele hizo kuzidi, alishuka na kuwapungia mkono. Kitendo hicho kiliwafanya wazidi kulipuka wakisema wanataka kusikia chochote kutoka kwake.
JUMA DUNI ALIPUKA
Kutokana na ombi hilo la wananchi hao, saa 4:12 asubuhi Duni alishuka ndani ya gari na kupewa kipaza sauti na kuwaambia wananchi hao kuwa wamepita kuwasalimia na kuwapa pole malofa na wapumbavu wenzao.
“Sisi tumepita kuwasalimia ninyi malofa na wapumbavu wenzetu, leo tumeamua tuamke asubuhi na mapema kuja kuwasalimia. Tusije tukaambiwa tumeitisha mkutano ambao hauna ruhusa. “Tumepita kuwasalimia ninyi wanyonge wenzetu mnaoitwa kila aina ya majina, mara vibaka na wahuni. Sasa sijui masikini anayetafuta riziki kuitwa majina hayo, lakini tunaomba mtuache leo tutakutana Jumamosi pale viwanja vya Jangwani,” alisema Duni huku alishangiliwa na umati huo wa watu. Pamoja na hilo, pia aliwaambia kwa muda huo wakutane Dar Live kwani Lowassa angeendelea kuwatembelea wafanyabiashara na kero wanazozipata abiria katika vituo vya daladala. Kitendo hicho kilisababisha wananchi hao kukimbilia msafara huo huku wengine wakiacha shughuli zao, lakini ilishindikana Lowassa kusimama katika eneo hilo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mazingira hayakuruhusu.
MSEMAJI WA LOWASSA ANENA
Msemaji wa Lowassa, Abubakari Liongo, alisema lengo la ziara hiyo ni kujifunza kuhusu kero ambazo wanazipata wafanyabiashara, abiria pamoja na foleni katika Jiji la Dar es Salaam. “Lengo la ziara hii ni kuangalia uhalisia wa tatizo la usafiri Dar es Salaam, wafanyakazi wanaamka asubuhi wanachelewa kufika kazini, wanafunzi nao vivyo hivyo, ndiyo maana ametoka Gongo la Mboto hadi Mbagala kujionea hali ilivyo, lakini pia ametumia fursa hii kuzungumza na wananchi na wafanyabishara ndogondogo ili awasikilize shida zao,” alisema Liongo.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Tuesday, August 25, 2015

MGOMBEA URAISI KWA TICKETI YA CHAMA CHA CCM POMBE MAGUFULI AAHIDI KUWASHUGHULIKIA MAFISADI BASI ANZA NA HAO WA EPA NA ESCROW


Rais Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na Mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere wa nchi ya Tanganyika, Makongoro Nyerere wameshambulia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).  Wakizungumza kwa zamu katika Uwanja wa Jangwani jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua kampeni za chama hicho wamesema, mgombea wa UKAWA hana sera za wapinzani.Katika mkutano huo uliotawaliwa na vijembe kwa UKAWA Rais Kikwete bila kutaja jina amesema, katika umoja huo kuna mgombea anayesimama kama mgombea binafsi kwa kuwa, sera zake ni tofauti na chama anachosimama kugombea. Alikwenda mbali na kuonesha kushangazwa kuwa, mmoja vyama viwili ambavyo sio msingi wa chadema ndio vimesimama katika ngazi ya urais na mgombea mwenza wake.

Rais Kikwete aliwalenga Mgombe Urais wa Chadema, Edward Lowassa aliyejiunga na chama hicho akitokea CCM pamoja na Juma Duni Haji aliyejiunga na Chadema akitokea Chama cha Wananchi (CUF). “Wagombea sio wa Chadema. Mmoja ni CCM na mmoja ni CUF.., Pale kuna mgombea urais ambaye unaweza kusema kama mgombea binafsi maana ana sera zisizofanana na chama,” amesema Rais Kikwete na kuongeza “lakini wameyataka wenyewe.”
Hata hivyo Kikwete hakumwacha Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye aliyejiunga na chama hichi siku moja iliyopita. Kikwete amesema, pamoja na Sumaye kujieleza lakini hakumwelewa alichokuwa akikusudia “nimejaribu kusikiliza anasema nini lakini sikuelewa kabisa,” amesema. Hata hivyo amesema, CCM haikubahatisha kumteua Dk John Magufuli kuwa mteule wa chama hicho katika urais na kwamba, “tumemweka kwa sifa zake, tunataka rais anayeipenda nchi na anayependa wananchi wa nchi hii.”

“Magufuli anayo sifa hiyo. Tumesema, hatutaki kuchukua mgombea mwenye makando kando mengi na tukatumia muda wetu mwingi kujitetea sisi na yeye kabla ya kuomba kura. Tunamtaka mgombea mwaminifu, mwadilifu. Safari hii Mungu kamchagua Magufuli.” Kabla ya Rais Kikwete kuzungumza, alitanguliwa na Mkapa ambaye amesema, kuna vyama vinawadanganya Watanganyika ((Watanzania)) Wazanzibari kuwa wanawatafutia ukombozi-wapumbavu. “Kuna chama kimoja tu cha ukombozi hapa Tanganyika ((Tanzania)) Zanzibar, ni CCM iliyotokana nas ASP na TANU. Kuna vyama vinawadanganya Watanganyika ((Watanzania)) Wazanzibari eti wanataka kuwakomboa wananchi-wapumbavu, nenda nchi zote za jirani uliza chama cha ukombizi Tanganyika ((Tanzania)) Zanzibar watakwambia CCM. Nina kila sababu ya kusema wapumbavu,” amesema. Hata hivyo amesema, haitoshi kusema mtu anauchukia umasikini peke yake. “Haitoshi kusema unauchukia umasiki, lazima useme unauchukiaje umasikini?” amesema Mkapa.

Lowassa katika hotuba zake mbele ya wananchi kwenye safari zake za kutafuta wadhamini alipokuwa CCM na hata baada ya kuhamia Chadema, amekuwa akisema anauchukia umasikini-haupendi. Hata hivyo Mkapa amesema, timu ya CCM ni madhubuti kwa kuwa Magufuli anapenda kushirikiana na wenzake, yupo mstari wa mbele katika kutekeleza mambo yote ya umma na kwamba, wakati wote ni mfano wa tabia nzuri kwa vitendo vyake. Makongoro ndio aliyefungua ukurasa wa mashambulizi kwa UKAWA kwa kumvaa Sumaye baada ya kujiengua CCM.
Makongoro amesema, anamshangaa Sumaye aliyejiunga na vyama vinavyounda UKAWA na kwamba, alipaswa kukubali matokeo ya kushidwa Makongoro alianza kwa kibwagizo “kuna mmoja-au niache?- kuna yule kaka yangu mmoja nasikia afya yake sio kweli. Kuna huyu mwingine wa jana (Sumaye)? “Sumaye tumpige kanzu au tumuache hivihivi, kwani angetulia tungeshughulika naye, kajileta mwenyewe sasa mimi nifanyeje, nimpige tobo?” amesema na kuongeza; “Sumaye akiwa Waziri Mkuu na kaka yangu Kikwete (Rais Kikwete) waliingia kwenye tano bora, Sumaye alikuwemo, kura zake hazikutosha zikatosha za Kikwete, kwa kuwa aliingia tano bora akasema, chama kizuri.

“Miaka 10 baadaye tano bora hakuingia- Sumaye akatuambia mkimpa Lowassa kugombea urais hiki chama mimi nitahama, sasa huyo ni mkweli ama muongo. Hii ndio shida ya kusema uongo, kusema rahisi kuukumbuka tabu,” amesema Makongoro. Katika mkutano huo, mgombea mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan amesema, atasimamia na kuwawezesha akina mama. Pia ameahidi kusimamia pesa Sh. Mil 50 zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kupelekwa vijijini.
“Nitasimamia kuwawezesha akina mama, pesa za vijijini Sh. Mil 50 zitatoka kwa ajili ya vijijini nitazisimamia. Mimba za utotoni nitasimamia kuhakikisha zinaondoka, pia nitahakikisha maji yanapatikana na kusaida akina mama wote,” amesema. Akizungumzia uzowefu alioupata amesema, amekuwa karibu na Makamu wa Rais wa sasa, Dk. Mohammed Gharibu Bilal hivyo hakuna wasiwasi katika nafasi hiyo. “Nilikuwa kwenye mikono mizuri ya Dk. Bilal, najua kazi zilivyo nawahakikishia Ofisi ya Makamu wa Rais itasiamama vyema kutekeleza ilani ya uchaguzi pamoja na muungano,” amesema. 

Dk. Magufuli amewaahidi watanzania kujikita katika kutetea maendeleo ya wananchi kwenye Nyanja zote. Dk. Magufuli amesema utawala wake utajikita katika masuala ya kilimo, afya, uchumi na amani ya nchi. “Watanzania natambua mnapenda kuona mabadiliko, nitasimama vizuri katika miradi ya uchumi. Watanzania nawahakikishia shida na matarajio yenu nayajua, nayafahamu na natambua ninao uwezo wa kuyashughulikia. "Mnataka suala la rushwa, wizi serikalini vikomeshwe haraka. Kwa kuwa palipo na rushwa ufisadi hakuna maendeleo, nitasimamia hilo,”amesema. Amesema, kama atachaguliwa “nitahakikisha naunda mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi na majizi yafungwe haraka.”
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

NCHINI TANGANYIKA CHAMA CHA CHADEMA KIMESEMA ZAIDI YA KADI MILLIONI MBILI ZA KUPIGIA KURA ZINATENGENEZWA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NEC KUISAIDIA CCM USHINDI JE MALOFAA NA WAPUMBAVU NI NANI HAPA...???

mgombea
Mgombea Ubunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea.
Chadema yaituhumu Nec.Mgombea Ubunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, amesema kuwa zaidi ya kadi milioni mbili za kupigia kura zinatengenezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kwa ajili kuongeza kura za ziada za kukiwezesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushinda katika uchaguzi Oktoba 25, mwaka huu. Kubenea alisema tayari amepata kadi 100 ambazo amesema amepatiwa baadhi ya maafisa wa Tume ambao walimuahidi kumpatia kadi nyingine zaidi. “NEC wameweka mkakati wa kukisaidia CCM kupata ushidi katika kufanikisha hilo wametengeneza kadi ambazo hazijajazwa taarifa zozote ambazo wanatarajia kuzitumia kwa kuingiza taarifa za watu ambao hawastahili ili wapige kura,” iliwasaidie na kuongeza:
“Tunashukuru kuna wasamaria wema ndani ya Nec ambao hawakubaliani na hujuma hizo, wameamua kutuambia na wametuahidi kutupa kadi nyingine zaidi, na huyo aliyenipa hizi 100 aliniambia hata nikitaka kadi hizo 100,000 atanipa.” Kubenea alisema tayari amekabidhi kadi hizo kwa mwanasheria na kwamba kabla ya kuzikabidhi, aliapishwa kwanza. “Naomba Nec iache kufanya kazi za CCM, kama itaendelea kufanya hivi itaipeleka nchi kwenye machafuko, tunaomba ifanye kazi kwa uadilifu na ninamuomba Mwenyekiti wa Tume hiyo asiipeleke nchi pabaya, hatutaki kuona watu ambao hawakuandikishwa wanaingizwa kwenye daftari,” HUU NDIO MWISHO WA UROHO WA MADARAKA NA KINGANGANIZI KUTAKA KUENDELEA KUTAWALA JAPO KUWA WATU WASHAKICHOKA CHAMA NA WEWE MWENYEWE PIA KAMA YAMEMPATA GADDAF NA BAGBAO SI AJABU KUWA WAPA TA NYINYI CCM KWA HIYO NYINYI ENDELEANI TU NA KUJIDAGANYA KUWA MNA TUME NEC NA JESHI HAWA WALIKUWA NAVYO HIVYO VYOTE NA LEO HII WAONE WANAVYO IBIKAA.WAPUMBAVU WAKUBWA NA MALOFA WAKUBWA WAROHO WA MADARAKA NA TAMAA YA KUKA MADARAKANI MILELE MUME KWISHA HUU NDIO MWAKA WENU WA MWISHO KUBALINI KUSHINDWA AU LAZIMISHENI MUISHIE ICC NDIO YATAKUWA MALAZI YENU PEMA KAMA ALIVYOHUU NDIO MWISHO WA UROHO WA MADARAKA NA KINGANGANIZI KUTAKA KUENDELEA KUTAWALA JAPO KUWA WATU WASHAKICHOKA CHAMA NA WEWE MWENYEWE PIA KAMA YAMEMPATA CHARLES TAYLOR NA HOSNI MUBAROUK SI AJABU KUWA WAPATA NYINYI CCM KWA HIYO NYINYI ENDELEANI TU NA KUJIDAGANYA KUWA MNA TUME NEC NA JESHI HAWA WALIKUWA NAVYO HIVYO VYOTE NA LEO HII WAONE WANAVYO IBIKAA.alisema. Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji, Damian Lubuva, alisema hawezi kuzungumzia chochote kwa kuwa hajaziona kadi hizo.
“Kama Chadema wamesema kadi hizo ni za kwetu ni vema wangezileta kwetu ili tuone kama kweli ni zetu, kwa kuwa wamezungumza hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari na mimi sijaziona kadi hizo siwezi kuzungumza chochote mpaka nidhibitishe,” alisema Jaji Lubuva na kuongeza: “Hata nikizungumza hapa itaonekana tunabishana Tume na Chadema, wao kama kweli wanazo watuletee tuthibitishe.”
Naye mgombea ubunge wa Chadema Kawe, Halima Mdee, Halima Mdee, aliitaka Tume hiyo kuhakikisha inahakiki taarifa za wananchi katika vituo vya kupigia kura walivyojiandikishia na si katika kata. Alisema taarifa ambazo amepata ni kwamba baadhi ya ofisi za wakurugenzi wameambiwa na Nec kwamba wananchi wao watahakiki taarifa zao katika ofisi za kata na si katika vituo walivyojiandikishia kama inavyotakiwa kutokana na uchache wa vitabu. Jaji Lubuva alisema changamoto za uhakiki wa wapiga kura ni suala ambalo linashughulikiwa kwa kushirikiana na wakurugenzi na kwamba watahakikisha kila aliyejiandikisha anahakikiwa.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Monday, August 24, 2015

PICHA ZA MKUTANO ULIOFANYIKA KIBANDA MAITI NCHINI ZANZIBAR CUF VS CCM KWA CHAAA KWEUPEE TUACHIWEE TUPUMUWEEE TUACHIWEE TUPUMUWEEE TUACHIWEE TUPUMUWEEE WAZANZIBARI

cuf2

cuf1KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

MUUWAJI WA WAZANZIBARI 26-27,2001 AMPIGIA DEBE POMBE MAKUFULI ILI AWEZE KUENDELEA KUWALINDA CCM WAUWAJI NA MAFISADI APE,ESCROW N.K.


Rais  Mstaafu wa nchi ya Tanagnyika iliye waulisha Wazanzibari wengi sana wakati wa utawala wake  wa  awamu  ya  tatu  mh. Benjamini  William  Mkapa  amesema  kuwa  wapinzani  wanaodai  vyama  vyao  ni  vya  ukombozi atii  ni  Wapumbavu  na  malofa  kwa  kuwa  Watanganyika ((watanzania)) Wazanzibari  walikwisha  kombolewa  na  chama  cha  ASP  na  TANU  na  kwamba  chama  pekee  cha  ukombozi  kilichobaki  hivi  sasa  ni  CCM  pekee.

Mkapa  ametoa  kauli  hiyo  leo  katika  viwanja  vya  Jangwani  jijini  Dar  es  Salaam wakati  akimnadi  mgombea  urais  wa  CCM,  John Pombe  Magufuli.anafikiri tushasaha lakini sisi Wazanzibari hatuja sahau na kama alivyo yeye kufuguwa mdomo na kuipigia debe CCM chama cha wauwaji na mafisadi basi nasi tutaendelea kumkumbusha yale mauwaji ya pemba ya wananchi zaidi 35 ya januari 26-27,2001.kwa hiyo mkapa endelea kupiga debe lako kuwa CCM ibaki madarakani lakini kaa ukijuwa ipo siku utakwenda tu ICC kujibu mashataka ya kuwauwa Wazanzibari wasio na hatia yoyote.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

VIDEO-WAZIRI MKUU MSTAAFU,FREDDERICK SUMAYE AONDOKA CCM NA KUJIUNGA NA UKAWA

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

WAZIRI MKUU MSTAAFU,FREDDERICK SUMAYE WA NCHI YA TANGANYIKA AMETANGAZA RASMI KUJIVUA UAWANACHAMA WA CCM NA KUJIUNGA NA UKAWA CCM BYE BYE


WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ametangaza rasmi kujivua uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga kwenye vuguvugu la mabadiliko kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Sumaye ametangaza uamuzi huo leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Legde Plaza uliopo katika Hoteli ya Bahari Beach Jijini Dar es Salaam. “Leo nimeamua kuondoka CCM na kujiunga na UKAWA, uamuzi huu haukuwa rahisi katika familia yangu…, suala la kujiunga na chama gani itajulikana baadaye,” amesema. Amesema, atasaidiana na Edward Lowassa ambaye ni mgombea urais wa Chadema na pia mwakilishi wa UKAWA kufanikisha mageuzi. UKAWA unaundwa na vyama vinne vya upinzani ambavyo ni Chadema yenyewe, Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha NCCR-Mageuzi na NLD. Sumaye amesema, Lowassa amekaa kwenye nafasi mbalimbali za utawala ndani ya serikali hivyo anastahili nafasi hiyo na kwamba, hana tatizo na utendaji wa mgombea urais kupitia CCM, Dk. John Mgufuli lakini sio katika ngazi ya urais.
“Sina tatizo na Magufuli, naamini hakuhonga na ni mchapakazi lakini ana mapungufu mengi katika nafasi hiyo (urais),” amesema.

Mkutano huo wa Sumaye na waandishi wa habari pia umehudhuriwa na Lowassa, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Naibu Mkurugenzi wa Mipango, Siasa na Bunge wa CUF, Shaweji Mketo na viongozi wengine wa UKAWA. Tayari Lowassa na mgombea mwenza wake Juma Duni Haji jana wamerudisha fumu za kugombea urais kwenye Ofisi za Tume ya Uchaguzi (NEC) na kukidhi vigizo vilivyowekwa. Hatua ya Sumaye kuhama CCM inakuja ikiwa ni siku moja kabla ya Dk. Magufuli kufungua rasmi kampeni ya chama chake kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu. Kwenye mkutano huo Sumaye ambaye aliongozana na mkewe Esther Sumaye pamoja na wana familia wengine amesema, anaondoka kwenye chama hicho ili kuongeza nguvu ya upinzani. “Siji upinzani kufuata cheo, nakuja kuimarisha nguvu. Sijadai cheo wala fedha. Nipo tayari kusaidia upinzani ili uwe na nguvu,” amesema Sumaye na kuongeza: “CCM imezubaa, inajifanya itashinda. Wananchi wanataka mabadiliko na hatuwezi kuwaacha hivi hivi, sisi wenye uchungu na nchi hii hatuwezi kuwaacha hivi hivi. Nimekuja huku ili kuongeza nguvu ya mabadiliko.” Hata hivyo Sumaye amewataka wanachama wa CCM pamoja na watumishi wa serikali walio tayari pia wajiunge na UKAWA ili kuhakikisha wimbi la mageuzi linafanikiwa.

“Mimi sijui kama ni mmoja wa wale walioitwa makapi, ningejua ningetoka mapema…, sitoki CCM kwa hasira ya kutoteuliwa, kumchukia mgombea urais wa CCM, kuchukia uongozi wa juu wala kudhoofisha CCM, badala yake natoka ili kuimarisha CCM,” amesema. Akifafanua kauli hiyo amesema kuondoka kwake CCM na kuimarisha nguvu ya UKAWA kutaisaidia CCM kutolala na kuongeza nguvu ili kupambana na vyama vya upinzani. Amesema, wana CCM hawapaswi kusikitika kwa yeye kuhama chama hicho kwani ni mtu wa kawaida ndani ya chama hicho na kwamba, hana cheo chochote. “Wana CCM hawana sababu ya kulalamika, mimi ni sisimizi ndani ya CCM, sina nafasi yoyote hata ujumbe wa tawi,” amesema na kuongeza, chama hicho hakikuona umuhimu wake na pengine kitauona baadaye. Hata hivyo Sumaye amesema, hakuhama kwa sababu ya kumfuata Lowassa kwa kuwa, ametoka Kaskazini, “lakini pia si kwa sababu Mbowe ni mtu wa Kaskazini,” isipokuwa ni kuimarisha mageuzi. Hata hivyo ameoneshwa kutishwa na wimbi la mageuzi nchini na kusema “wimbi hili kulizuia si kazi rahisi.”

Sumaye ameshutumu vikali hatua ya wachache kuharibu taratibu za CCM katika kupata mgombea urais kupitia chama hicho na kuwa, alijua mapema kwamba jina lake halitafika mbali. Anasema, hana tatizo na mfumo wa kupata wagombea isipokuwa tabia ya watu wachache kwenda na majina ya wagombea kinyume na taratibu za chama. “Katika mfumo huu mtu mwenye nafasi ya juu na anataka akuingize anaweza kufanya hivyo na kama hataki anakuondoa. Mfumo huu ni mbuvu, safari haya yametokea sana. “Rais, katibu mkuu hana nafasi ya kuweka mgombea. Rushwa ni tatizo ndani ya CCM, ukipinga rushwa unaonekana tatizo ndani ya CCM. Hili linathibitika,” amesema. Hata hivyo ameshauri wale walio na mtazamo kwamba, nje ya CCM hakuna maisha ya siasa wabadilike  maana mawazo hayo yamepitwa na wakati.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD AMECHUKUWA FOMU KUGOMBE URAISI WA NCHI YA ZANZIBARMgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Shariff Hamad akiwa na mgombea wa Urais wa nchi ya Tanganyika Mh Edward Lowassa leo katika ukumbi wa Salama  Bwawani..Mh Lowassa alimsindikiza Maalim Seif Shariff Hamad kwenda kuchukua fomu.

 Viongozi,wananchi na wageni maalum walimsindikiz Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Shariff Hamad kwenye hafla ya uchukuwaji fomu.Kutoka kushoto ni Bi Fatma Fereji, Mhe Abubakar Khamis Bakary, Mzee hassan Nassor moyo, Mgombea mweza wa Urais wa nchi ya Tanganyika, Mhe juma Duni na mgombea urais wa nchi ya Tanganyika kupitia UKAWA mhe Edward Lowassa.
DSC01631
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchi Zanzibar MH. Jecha Firauni Jecha kwa makini akionesha fomu ya uteuzi kwa wananchi kabla ya kumkabidhi mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF MH Maalim. Seif Shariff Hamad. Leo tarehe 23/08/2015 Salama Hall Bwawani Zanzibar.
DSC01635
Makamo wa Kwanza wa Rais ambae pia ni Mgombea wa Urais wa nchi ya Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi CUF, MH Maalim. Seif Shariff Hamad akipokea fomu za Uteuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Zanzibar MH: Jecha Firauni Jecha tarehe 23/08/2015 katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Malindi Mjini nchini Zanzibar

 Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Shariff Hamad akionesha fomu za kugombea Urais mara alipokabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi hapa nchini Zanzibar

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Zanzibar MH: Jecha Firauni Jecha akitoa ufafanuzi kuhusu fomu za kugombea uchaguzi kabla ya kukabidhi kwa Mgombea wa CUF , Maalim Seif Shariff Hamad
Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Shariff Hamad akizungumza na wanahabri baada ya kuchukua fomu za kugomea Urais wa nchi ya Zanzibar.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.