Wednesday, August 12, 2015

CCM ATII NI CHAMA GANI HASWA.....?? CCM NI CHAMA CHA NCHI GANI KATIKA NCHI ZA AFRIKA...?? HAHAHAHA

 


IMG-20150810-WA0025
IMG-20150810-WA0023
Screenshot_2015-08-10-20-40-57-1
lowassa
11856528_766736266770683_4263750936932267814_o

Alisema ana mambo mawili ya kusema; kwanza kuwashukuru wafuasi na wapenzi wa Ukawa kwamba kwa kujitokeza kwa wingi wamepeleka meseji moja kwa wasiowatakia mema, wanaosema CUF na Chadema ni watu wenye fujo, wamethibitisha kwamba si kweli. “Tumewahakikishia kuwa sisi ni watu wenye nidhamu na uwezo, Mwenyezi Mungu akipenda Oktoba tunachukua nchi asubuhi peupeee, kwa hiyo watu wasitafute visingizio, watafute vingine, watoto wa mjini wanasema wameisoma namba,” alisema Lowassa huku akishangiliwa na umati wa watu. Akizungumzia jambo la pili, mbunge huyo wa Monduli aliyejiondoa CCM, alisema anauchukia umaskini kiasi kwamba anauona kama ukoma.
Lowassa ambaye mara nyingi husema hajakutana barabarani na Rais Jakaya Kikwete, alisema rafiki yake huyo ndiye aliyeharibu uchumi wa nchi, lakini akasema asingetaka kutoa mashtaki bali kutoa takwimu za hali ilivyobadilika. “Wakati Rais Benjamini Mkapa anaondoka madarakani, bei ya sukari ilikuwa Sh650, leo ni Sh2,300, kutoka 650 hadi 2,300 ameharibu uchumi, hajaharibu...???” aliuliza na kujibiwa, “ameharibuuu.” “Bei ya mchele ilikuwa Sh550 leo Sh2,200, ameharibu uchumi, hakuharibu....??? Sembe kilo ilikuwa Sh250 leo ni Sh1,200, ameharibu hakuharibu..??” alihoji Lowassa na watu wakamjibu ‘ameharibuuu” na kisha akaongeza kuwa kwa sababu hizo, CCM haistahili kuendelea kutawala.
Lowassa alitumia fursa hiyo kuwaalika wanachama wa CCM wasioridhika na hali ilivyo kujiunga na Ukawa kwa kuwa inawezekana kutafuta mabadiliko nje ya chama hicho na kwamba wasione haya bali waangalie idadi kubwa ya vijana waliojitokeza jana. Mgombea huyo, alisema Tanganyika ((Tanzania)) imeshuhudia uporaji mkubwa wa mali za Taifa, ambapo tembo wameuawa kuliko wakati mwingine wowote, hivyo kutokana na vitendo hivyo, CCM haistahili kuendelea kutawala. Kuhusu kutunza shahada za kupigia kura, Lowassa alisema Wanaukawa hawapaswi kufanya mchezo kwa kuwa CCM imekuwapo madarakani muda mrefu watatumia kila kitu ndani ya uwezo wao kubaki madarakani.“Na sisi tutumie kila kitu kilicho ndani ya uwezo wetu kuingia madarakani. Kitakachotuingiza madarakani ni kura, hifadhi shahada yako, shawishi na wengine, tarehe 25 Oktoba tunawatoa madarakani,” alisema.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment