Thursday, August 6, 2015

JE NI KWELI AU UZUSHI TU WA MAGAZETI NA MITANDAO.....?? IKIWA NI KWELI KWA NINI AKAMUWA KUFANYA HIVI....? KISA LOWASSA AU KUKOSA URAISI....??


MWENYEKITI wa Taifa wa  Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho leo majira ya saa 5 asubuhi katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika.
Akizungumza mbele ya waandishi habari,Pro.Lipumba amesema ametafakari sana katika kuendelea kuwa Mwenyekiti wa chama hicho lakini dhamira yake inamsuta.

Amesema kuwa mwaka 2014 hakutaka kugombea nafasi hiyo kutokana na mchakato wa katiba mpya akaamua kugombea kwa lengo ya kuwapa Watanganyika ((watan))  katiba itakayoindoa Chama cha Mapinduzi (CCM). 
Lipumba amesema katika mchakato wa bunge maalumu wakaunda umoja wa katiba (UKAWA) wenye lengo wa kusimamia katiba iliyopendekezwa lakini sasa waliopitisha ndio wanataka kuisimamia katiba hiyo ambayo haingii akilini.

Amesema alikuwa akishiriki vikao vya UKAWA lakini Aprili 1 mwaka huu alisema atang'atuka katika nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Wanannchi (CUF). 

Amesema amepita katika misukosuko mingi katika kukijenga chama hadi kufikia kiasi hata kabambikiziwa  kesi ya kufanya maandamano bila kibali. Lipumba amesema kazi yake atakuwa mwanachama wa kawaida, kufanya utafiti wa maendeleo endelevu  pamoja na kufanya ushauri wa masuala mbalimbali katika chama hicho.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment