Friday, August 14, 2015

NCHINI TANGANYIKA WANAJESHI WA JESHI LA JWT WAKANUSHA KUNYANGANYWA KADI ZAO ZA KUPIGIA KURA


Mkutano na wanahabari ukiendelea.

JESHI la Wananchi wa nchi ya Tanganyika (JWT), limekanusha kuwanyang'anya kadi za kupigia kura maofisa na askari wake kama ilivyodaiwa na mmoja wa viongozi wa chama kimoja cha siasa na kutolewa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika leo asubuhi Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Wananchi Tanganyika (JWT), Kanali Ngemela Lubinga alisema madai hayo siyo ya kweli na  kuwa jeshi hilo halijafanya hivyo na wala haliwezi kufanya hivyo.

"Wanajeshi hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama chochote cha kisiasa na kuwa mwanajeshi haruhusiwi kuwa shabiki wa chama chochote cha kisiasa."

((WACHA KUSEMA UWONGO WEWE WATU WOTE WANAJUWA KAMA CCM HAINA LAKE JAMBO ISIPOKUWA INALINDWA NA POLISI NA NYINYI MAJESHI UNAJIDAI ATII MAJESHI HAWARUHUSIWI KUWA MASHABI WA CHAMA CHOCHOTE.....SASA ILE KUUWA WAZANZIBARI KUANZIA UCHAGUZI WA KWANZA WA VYAMA VINGI ULE ULIKUWA SIO USHABIKI MULIKUWA MUNAUWA TU KWA RAHA ZENU SIO...? WALA SIO MASHABIKI WA CCM.)) KUFICHA WAPIGA KURA FEKI KATIKA KAMBI ZENU SIO USHABIKI...? VIKOSI VYENU KULETA WAPIGA KURA HARAMU FEKI KATIKA VITUO VYA WAPIGA KURA NA KUWALINDA SIO USHABIKI....? N.K. 

Lubinga alisema Jeshi la Wananchi wa Tanganyika linafanya kazi zake kama 'professional state organ duniani na kuwa mwanajeshi anayekiuka huchukuliwa hatua za kinidhamu za kijeshi wala si za kiraia.

Alisema Jeshi la Wananchi wa Tanganyika limesikitishwa na kauli hiyo iliyotolewa na kiongozi huyo.

"Wananchi na viongozi wa kisiasa mnaombwa mfanye kazi zenu za kisiasa na zisianzishwe hoja nje ya maeneo hayo ya kisiasa kwani lugha hizo za upotoshaji zinaweza kuleta hofu, ukakasi na wasiwasi kwa wananchi" alisema Kanali Lubinga.

Kanali Lubinga alisema jeshi hilo linaendelea na shughuli zake kama kawaida halipendi litolewe kauli za upotoshaji, kusikoeleweka ufuatwe utaratibu wa kuuliza kupata majibu ya uhakika kwani wananchi wanaimani na jeshi lao.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment