Friday, August 14, 2015

NCHINI ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD ASEMA UPEPO WA KISIASA NCHINI ZANZIBAR UNAKIVUMIA VYEMA CHAMA CHA CUF


Katibu Mkuu wa Chama cha Wanancfhi CUF, Mhe. Maalim Seif SharifF Hamad amesema upepo wa kisiasa nchini Zanzibar unakivumia vyema chama hicho na matarajio ni kupata ushindi wa kishindo ambao haujawahi kutokea wa asilimia 80 katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Maalim Seif Shariff Hamad amesema hayo jana alipokuwa akiwahutubia viongozi wa Wilaya na majimbo wa chama hicho huko Kiembesamaki, ambapo pia alitangaza timu itakayo kiongoza chama hicho kupata ushindi katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Maalim Seif Shariff Hamad amesema kwa namna wananchi wanavyokikubali chama hicho na namna kilivyojipanga na iwapo kila kiongozi na mwanachama atatekeleza majukumu yake bila ya kulalamika kitachukua idadi kubwa ya majimbo ya uchaguzi na kushinda nafasi ya Urais kwa kishindo.

“Mazingira yaliyopo nchi Zanzibar ni mazuri sana kwa CUF kupata ushindi ambao haujawahi kutokea, hivyo kila mmoja wetu aongozwe na dhamira ya kuchukua nchi mwaka huu, na mara hii haibiwi mtu kura yoyote”, alisema Maalim Seif Shariff Hamad.  

Alisema malengo ya CUF katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni kuwa na idadi ya kutosha ya majimbo yatakayo kiwezesha kufanikisha kikamilifu mipango yake ya kuwaletea matumaini na maisha bora Wazanzibari chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Katika mkutano huo ambao umehudhuriwa na wagombea waliopitishwa na chama kwa upande wa Unguja, Maalim Seif Shariff Hamad amemtangaza Naibu Katibu Mkuu wa CUF nchini Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui kuwa ndiye Meneja wa Kampeni za Urais wa hapa nchini Zanzibar, akisaidiwa na mshauri wake wa Mikakati, Mansour Yussuf Himid.

Aidha kwa upande wa Pemba, Maalim Seif Shariff Hamad alisema Mratibu wa kampeni hizo ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi, Hamad Masoud Hamad akisaidiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk.

Maalim Seif Shariff Hamad alisema Zanzibar hakuna hata jimbo moja ambalo chama hicho kinaweza kusema kwamba hakina matumaini ya kushinda na kwamba suala la kushinda au kutoshinda litategemea chama hicho kimejipanga vipi kuchukua ushindi.

Katibu Mkuu huyo wa CUF ameonya kuwa huu si wakati wa viongozi na wanachama kuvutana na wala si wakati wa kukumbatia ubinafsi kwa baadhi yao kupeana majukumu wasiyo yamudu kwa kuzingatia urafiki au ujamaa.

Kaimu Naibu Katibu Mkuu, Ismail Jussa Ladhu alisema CUF katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu CUF kitakuwa na kampeni ya aina yake kwa makusudi ya kuwathibitishia Wazanzibari na nchi nzima kuwa kweli kimejiandaa kuiongoza nchi ya Zanzibar.

Jussa alisema Agosti 22 wagombea wote waliopitishwa na chama kugombea Uwakilishi watakwenda kuchukua fomu Tume ya Uchaguzi hapa nchini Zanzibar kwa sherehe kubwa ili kila mtu apate habari kuwa safari ya chama hicho kuiongoza nchi ya Zanzibar na kutimiza matarajio yao imeanza rasmi.

“Siku hiyo wagombea wote wa Uwakilishi nchini Zanzibar watakwenda kuchukua fomu, mwenye kupiga dufu, mwenye kupiga mbwa kachoka, mwenye kupiga rusha roho ni ruhusa kufanya sherehe hizo”, alisema Jussa.

Kaimu Naibu Katibu Mkuu huyo alisema kwa upande wa nafasi ya Urais hapa nchini petu Zanzibar, ambayo mgombea wake ni Maalim Seif Shariff Hamad atakwenda kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo Agosti 23, ambapo pia chama hicho kimeandaa shamra shamra za aina yake.  

Katika mkutano huo, Maalim Seif Shariff Hamad aliwakabidhi viongozi wa Wilaya na majimbo seti 40 za jezi kwa kila jimbo moja pamoja na mipira 120. 

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment