Thursday, August 6, 2015

WASIKILIZE WALEVI WANAVYO MTETEA BALOZI MDOGO WA NCHI YA TANGANYIKA BALOZI SEIF


Chama cha Mapinduzi Taifa kimeombwa kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini uzushi ulioandikwa na baadhi ya Mitandao ya Kijamii wa kueneza uongo dhidi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyekuwa miongoni mwa Wana CCM waliowania nafasi ya kuomba Uwakilishi katika mchakato wa kura za maoni uliofanyika hivi karibuni. Ombi hilo limetolewa na Viongozi wa Matawi 12 yaliyomo ndani ya Jimbo Jipya la Mahonda pamoja na wale wa Jimbo la zamani la Kitope wakati wakitoa tamko la kulaani uzushi huo uliomdhalilisha kiongozi wao walipokuwa wakizungumza na vyombo mbali mbali vya Habari hapo Ofisi ya CCM Jimbo iliyopo Kinduni Wilaya ya Kaskazini “B”. Viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Jimbo la Kitope Mzee Suleiman Thabiti walisema uchunguzi unapaswa kufanywa mara moja na yule atakayebainika kubuni na hatimaye kusambaza shuktuma hizo sheria ichukuwe mkondo wake kwa muhusika huyo kufikisha Mahakamani kujibu fitina walizozieneza.
Walisema kumpaka matope yasiyostahika Balozi Seif Ali Iddi ni kukivunjia Heshima Chama cha Mapinduzi jambo ambalo wao kama wanachama hawatakuwa tayari kuona muhusika wa uzushi huo anaachiliwa bila ya kuchukuliwa hatua yoyote.
Mzee Suleiman Thabit alisema Balozi Seif ni Mtu muadilifu anayeheshimu watu wa rika zote ambae sifa pamoja na umakini wake uko wazi. Hivyo kujitokeza kwake kuomba ridhaa ya kutaka kuendelea kuwaongoza Wananchi ndani ya Jimbo hilo kutaleta faraja kubwa kwao. Alisema Wananchi anaowaongoza Balozi Seif ndio wanaomuelewa kama anastahiki kuwaongoza, sasa kutokea watu wakajifanya wasemaji wa wananchi hao ni kitendo cha unafiki na kinastahiki kulaaniwa na wapenda amani wote ndani na nje ya Nchi. Nao baadhi ya Viongozi hao akiwemo Bwana Alhaj Bakari Juma wa Mahonda, Mwinyi Mahfoudh wa Kichungwani,Yussuf Muhsin wa Kwagube,Idarous Makame Kitope A,Bibi Maryam Ahmad Kinduni,Mbwana Said Fujoni,Marijan Maulid Kichungwani walisema Kashfa alizosingiziwa Balozi Seif wameahidi kuzithibitisha wakati wa uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba kwa kumpa ushindi wa kishindo ili aendelee kuwa kiboko wa wapinzani Nchini.
Walisema Wananchi wa Jimbo pamoja na Wilaya Nzima ya Kaskazini “B” bado wanamuhitaji Kiongozi huyo kutokana na juhudi anazoendelea kuzichukuwa katika kusimamia maendeleo ya Wananchi. Walifahamisha kwamba yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta mbali mbali za maendeleo ambayo yalisimamiwa kwa nguvu zote ni Kiongozi huyo na kushuhudiwa na kila mwana Jamii mwenye macho. Walisema Vijiji kadhaa vilivyomo ndani ya Jimbo aliloliongoza katika kipindi cha miaka kumi iliyopita vimeimarika kielimu na ustawi wa Jamii kiasi kwamba hakuna mtoto anayetembea masafa marefu kutafuta elimu ndani ya Jimbo aliloliongoza.“ Fujoni imeendelea kielimu na kuijingea sifa Wilaya Nzima ya Kaskazini “B” kwa kuanzisha madarasa ya Kidatu cha tano na kuendelea cha sita. Hii ni miongoni mwa juhudi aliyochukuwa Balozi Seif akiwa kama Mbunge wa Kitope ambayo sisi wananchi tunafaidika nayo “. Alisema Bwana Ali Haji Abdullah wa Fujoni.
Wakizungumzia sekta ya michezo Viongozi hao walieleza kwamba Jimbo la Kitope limepiga hatua kubwa katika uimarishaji wa michezo na kulifanya litajike baada ya ushiriki wa wanamichezo wake katika mashindano mbali mbali ya ndani. “ Tumeshiriki kwenye mashindano ya ujirani mwema yaliyotusaidia kujijengea umaarufu Visiwani ambayo yalitung’arisha kutokana na msaada mkubwa wa vifaa vya michezo alivyotupa Mbunge wetu “. Sasa kama Baniani mbaya hilo mtajua nyinyi. Sisi tutaendelea kumuheshimu na kumpenda kwa imani yake kwetu “. Alisema kwa hamasa Idarous Makame wa Kitope A. Mkutano huo wa Viongozi wa Matawi 12 yaliyomo ndani ya Jimbo Jipya la Mahonda pamoja na wale wa Jimbo la zamani la Kitope umekuja kufuatia mitandao ya Kijamii kuandika na kusambaza uongo kwamba uchaguzi wa kura za Maoni Jimbo la Mahonda umeahirishwa kufuatia tuhuma kwamba Balozi Seif amewatia ndani vijana pamoja na kukutwa visanduku vya kura vilivyoingizwa vikaratasi vyenye jina lake kwenye mchakato huo uliofanyika Jumamosi ya Tarehe 1 Agosti 2015. Uchaguzi ulioahirishwa ni ule wa nafasi ya Ubunge pekaa tena katika Tawi moja tu la Mahonda. Lakini Uchaguzi wa Nafasi ya Uwakilishi uliokuwa na wagombea wawili kwenye Jimbo hilo ulikwenda kama kawaida katika Matawi yote ya Jimbo hilo ambapo Balozi Seif Ali Iddi alifanikiwa kuongoza kwa Kura 2,089 wakati mgomgea mwenzake Faraji Ramadhan Faraji alipata kura 603.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment