Saturday, September 5, 2015

MNARA WA DAMU ZA WAZANZIBARI WAKAMILIKA


Sioni tatizo na wala siogopi kusema kuwa Dr. Ali Mohammed Shein na viongozi wenzake juzi wamezindua mnara wa mauaji ya kimbari ya Wazanzibari wasiokuwa na hatia na tunakaririshwa kuwa tuyaite ‘mapinduzi matukufu’, wakati kilichofanyika ni ubakaji wa wanawake, uwaaji, utesaji na udhalilishaji. Maisha ya takribani watu 2,000 yaliondoka, 26,000 wakafungwa magerezani, 100,000 wakaihama Zanzibar, takwimu hizi ni kwa mujibu wa Mail & Guardian Africa, katika makala yao yenye anuani; “Africa’s ‘forgotten genocide’ marks its 50 anniversary: Revisiting the Zanzibar revolution”. Nikisema ni mauaji ya kimbari si kwa mujibu wa matakwa yangu, awali nimetanguliza makala ya Cris Oke, yakizungumzia mapinduzi ya Zanzibar kuwa ni mauaji ya kimbari yaliyosahauliwa, pia wanahistoria wengi wameyaita mapinduzi hayo kuwa ni mauaji ya kimbari. Si lengo la makala haya kuamsha hisia na hasira za watu, lengo lake ni kutazama kilichofanywa ili iwe ni funzo, pengine watu wamesamehe lakini naamini ni ngumu kusahau, kizazi cha sasa lazima tuelezwe kipi hasa kilitokea ili nasi tuje tuwaeleze watoto wetu nini kilitokea, tusifiche historia kwani tukiificha itapotea.
Mapinduzi ni matokeo ya mambo makubwa matatu, kama unalo la nne na la tano unaweza kuongeza, mimi ninayo matatu tu. Moja, ni kuondosha utawala wa kidhalimu/ kidikteta/kimabavu.Pili, mapinduzi ni matokeo ya uchu wa madaraka. Tatu, ni matokeo ya chuki za watu dhidi ya kiongozi na huenda hawana mpango wowote na uongozi wake . Historia haiyoneshi kuwa Zanzibar kulikuwa na dikteta aliyeiyongoza nchi hii, kwahiyo tafsiri ya mapinduzi ya Zanzibar ni matokeo ya mambo mawili yaliyobaki nayo ni uchu wa madaraka na chuki ambazo wapinduaji walikuwa nazo. Wakati historia ikitueleza kuwa Field Marshal’ John Okello ndiye aliyeyaongoza mapinduzi ya kuupindua utawala wa Kisultani, basi si ajabu kuwa Okello alibebwa zaidi na chuki za kuchukia mambo mawili. Moja Waarabu, Pili Uislamu. Kwani Samantha Spooner mwandishi wa makala ya; Africa’s ‘forgotten genocide’ marks its 50 anniversary: Revisiting the Zanzibar revolution; ameandika kuwa; “A Ugandan by birth (Marshal John Okello) who believed that he was divinely chosen by God to remove Arabs from power” na pia katika mkutano wa hadhara Okello alisema;“Therefore my brethren, we must get them out of the Island by guns and knives”. Katika sababu mbili zilizobaki ambazo zilipelekea mapinduzi ya Zanzibar, basi Okello yeye alifanya mapinduzi kwa sababu ya chuki ya kidini zaidi na Uarabu, huku akijinasibu kuwa yeye ni mtu wa Mungu na ameelezwa na Mungu kuwaondoa Waarabu.
Sasa wale wa ndani ambao nao walishiriki katika mapinduzi ajenda yao wao ilikuwa ni tofauti na Okello, wao walibebwa zaidi na uchu wa madaraka na ndio dhamira yao hii ikapelekea hata wale wasiokuwa Waarabu (Waafrika) lakini ni watiifu kwa utawala wa kisultani kuuwawa pia, wapinduaji wa ndani Uislam halikuwa tatizo kwao, lakini uchu wa madraka ndio ilikuwa sababu kubwa ya kuunga mkono na kushiriki mapinduzi. Tuseme sababu yoyote iwayo ya mapinduzi yale ndio yameshafanyika, lakini kuna suali la kujiuliza na nitaliuliza pia mwisho wa makala haya; Kulikuwa na haja gani ya kuuwa watu elfu mbili kwa sababu tu ya kutaka utawala uondoke? Napata jawabu kuwa mauaji yaliyofanyika si mauaji yaliyotoa picha kwamba utawala wa kisultani ulikwa na nguvu nyingi hivyo ili kuuwondoa ilibidi watu elfu mbili wauwawe. Si kweli. Samantha Spooner anasema; “Many call it “the revolution”, but for the victims this year marks the 50th anniversary of the mass murder of Zanzibar’s Arabs and Indians by the black majority”. Ukweli unauma lakini mapinduzi yetu yalikuwa tu ni matokeo ya chuki dhidi ya jamiii fulani na imani na uchu wa madaraka, hilo ndio liko hivyo na litabaki hivyo. Wazanzibari Waarabu ndio walioteketea kwa kiasi kikubwa. Hatupaswi kusema? Kwanini wao wakiyakumbuka mapinduzi kwa kuyaenzi kwa gharama na vifijo huku wakificha ukweli wa kile kilichofanyika, sisi tusiseme ukweli wa walichokifanya wapinduaji hakikuwa kizuri?
Kulikuwa na haja gani ya kuuwa Wazanzibari kwa sababu ya rangi zao? Kwani kuipindua serekali ya Kisultani kusingetosha na kuwaacha Wazanzibari na shughuli zao? Kulikuwa na haja gani ya kuwatafuta watu majumbani mwao kuwafanyia unyama wa kuuwa na kuwabaka? Na siku zote mapinduzi hayakupi uhakika wa kinachofuata baadae, lakini ukweli wa mambo ni kuwa hali za Wazanzibari zimekuwa ngumu zaidi kuliko hata baada ya mapinduzi, huo ndio moja ya ukweli unaofichwa. Sioni tatizo kusema kuwa Dr. Ali Mohammed Shein na viongozi wenzake juzi wamezindua mnara wa mauaji ya kimbari ya Wazanzibari wasiokuwa na hatia na la kuumiza zaidi ni kuwa mapinduzni ya Zanzibar ni mauaji ya kimbari yaliyosahauliwa. Kwangu mimi nafsi za watu zinathamani kubwa mno na wala sijali kuwa wengi wao walikuwa Waarabu au laa! Hata wangekuwa wengine wowote wale lakini ukweli utabaki kuwa hakukuwa na haja ya kuuwa watu elfu mbili kwa sababu ya kumuondoa kiongozi mmoja madarakani. Kati ya Waarabu 14,000 hadi 20,000 waliouwawa, ni pamoja na Wahindi na Waafrika ambao walikuwa watiifu kwa utawa wao,na wala si kweli kwamba kulikuwa na unyanyasaji kwa jamii nyengine kutoka kwa Waarabu, historia inatueleza kuwa walikuwepo pia Waarabu masikini na kulikuwa na ushirikiano mkubwa wa Waarabu na wasiokuwa Waarabu kwani dini ndio ilikuwa kiungo kikubwa.
Si lazima tuifungue historia yote na kuyasema yaliyotendeka kinaga ubaga, kwani mengi ya hayo ni machungu na yanaumiza kupita kiasi, mengine hayasemeki ambayo watu walifanyiwa, eti sababu ni mapinduizi. Matokeo ya mapinduzi yale ni kuingia katika ukoloni wa Tanganyika, ni makosa ya kihistoria ambayo siogopi kusema yanaendelea kutughariumu hadi leo, mapinduzi ya kuuwa watu elfu mbili na kisha muungano ni makosa ya kihistoria yanayoendelea kutafuna kizazi cha Wazanzibari. Kwani kufanya mapinduzi kulikuwa na lazima ya kubaka,kuuwa, watese, wanyanyase na kudhalilisha, kisha wawachukue watoto weupe na kuwaoa kwa nguvu, yote haya yalikuwa matokeo ni mapinduzi ambayo sasa tunakaririshwa kuwa tuyaite ‘matukufu’ na tunayajengea minara mirefu ya gharama, kama vile tumesahau hasa wapinduaji walifanya nini. Historia inasema kuwa mapinduzi ya kumuondoa Sultani madarakani yalichukua masaa machache tu lakni mauaji yaliendelea kwa siku nne, hivyo baada ya wenye uchu wa madaraka kupata madaraka wale akina Okello waliofanya mapinduzi kwa chuki wakaendelea kuiandama jamii ya rangi fulani. Africa Addio ni makala iliyotengenezwa na Wataliano Gualtiero Jacopetti na Franco Prosperi, ikionesha mistari ya wafungwa wakipelekwa katika kaburi la pamoja kisha wanapigwa risasi na kuuwawa, vijiji vinaharibiwa, na malori ya maiti yakienda kuzika katika makaburi ya pamoja. Usishangae haya yote yametokea Zanzibar. Kulikwa na haja gani ya kufanya haya yote wakati utawala wa Kisultani ulikuwa umeshapinduliwa na yeye mwenyewe ameshakimbilia Uingereza?
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

1 comment:

 1. abedi amani karume, the UNEDUCATED IDIOT, RAPIST and the leader of the ASP, had absolutely NO right nor any legitimacy to proclaim himself as the president of Zanzibar after the revolution since he was NOT even born in Zanzibar! See the memoirs of the reknowned Zanzibar politician, Seif Sharif Hamad pages 205 to 220 cited below.

  abedi amani karume is said to have been born in Nyasaland (Malawi)[1].Other sources [2] say he was born in Ruanda-Urundi or even eastern Congo, see page 220, memoirs of Seif Sharif Hamad, reference [1].

  abedi amani karume was thus an ILLEGITIMATE leader of Zanzibar!

  Some twenty thousand innocent and defenseless men, women and children were killed during and after the revolution in Zanzibar in 1964.

  May the curse of ALLAH be upon abedi amani karume and his associates for the murder of these innocent people simply in order to grab power and perpetrate more injustice, rape and torture on the people of Zanzibar.

  References
  [1]Race Revolution and the Struggle for Human Rights in Zanzibar The Memoirs of Ali Sultan Issa and Seif Sharif Hamad by G. Thomas Burgess

  [2] Sheikh Abeid Amani Karume Biography from Answers_com.mht

  ReplyDelete