Wednesday, September 2, 2015

MNARA WA MIAKA 50 WAZINDULIWA NCHINI ZANZIBAR


 Muonekano wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ukionekana wakati wa mandhari ya usiku katika bustani ya michezani kisonge ukiwa katika maandalizi ya uzinduzi wake uliofanyiuka asubuhi hii na kuzinduliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Shein.


Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Shein amewatahadharisha watu wanaoogopa mabadiliko ya Maendeleo kwamba waachane na tabia hiyo vyenginevyo Dunia  bila ya shaka na ajizi itawabadilisha. Alisema Wazanzibari wanapaswa kwenda na wakati katika  kuendesha  pamoja na kusimamia masuala yao ili waende sambamba na wananchi wa visiwa vyengine Duniani wanaoonekana kupiga hatua za haraka za Maendelei ya Kiuchuni na Ustawi wa Jamii. Shein alieleza hayo wakati akizungumza na Watu wa rika mbali mbali ambao wengi wao ni vijana na Watoto mara baada ya kuuzindua Mnara wa Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 uliojengwa katika Majumbe ya Maendeleo Michenzaji Kati Kati ya Mji nchini Zanzibar.

Alisema wapo watu wakiwemo baadhi ya watendaji wa Taasisi za Umma wenye madaraka ya kutoa maamuzi ambao wana tabia ya kuogopa Mabadiliko kwa kuchelewesha kuidhinisha miradi ya Kiuchumi inayokusudiwa kuwanzishwa na wawekezaji walioamua kuwekeza hapa nchini Zanzibar.Shein alikemea kwamba tabia hiyo mbaya isiyo na sababu za kimsingi imekuwa ikichelewesha na kuviza Maendeleo ya Wananchi na kupunguza Mapato ya Taifa kupitia uanzishwaji wa miradi hiyo wakati Serikali tayari imeshaweka milango wazi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi. Aliupongeza Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar chini ya usimamizi wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko huo kwa juhudi iliyochukuwa ya kujenga mnara huo wenye urefu wa Mita 33.5 ambao utatoa fursda kwa wananchi na wageni kuona mamdhari nzuri ya Mji wa Zanzibar sambamba na kupata huduma za msingi.

Alisema chimbuko la Mnara huo lililoibuliwa na Baraza la Mapinduzi Zanzibar  wakati wa maadhimisho ya sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar  lilikuwa na lengo la kuonyesha vugu vugu la Maendelei ya Zanzibar tokea kufanyika kwa Mapinduzi ya Zanzibar ya Tarehe 12 Januari Mwaka 1964. Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar {ZSSF } Nd. Abdulwakil Haji Hafidh alisema ujenzi wa Mnara huo mbali ya kutoa fursa kwa wananachi na wageni kuangalia mamdhari ya Mji wa Zanzibar lakini pia utatoa nafasi kwa wazazi kupata mapumziko  huku wakiwasubiri watoto wao wanaowapeleka katika Viwanja vya Kufurahishia Watoto Kariakoo. Alisema tahadhari hiyo imechukuliwa maalum kwa kuzingatia kwamba Mji wa Zanzibar bado haujawa na maeneo mengi ya kupumzikia kiasi cha kuongezwa maeneo hayo ili kukidhi mahitaji kwa siku zinazotokea kuwa na idadi kubwa ya watu  hasa siku za siku kuu ambazo watu wengi huamua kutembelea viwanja hivyo.

Mkurugenzi huyo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } alifahamisha kwamba mnara huo utakuwa na sehemu maalum zitakazowekwa kwa ajili ya watu na wageni kujifunza Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar, sehemu za kujifunza wachezaji wa michezo mbali mbali maarufu duniani, kuangalia mandhari ya Mji wa Zanzibar pamoja na Mkahawa unaozunguuka. Alisema taasisi za Fedha kama Benki ya Wananachi wa Zanzibar PBZ, na Ile na NMB zitatoa huduma za fedha kwa kutumia mtandao wa ATM ili kuwaondoshea usumbufu wateja wao wakati wanapoishiwa na Matumizi. Nd. Abdulwakili alieleza kwamba  katika kulibadilisha eneo hilo la Michenzaji Mfuko huo umeshaandaa mpango wa kujenga majengo la Kimataifa ya Kibiashara  { SHOOPING  MALLS } upande wa Kaskazini kwa kutafuta washirika wa Maendeleo watakaoshirikiana katika kujenga majengo hayo. Mnara huo wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar  wenye ghorofa 9 uliojengwa kwa gharama ya Shilingi za Kitanzania Bilioni Nane unatarajiwa kurejesha thamani ya Fedha hizo katika kipindi cha miaka 12 ijayo.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

1 comment:

 1. abedi amani karume, the UNEDUCATED IDIOT, PAEDOPHILE and RAPIST, and the leader of the ASP, had absolutely NO right nor any legitimacy to proclaim himself as the president of Zanzibar after the revolution, since he was NOT even born in Zanzibar! See the memoirs of the reknowned Zanzibar politician, Seif Sharif Hamad pages 205 to 220 cited below.

  abedi amani karume is said to have been born in Nyasaland (Malawi)[1]. Other sources [2] say he was born in Ruanda-Urundi or even eastern Congo, see page 220 in the memoirs of Seif Sharif Hamad, reference [1].

  abedi amani karume was thus an ILLEGITIMATE leader of Zanzibar!

  Some twenty thousand innocent and defenceless men, women and children were killed during and after the revolution in Zanzibar in 1964.

  May the curse of ALLAH be upon abedi amani karume and his associates for the murder of these innocent and defenceless people simply in order to grab power and perpetrate more injustice, rape and torture on the people of Zanzibar.

  References
  [1]Race Revolution and the Struggle for Human Rights in Zanzibar The Memoirs of Ali Sultan Issa and Seif Sharif Hamad by G. Thomas Burgess

  [2] Sheikh Abeid Amani Karume Biography from Answers_com.mht

  ReplyDelete