Tuesday, September 15, 2015

NCHINI TANGANYIKA FREDERICK SUMAYE ASEMA HANA UCHU WA MADARAKA ILA UCHU WAKE WA KUJIUNGA UKAWA NI KUTAKA KUINGOA CCM
Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za ubunge wa Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, alisema kwa sasa hakuna njia au mtu atakayeweza kuifufua CCM.

Sumaye alisema wamezunguka maeneo mengi ya nchi kila walipokuwa wakienda wamebaini Watanganyika ((Watanzania)) Wazanzibari hivi sasa wanahitaji mabadiliko na hawana mpango wa kuongozwa tena na CCM.

Aidha Sumaye alipingana na wale wanaosema amejiunga Ukawa kwa uchu wa madaraka, na kusema kuwa uchu wake wa kujiunga Ukawa ni kutaka kuing’oa CCM.

“Sikuja UKAWA kutafuta cheo kwa sababu nimeshakuwa waziri mkuu na hata hapa Ukawa hakuna nafasi ninayotaka kwa sababu nafasi ya urais yupo Lowassa na nafasi ya waziri mkuu siwezi kupata kwa sababu sijagombea ubunge ila ninachofanya ni kuhakikisha CCM inaondoka madarakani,”

Sumaye alisema kwa kuingia kwake UKAWA, amejikuta akipata vitisho kutoka serikalini:.

“Suala la kunitisha kuninyang’anya mashamba yangu ni kunikomaza zaidi kwa kuwa naamini suala hilo ni sawa na kumpiga chura teke.”

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment