Monday, September 14, 2015

NCHINI TANGANYIKA LOWASSA ASIMIKWA KUWA KIONGOZI WA WANYATURU, MKOANI SINGIDA


Mmoja wa wazee wa Kimila wa Kabila la Wanyaturu, Mzee Semani Nyambia akimvisha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, vazi la kimila (mgololi) ikiwa ni ishara ya kusimikwa kuwa mlezi wa Wanyaturu, wakati wa Mkutano wake wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini, leo Septemba 13, 2015


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini, leo Septemba 13, 2015. katika hotuba yake, Mh. Lowassa amesema iwapo atapata ridhaa ya wananchi kuwa Rais wa Tanzania, ataanzisha viwanda vya kusindika zao la alizeti, ili wakulima wa zao hilo waweze kufaidika na pia atakabiliana na kero zote za Mkoa wa Singida kwa ujumla. Mh. Lowassa, kesho Septemba 14, 2015 ataendelea na ziara yake ya Kampeni katika Mkoa Shinyanga, baada ya leo kumaliza katika Mkoa wa Singinda, kwenye Majimbo ya Manyoni Magharibi, Singida Kaskazini, Iramba Mashariki na Iramba Magharibi.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, baadhi ya wagombea wa Udiwani wa maeneo mbalimbali ya Jimbo la Singida Kaskazini, wakati wa Mkutano wake wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini, leo Septemba 13, 2015.









TUNDU LISSU A.K.A. RONALDO AKIWA UKWELI WANANCHI





Hawa wote wameahidi kuwapakura.














KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment