Tuesday, September 1, 2015

NCHINI TANGANYIKA SHERIA YA MAKOSA ATII YA MTANDAO KUANZA KUTUMIKA LEO NCHINI TANGANYIKA


Nchini Tanganyika Serikali atii imewatoa hofu wananchi kuhusu Sheria ya Makosa ya Mtandao inayoanza kutumika rasmi leo kuwa haijatungwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu, bali kwa maslahi mapana ya taifa na kuleta maendeleo ya nchi, kujenga uchumi imara na kupambana na wahalifu.

Aidha,  serikali imewasisitizia wananchi kutumia vizuri mitandao kwa faida yao na taifa na kujiepusha na mambo ambayo yanakatazwa na sheria hiyo  ili kutoingia matatani.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika jana kuhusu kuanza rasmi kutumika kwa sheria hiyo na ya miamala ya kielektroniki.

“Serikali imejiridhisha baada ya kufanya maandalizi yote muhimu ikiwamo kutoa elimu kwa umma na kujenga uelewa kwa watekeleza wa sheria hizi. Sasa sheria hizi zitaanza kutumika rasmi Septemba 1 (leo),” alisema Prof. Mbarawa.

Alisema sheria hiyo itasaidia kupambana na uhalifu kwenye mtandao kutokana na watu wengi kutumia vibaya mtandao na kuwalaghai watu kutuma fedha ama kuiba katika mabenki.

Alisema kwa mujibu wa sheria hiyo, watu wanaosambaza meseji za uchochezi ama za uongo kwa watu wengine ni kosa la kisheria na kufanya hivyo watakumbana na adhabu kali.

Alisema mtumiwaji wa meseji za aina hiyo akifuta pasipo kusambaza kwa watu wengine sheria hiyo haitamwadhibu wala kumhusu.

“Sehemu ya kifungu cha sheria ya makosa ya mtandao, kifungu cha 16 kinaeleza: mtu   atakayechapisha   taarifa au data katika picha, maandishi, alama au katika namna nyingine yoyote katika mfumo wa kompyuta, huku akijua kwamba taarifa au data hizo ni za uongo, zinapotosha, zisizo sahihi, na kwa lengo la kudhalilisha, kutishia, kuudhi au kwa njia nyingine au kudanganya umma au kuchochea utendaji wa kosa, atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atalipa faini isiyopungua Sh. milioni tano au kutumika kifungo kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja,” alisema.
Prof.   Mbarawa alitoa wito kwa wananchi wazingatie matumizi salama na sahihi ya huduma za mawasiliano na mitandao kwa manufaa ya kila mtu na kwa maendeleo ya taifa na kuepuka matumizi yasiyo sahihi.

Baadhi ya makosa ambayo yanaweza kukufanya ushtakiwe
  1. Kuweka mtandaoni picha za kingono za watoto
  2. Kuweka mtandaoni picha za ngono au za utupu
  3. Kuweka taarifa za uongo mtandaoni
  4. Kuweka taarifa za uchochezi mtandaoni
  5. Kutukana au kumdhalilisha mtu
  6. Kuweka mtandaoni tetesi zisizothibitishwa
  7. Kutukana au kumdhalilisha mtu kwa misingi ya udini/ukabila.
  8. KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment