Tuesday, September 15, 2015

NCHINI ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD AHIDI KUPANDISHA BEI YA ZAO LA MWANI AKICHAGULIWA KUWA RAIS WA NCHI YA ZANZIBAR


Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kupitia chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutubia wananchi wa Tumbe alipotembelea eneo hilo.

Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kupitia chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewaahidi wakulima wa zao la mwani hapa nchini Zanzibar kuwa atapandisha bei ya zao hilo mara moja, iwap atachaguliwa kuwa Rais wa nchi ya Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwezi ujao. Maalim Seif alisema bei wanayolipwa wakulima ya shilingi 700 na 800 hivi sasa ni ndogo na hailingani na gharama wanazozitumia wala haiwasaidii wakulima wengi wao wakiwa ni akinamama katika kuondokana na umasikini. Mgombea alisema hayo alipowatembelea wakulima wa mwani, wakulima wa mpunga na kukagua soko la mboga mboga na samaki katika majimbo ya Tumbe na Konde, mkoa wa Kaskazini Pemba.

Awali katika risala ya wakulima wa mwani na wavuvi wa maeneo hayo iliyosomwa na Aisha mour Ali walisema wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa vifaa, bei isiyoridhisha na kukosa boti za kisasa za kufanyia shughuli za uvuvi. “Tangu 1994 tulipoanza kulima mwani hatujafaidika na bei tunayo lipaa, shilingi 700 tunazopewa hazilingani na ugumu wa kazi hii na hilo tumelilalamikia miaka mingi”, walisema katika risala hiyo. Maalim Seif Shariff Hamad alisema utafiti uliofanywa unaonesha iwapo wakulima wa mwani watawezeshwa kutumia mbegu za kisasa na kufanya kazi kitaalamu zaidi, zao hilo linaweza kutoa mchango mkubwa katika juhudi za kuwatoa wakulima katika umasikini. Alia ahidi kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa nchi ya Zanzibar atahakikisha wanaleta wataalamu wa kutosha kutoa mafunzo ya uzalishaji bora wa zao hilo, kutafuta vifaa pamoja na mbinu mbadala kuliongezea thamani zao la mwani.

“Azma yangu ni kuona wakulima wa mwani wananufaika na jasho lao kama vile wanavyo nufaika wakulima wenzao wa zao la karafuu”alisema Maalim Seif Shariff Hamad. Aidha, aliahidi kuwa atahakikisha mwani unaozalishwa hapa nchini Zanzibar una sarifiwa (processing) kabla a kuuzwa na kuondokana na utaratibu wa kuuzwa mzima, utaratibu ambao hukukosesha thamani kubwa katika soko la Kimataifa. Kilimo cha zao la mwanai kimepata umaarufu mkubwa nchini Zanzibar kwa kujumisha wakulima katika vijiji vya mwambao wa bahari, wengi wao wakiwa ni akina mama, kwa mwaka wastani wa tani 13, 000 huzalishwa hapa nchini Zanzibar na kuuzwa nje ya nchi. Kuhusu uvuvi, Malim Seif Shariff Hamad alisema azma yake ya siku nyingi ni kuhakikisha wavuvi kote hapa nchini Zanzibar wanapatiwa vyombo vya kisasa vya uvuvi ambavyo vitawawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi mkubwa.

Alieleza kuwa kinachojitokeza hivi sasa ni kupungua kwa samaki katika eneo la mwambao wa visiwa, hivyo atahakikisha anaandaa mikakati ya kuwawezesha wavuvi wa hapa nchini Zanzibar ambao wanafikia 32, 000 kufanya shughuli hizo katika bahari ya kina kirefu ambapo kuna samaki wa kutosha. Sambamba na mikakati hiyo, Maalim Seif Shariff Hamad alisema atafanya kila njia kuhakikisha zao la mpunga linazalishwa kisasa chini ya utaratibu wa umwagiliaji maji, kwa vile mchele ndio chakula kikuu kwa watu wa Zanzibar. Akizungumza na wakulima wa mpunga katika mabonde la kinyakuzi na Saninga alisema nia yake ni kuhakikisha Zanzibar inapunguza utegemezi wa bidhaa za chakula kutoka nje ya nchi na iweze kuzalisha asilimia 60 ya mahitaji yake ya chakula hasa mchele. “Mipango hiyo itawezekana bila wasi wasi, nitaanzisha benki maaluma ya kusaidia wakulima, wavuvi na wajasiriamali na wataweza kupata mikopo yenye masharti nafuu”, aliahidi Maalim Seif Shariff Hamad. Aliwataka watendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Micheweni kutafuta watu wenye uwezo wa kuliendesha soko jipya la kisasa lililopo katika kijiji cha Tumbe ili liweze kutumika na kuwanufaisha wakaazi wa maeneo hayo.

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment