Saturday, September 19, 2015

NCHINI ZANZIBAR WALINZI WA VIONGOZI WA CCM WAZUIA WANDISHI BINAFSI,WACHUKUWA KAMERA NA BLOG KATIKA MIKUTANO YAO YA KAMPENI

S3090021

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Hamad Mberwa Hamad akiwahutubia na kutuoa Sere za CCM zilivotelekezwa na kuiletea Maendeleo ...nchi ya Zanzibar.

Katika mkutano wa leo wa CCM wa huko Konde, Pemba nilikuwa nimejipanga kuurusha moja kwa moja kama kawaida yangu ya kurusha mikutano ya kampeni inayofanyika kisiwani Pemba na Unguja ili watu wajuwe nini kinaendelea nchi petu.
Tayari nimesharusha live mikutano mitatu ya chama cha Wananchi C.U.F, Mkutano wa Ufunguzi ulofanyika Tibirinzi Chake Chake Pemba, Mkutano ulofanyika Ole na ule ulofanyika Kiungoni ila kwa masikitiko makubwa walinzi wa mikutano wa Chama Cha Mapnduzi wameweka vikwazo vyengi dhidi ya waandishi binafsi, hii leo nilikuwa nina lengo la kurusha Mkutano wao unaofanyika maeneo ya Konde, Kaskazini Pemba, ila kwa masikitiko makubwa nimekumbana na vikwazo kutoka kwa walinzi wa mikutano hiyo, nilikuwa teyari kufanyiwa checkup lakini hawakutaka na kusisitiza kuwa nisiende mbele wanapokaa waandishi wengine na wachukuzi wa video hata baada ya kutoa vielelezo vyote vya kiusalama.
Nilimuuliza mmoja miongoni mwa walinzi wa wa eneo hilo kwa nini waandishi na wachukuzi wa filamu binafsi wanazuiwa..?? alijibu kuwa ni lazima uwe na kitambulisho na vielelezo vitokavyo Serikalini. Huu si uhakika, sababu mmoja miongoni mwa watu ambae anashoot video katika eneo lile alikuwa ni mtu ambae ninamjua sana na wala hakuwa na kitambulisho na kielelezo chochote cha uandishi, alikuwa yuko mbele anachukua video; ni kwa masikitiko makubwa Chama Cha Mapinduzi kinatuzuia watoa habari binafsi na wanablog wala hawajaanzisha mfumo wowote wa kuwatambua waandishi binafsi na wanablog binafsi.
Kwa hivyo tunaomba radhi kwa kutorusha matangazo hayo katika mtando wetu.
Mzalendonet (c) 2015 na blog binafsi.
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment