Thursday, September 3, 2015

SAMIA TATIZO SIO MADEREVA WA BODABODA BALI NI SEREKALI YAKO YA CCM IMESHINDWA KUIPA VAMPAUMBELA VYA WANAFUNZI,UMEME NA MAJI KWA MIAKA 54 UTAWEZA WEWE KAMA WAWEZA MBONA MPAKA LEO MAKUNDUCHI ZANZIBAR HAKUNA MAJI WALA UMEME.....???


Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu.
Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu, atii ameonya vijana waendesha bodaboda kuacha tabia ya kuwarubuni wanafunzi wa kike kwa chipsi na ‘lifti’ jambo linalowasababishia mimba zisizotarajiwa. “Vijana ninyi na vipikipiki vyenu mnawaharibia maisha watoto wa kike kwa kuwapa mimba zisizotarajiwa,” alisema Samia Kutokana na tatizo hilo, Samia alisema akichaguliwa yeye na mgombea wa urais kupitia CCM, Dk. Pombe Magufuli atahakikisha anakabiliana na hali hiyo kwa kujenga mabweni ya wasichana katika shule za kata. Alisema bila mabweni wasichana wa kike wataendelea kupata mimba zisizotarajiwa na hivyo kuharibu maisha yao. Kuhusu tatizo la maji katika jimbo la Kibakwe, Samia aliahidi kutatua kero hiyo kwa kuchimba visima virefu. ((anachekesha kweli atii 2015 bado unawza kuchimba visima))
Akizungumza na wananchi, mgombea wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene, alikiri kuna tatizo sugu la maji na kuahidi kwamba wampe kura ili aweze kumaliza tatizo hilo. Kwa upande wake, mgombea wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde, alisema kuna tarafa nzima katika jimbo lake ambalo halina umeme. Lisinde alitumia lugha ya kigogo kuomba kura kama ilivyotokea katika Jimbo la Iramba Magharibi kwa Mwigulu Nchemba wiki iliyopita alipotumia lugha ya kwao kuomba kura. Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa, aliwataka wapigakura kubali njia kuu na kwamba mchepuko siyo dili. Kimbisa alimkabidhi Samia zawadi ya mbuzi jike katika Jimbo la Mtera ambaye hata hivyo hakuichukua na badala yake aliikabidhi kwa mkuu wa wilaya akimtaka aitunze mapaka azae mapacha. Samia alikiri kuwa Jimbo la Mtera linakabiliwa na hali ya ukame, lakini akawahakikishia wananchi kwamba serikali itapeleka chakula kwa ajili ya kukiuza kwa bei nafuu.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment