Tuesday, September 1, 2015

UFISADI WA ESCROW UMEPEWA BARAKA ZOTE NA IKULU YA NCHI YA TANGANYIKA


Mgombea Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa akizungumza katika uzinduzi wa mkutano wa kampeni za Rais, wabunge na madiwani kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Jumapili, Agosti 30, 2015
Sumaye awa mbogo, amvaa Kikwete
Ajibu mapigo, aorodhesha ufisadi Serikali ya Kikwete
Umo Escrow…EPA…Mabehewa mabovu ya Mwakyembe
Hotuba kiduchu ya Lowassa yazua maswali
Mgombea Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa akizungumza katika uzinduzi wa mkutano wa kampeni za Rais, wabunge na madiwani kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). ‘Kama unaishi nyumba ya vioo basi ni vema usiwarushie wenzako mawe’ usemi huu ulidhihirika jana baada ya baadhi ya viongozi waandamizi wa upinzani wakiongozwa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye kujibu tuhuma za ufisadi huku akiorodhesha ulaji rushwa uliokithiri ndani ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete. Akizungumza mbele ya umati wa kihistoria katika Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika, Sumaye alisema Edward Lowassa, alijiuzulu February 2008, ili kunusuru serikali ya Kikwete, isianguke kutokana na kashfa ya kufua umeme ya Richmond. Hata hivyo, kitendo cha mgombe urais wa Ukawa kutumia chini ya robo saa kuhutubia mkutano huo jana, kiliacha maswali mengi hasa kwa wapinzani wake wa kisiasa ambao wamekuwa wakihoji afya yake katika kuhimili mikiki ya kampeni siku sitini nchi nzima. Huku akishangaliwa kwa nguvu Sumaye aliyekuwa waziri mkuu kwa miaka kumi katika serikali ya awamu ya tatu, alisema tangu Lowassa ajiuzulu, kumekuwepo na kashfa kubwa za ulaji rushwa ndani ya serikali ya rais Kikwete zikiwemo ununuzi wa mabehewa mabovu uliofanywa na Yusufu Manji kwa kushirikiana na waziri wa zamani wa uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe, iliyogharimu zaidi ya Sh. bilioni 200. Sumaye alitaja kashfa kubwa kuliko zote katika masuala ya umeme ya Escrow iliyobarikiwa na Ikulu na kusababisha mfanyabiashara kutoka Afrika Kusini, Harbinder Singh Sethi, kuchota kiasi cha shilingi bilioni 305 toka katika akaunti maalumu ya benki kuu ya Tanganyika ((Tanzania,)) Zanzibar mwaka 2013.
Sumaye aliorodhesha kashfa zingine chini ya utawala wa Rais Kikwete ikiwemo utoroshaji wa twiga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, Wizi wa shilingi bilioni 133 toka katika akaunti ya madeni ya nje maarufu kama EPA, huku akisisitiza kwamba utawala wa Kikwete ulijaa ufisadi kupindukia lakini viongozi wa CCM wanamtuhumu Lowassa kama kinara wa rushwa. Alisema viongozi wa CCM wamekuwa wakimshambulia Lowassa kwamba ni fisadi lakini tangu ametoka madarakani mwaka 2008, ameendelea kuwapo nchini na hajachukuliwa hatua na kwamba kama angekuwa fisadi kweli wasingemuacha. “Tangu lini waziri mkuu anakuwa mkubwa wa serikali, waziri mkuu anabebeshwa mzigo ili kumuokoa Rais wake,”alisema. Alisema Lowassa aliamua kuwajibika ili kuinusuru serikali isiumbuke,” alisema Sumaye na kusisitiza kwamba Lowassa alijitishwa mzigo ili kumuokoa Rais Kikwete na serikali yake. Sumaye alikumbusha kwamba Mwalimu Nyerere alilia katika kikao kimoja cha Halmashauri Kuu akimsifia Kawawa kwamba anabeba mzigo asiostahili kwa ajili yake (Nyerere). “Hivi twiga waliopandishwa kwenye ndege, Lowassa alikuwapo madarakani mbona alikuwa ameondoka toka 2008, EPA waliochota mabilioni Lowassa alikuwapo?” “Hivi madawa ya kulevya yanapopita uwanja wa ndege hadi yanakamatwa Afrika Kusini, Lowassa alikuwapo?, Vichwa vya treni vilivyonunuliwa Lowassa alikuwapo?, Feri mbovu zilizonunuliwa na kuonekana mpya Lowassa alikuwapo? wamelamba Escrow Lowassa alikuwapo?” Alihoji Sumaye Sumaye aliweka bayana kwamba katika ufisadi wa Escrow, waliokula hela za James Rugemalira walitajwa lakini wale waliochota sehemu kubwa ya fedha hizo toka benki ya Stanbic kwa kutumia sandarusi mpaka leo hawatajwi.
Alisema serikali ni dhaifu na Katibu Mkuu wa CCM alishalithibitisha hilo kwani alishanukuliwa akisema kuna mawaziri mizigo na kwa kiongozi kama huyo akisema hayo inatakiwa chama chake kiondoke madarakani: “Wewe hiyo ni serikali yako unakuja kushitaki kwa wananchi ni ajabu,” alihoji Sumaye. “Wanamsema Lowassa kuhusu ugonjwa, kwani Magufuli ni mzima na kama wao wanajiona ni wazima wanakwendaga kufanya nini Ulaya,” alihoji Sumaye. “Rais Mkapa alipougua si alikwenda nje kufanyiwa operesheni kubwa, Rais Kikwete naye si alikwenda nje kufanyiwa upasuaji wa tezi dume,” alisema Sumaye. Alisema urais siyo kazi ya kwenda kubeba zege Ikulu hivyo wananchi wana kila sababu ya kumchagua Lowassa, ili kufanya mabadiliko ya nchi .MASHA
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, alisema yeye na wenzake ambao wamejitoa CCM na kujiunga na Chadema, siyo kwamba ni makapi bali ni haki yao ya kidemokrasia na hiari yao: “Kwa tuliojiunga Chadema sisi siyo makapi, tuna akili zetu sawa tumetumia hiari yetu,” alisema Masha. Masha alisema wananchi wasihofu kwa yaliyotokea, yeye pamoja na vijana 19 kuwekwa ndani na Jeshi la Polisi kwa hivyo ni vitisho vya kuwatisha wananchi, lakini mabadiliko yapo pale pale.MBOWE
Akizindua ilani ya Chadema, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe jana alisema kuwa imejaa maslahi mapana ya taifa, na kusisitiza kwamba lazima CCM iondolewe madarakani mwaka huu.“Tunawashukru walioamua kupata ujasiri kuondoka CCM na kujiunga na Ukawa wakiongozwa na Lowassa na Sumaye, kwani kuja kwenu Ukawa kumeleta chachu katika vyama vinavyounda umoja huu,” alisema Mbowe. Alisema wananchi wameitwa malofa lakini, waliowaita hivyo walisahau kwamba wao watakuwa chanzo cha ulofa huo kwa vile wametawala kwa miongo zaidi ya mitano. Mbowe alitaka rais mstaafu Benjamini Mkapa, asamehewe kutokana na kauli aliyoitoa hivi karibuni pale alipowaita Watanganyika na Wazanzibari walio vyama vya upinzani ni ‘wapumbavu…malofa’.Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba alinukuliwa akisema mgombea urais wa CCM hana urafiki na matajiri.
Alisema Jaji Warioba, lazima atambue kuwa umaskini siyo sifa na wala Ukawa hautamani umaskini, Watanganyika na Wazanzibari wote wanatamani kuwa matajiri, wakati wa kutamani umaskini uwe sifa ya uongozi umepitwa na wakati. “Tumeridhika na Lowassa anaweza kuwa chachu ya mabadiliko na tuwaahidi tutafanya kampeni za kistaarabu,” alisema Mbowe. Mbatia
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema hivi sasa wakuu wa wilaya na vyombo vya usalama wanakutana Ngurundoto mkoani Arusha, kupanga uhalifu na hujuma na kumtaka Lowassa atembee na tenzi za rohoni. “Mhe Lowassa, Maalim Seif na Duni, umma wa watanganyika na wazanzibari utawalinda…Rais Kikwete asilete uchochezi ndani ya taifa hili, Tanganyika ((Tanzania)) Zanzibar ni mali ya wote siyo ya kikundi cha watu wachache,” alisema Mbatia. Alisema wameitwa malofa na wapumbavu lakini heri ya kijana maskini mwenye hekima kuliko mzee mfalme mpambavu.LOWASSA
Alisema akiingia madarakani kipaumbele chake cha kwanza hadi cha tatu kitakula elimu kwa kutoa elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu. Alisema jambo hilo linawezekana na hakuna mtu kwenye utawala wake atakayesema haiwezekani. “Nanukuu maneno ya aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, Tony Blair aliulizwa atafanya nini akiingia madarakani na kujibu kipaumbele changu cha kwanza kitakuwa elimu, cha pili elimu cha tatu elimu na jambo hilo liliwezekana, kwa nini sisi tushindwe,” alisema Lowassa.
Kuhusu afya alisema ataiboresha kwa kujenga hospitali na Watanganyika na Wazanzibari watatibiwa nchini kwa sababu wengi hawana uwezo wa kwenda nje. “Tunapoteza fedha nyingi kuwapeleka watu nje lakini wengi hawana uwezo wanaoenda huko ni watu wakubwa,” alisema. Akizungumzia mawasiliano alisema serikali yake itajenga reli ya kati kwa kiwango cha kisasa kutoka Dar es Salaam, Mwanza mpaka Kigoma na kufufua Shirika la Ndege kwa kununua ndege mpya na kulifanya lijiendeshe kibiashara. “Hatuna sababu ya kushindwa na nchi ndogo kama Rwanda, Malawi na Kenya ambazo wana ndege nzuri na mashirika yanayotambulika,” alisema Lowassa.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment