Wednesday, October 21, 2015

BREAK NEWS: ULINZI MKALI NI ISHARA YA CCM KUTAKA BADILISHA MATOKEO YA KURA KAMA WALIVYO ZOWEA.Asalamu alaikhum Warahmatullahi Wabarakatu Ndugu kutoka nchini Zanzibar na nchini Tanganyika. Mpaka sasa habari rasmi ambazo zinafanywa Siri Siri Nikwamba. Uchaguzi wa Jumapili utatokea katika misingi ya Amani . Lakini Matokeo ya Raisi Wa Muungano yani nchi ya Tanganyika Yatakuwa ya Staill Ile YA “BANDIKA BANDUA” Kwa Watu hapa nchini Zanzibar nikisema matokeo ya Uchaguzi ya Uraisi kama yatakuwa ni Bandika Bandua nafikiri watakuwa Wamenifahamu. Na naweza kusema kwamba nitawarejesha kwenye Maumivu na Majonzi yasiosahaulika Wakati wa uchaguzi 1995. Wakati matokeo ya Uraisi Maalim Seif Shariff Hamad Alishinda kwa Asilimia 52.6 lakini Matokeo yake Yakabadilishwa na Yale ya Maalim Akatangaziwa Salmin Amour na Yaslmini Amour akabandikwa nayo Maalim Seif Shariff Hamad ndio tukaita BANDIKA BANDUA.
Hivo na uchaguzi huu jinsi yakuona Vikosi na Ulinzi mkali uliowekwa na JESHI LA POLISI KULETEWA MAGARI MAPYA nikwamba CCM Wamekusudia kubadilisha matokeo katika Utangazaji wa matokeo hayo.. Nikwamba Wapinzani watakuwa Wameshakubaliana na chama Tawala kwamba Wao Ndio Wameshinda Uchaguzi lakini TUME YA UCHAGUZI NEC Itatangaza Vyengine ili iipe Ushindi CCM. Na Ndio maana hivi sasa Nchi Nzima kuna Majeshi na Mizinga ya Kivita kama vile nchi hizi mbili Zanzibar na Tanganyika zimo katika Hatari ya Vita Kuu ya DUNIA.Matokeo ya Uchaguzi yatatolewa siku moja baada ya yale ya nchi ya Tanganyika kutangazwa. Hii nikuwapa Fursa Viongozi wa CCM ambao wamezoea kuja nchini kwetu Zanzibar na kuwakaba ZEC waitangaze CCM badala ya Wapinzani.. Mara hii Akina Mkapa,Ali hassan mwinyi mzee wa kondom,Kinana na mwengine yoyote yule wakiingia hapa nchini kwetu Zanzibar basi Wasitoke kabisa.
UKAWA tunakuombeni muwe makini muwe makini muwe makini kweni hili tukilipa nafasi Watanganyika na Wazanzibari basi tuwe tayari kusota kwa miaka mengine 50. ila tunamini kabisa kwa jinsi CCM walivyo wafanya wananchi kuwa masikini wa kutupwa na kuwanyanyasa bila ya huruma huku wao CCM wakiongoza kwa ufisadi na kujirundikia mimali na majumba ya kifahari ni hakika wananchi hawatakubali kusoteshwa na kupigwa na Askari mwaka huu isipokuwa ni Kuichukua Serikali ya Muungano kwa Nguvu zetu zote. Kwa Upande wa Zanzibar na ZEC Wazanzibari tayari wameshagundua Watu Waliokufa Wameendelea Kupigiwa Kura na CCM lakini Mwaka huu Ikulu hakutakuwa kwa Raisi bali ni IKULU ya Wazanzibari wazanzibari wote watahamia IKULU na KUISHI HUMO HUMO IKULU MAANA NDIO KWENYE MAJI YA UHAKIKA NA UMEME WA UHAKIKA NA MILO MITATU YA SIKU HAIPIGI CHENGA BASI WAZANZIBARI SOTE TUTAHAMIA HUMO MPAKA TUWE N UHAKIKA WA HAYA YOTE MAJUMBANI KWETU NCHI YA ZANZIBAR YENYE MAMLAKA KAMILI.
Natanguliza Shukrani Zangu za Dhati.
 KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment