Monday, October 12, 2015

NCHINI TANGANYIKA MKAPA AWATAKA WANA CCM WAVUNJE MAKUNDI


Mkapa Awataka WanaCCM Wavunje Makundi......Asema Mtu Anayehama Chama ni Msaliti na Hafai kuwa Kiongozi huko nchini Tanganyika nchini Zanzibar wafuasi wa chama cha CCM nao wanasema katika mabango yao kubadili chama sio kuritadi je sikuchanganyikiwa huko....??


RAIS mstaafu Benjamin Mkapa amewaasa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuacha kambi ambazo ziliweza kusababisha majimbo mawili kuchukuliwa na Chama cha Wananchi (CUF) mkoani Lindi katika uchaguzi wa mwaka 2010.

Rais Mkapa aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Mpilipili mjini Lindi.

Alisema “acheni tabia hiyo kwani mchakato wa kumpata mgombea inakuwa na utaratibu wake na inapotekelezwa anapatikana mmoja ili apeperushe bendera ya chama”.

Mkapa alisema wale wote ambao walishiriki kwenye kura za maoni za kumtafuta mgombea ubunge, wanatakiwa kuwa wamoja wakishirikiana na yule aliyeteuliwa kuhakikisha chama kinashinda katika uchaguzi wa mwaka huu.

Alisema kwenye uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka huu tabia hiyo iachwe mara moja ili ushindi uwe wa CCM. Alisema mgombea anaposhindwa kwenye michakato hiyo ndiyo anasema mfumo mbaya wakati wote yeye alikuwapo mwanzo mpaka mwisho, akishashindwa anaamua kulalamika na kuhama chama.

Alimtaja mtu wa aina hiyo kuwa ni msaliti wa chama na hafai kuwa kiongozi. 
  
Kiongozi huyo mstaafu alisema mawaziri watatu waliokaa zaidi ya miaka 15 kwenye serikali ya CCM kuanzia uwaziri hadi uwaziri mkuu na kuondoka wakidai serikali hiyo haifai, wao ndio hawafai kuongoza nchi.

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment