Tuesday, October 13, 2015

NCHINI TANGANYIKA RAIS WA NAMIBIA AWAMBIA WASHIRIKI WA NAFASI MBALIMBALI KUKUBALI KUSHINDWA WATAKAPO SHINDWA KATIKA CHAGUZI

Monday, October 12, 2015
Rais wa Namibia Dk Hage Geingob amesema nchi za Afrika zinapaswa kuweka mazingira ya uwazi katika chaguzi zake ili kuondoa manung’uniko baina ya wanasiasa na vyama vitakavyoshindwa. Akizungumza na mabalozi mbalimbali wa Afrika jijini Dar es salaam nchini Tanganyika jana Jumatatu, Dk Geingob amesema mazingira ya chaguzi yakiwa wazi na yenye uhuru na haki yataepusha wasiwasi kwa wanasiasa kuhisi wameibiwa hali aliyosema inaweza kusababisha machafuko. 
Amewaambia mabalozi kuwa wakati umefika kwa viongozi wa Afrika kuboresha mifumo yao katika kuendesha chaguzi sambamba na kutoa fursa kwa watu kufanya chaguzi za kidemokrasia. “Ni lazima chaguzi ziendeshwe katika mazingira ya uwazi na ukweli, hii itaondoa wasiwasi na kuepusha malalamiko ya hisia za kuwepo kwa udanganyifu kwa wale wanaoshindwa” amesema.
Akizungumzia uchaguzi mkuu ujao, rais huyo wa Namibia amesema nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar ni visiwa vya amani na anayo imani kubwa kuwa uchaguzi wake utafanyika katika hali ya amani na vile vile utakuwa wa haki na huru.
Amewataka wanasiasa na wananchi wa nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu na kwa washiriki wa nafasi mbalimbali kukubali kushindwa watakapo shindwa katika uchaguzi na sio kutumia ubabe kwani havitawasaidiya mamba yatakapo haribika au nchi kuchafuka.
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment