Tuesday, October 27, 2015

NCHINI TANGANYIKA VIONGOZI WA UKAWA HAWAYATAMBUI MATOKEO YA URAIS YANAYO ENDELEA KUTANGAZWA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NEC


Viongozi  waandamizi  wa   UKAWA wamesema  hawayatambui matokeo ya Urais yanayoendelea kutangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi NEC kwa madai kuwa  yamehujumiwa. Kauli  hizo  za  kutoyatambua  matokeo  zimetolewa  na  Freeman  Mbowe,Profesa  Safari  na  James  Mbatia  wakati  wakiongea  na  vyombo  vya  habari  leo kuhusiana  na  mwenendo  wa  uchaguzi  mkuu. Mwenyekiti  wa  Chadema, Mh Freeman Mbowe  amesema  serikali  ya  CCM  imeamua  kuwatumia  wakurugenzi,NEC  na  jeshi  la  polisi  kupindua  maamuzi  ya  wananchi  na  kuamua  kutangaza  matokeo  ya  uongo. Mbowe  ametumia  muda mwingi  kulilaumu  jeshi  la  polisi  kuwakamata  Ma IT  wa  Chadema  waliokamatwa  wakijumlisha  matokeo  ya  Lowassa  jijini  Dar  es  Saalam, huku  professa  Safari  akieleza  jinsi  NEC  ilivyochakachua  matokeo....

"Nimesikitishwa na taarifa za kukamatwa kwa vijana wenzetu Wataalamu Wenzangu wa IT waliokuwa katika vituo vya majumuisho ya kura za mgombea Urais UKAWA."Huu ni UONEVU dhahiri kabisa. Inauma zaidi kwa wao kunyimwa kabisa dhamana.Hii si HAKI."Sitaki kuamini tumefikia hapa,sitaki kuamini uonevu wa kiasi hiki unatendeka kwa manufaa ya kisiasa."  Amesema  Mbowe

Katika  tamko  lake, Profesa  Safari  ametolea  mfano  jimbo  la  tandahimba  ambapo  amesema, kwa  mujibu  wa  matokeo  yaliyotangazwa  na NEC  katika  jimbo   hilo,Magufuli amepewa kura 49,098 huku  Lowassa  akiambulia  46,288

Kwa  mujibu  wa  Profesa  Safari, matokeo  halisi  waliyoyakusanya  toka  kwa  mawakala  wao  yanaonyesha  kuwa  Magufuli  ana  kura 44,253   huku  Lowassa  akiwa  na  kura 44,537

Kwa  upande  wake  Mwenyekiti  wa  NCCR  Mageuzi, James Mbatia  amesema  NEC  watachakachua  matokeo  lakini  sio  hisia  za  wananchi.

Viongozi  hao  wa  UKAWA  wamesema  kesho  Oktoba 28  watakutana  kwa  dharura  na  kutoa  msimamo  wao  kwa  wananchi  juu  ya  mwenendo  wa uchuguzi  mkuu

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment