Monday, October 26, 2015

NCHINI ZANZIBAR HALI ILIVYO HIVI PUNDE HUKO CHAKE CHAKE PEMBA VIJANA WASHEREHEKEA USHINDI CHAMA CHA WANANCHI CUF

pemba
Mambo hayapo shwari kidogo katika mji wa Chake Chake huko pemba, hii ni baada ya vijana wale ambao wanasema kuwa wanashrehekea ushindi wa Chama cha wananchi C.U.F ambayo ni haki yao kuingiliwa na jeshi la polisi katika msafara huo ambao unatokea maeneo mbali mbali, jeshi la polisi lilijaribu kusimamisha msafara huo kwa mara kadhaa kwa maneno na maonyo, lakini vijana hao ambao wengi walionekana wakiwa na furaha kubwa walishindwa kujizui kusherehekea na kuamua kuendelea na sherehe zao kwa amani na kushereheka jeshi la polisi la Kusini Pemba baada ya kuona hivyo liliamua kutumia guvu na kuanza kurusha mabomu ya gesi za kutoa machozi maarufu kama mabomu ya machozi,
Police wakionya vijana wanaosherehekea C.U.F
Police wakionya vijana wanaosherehekea wa chama cha wananchi C.U.F kwa tatizo nini siwako katika nchi yao wanafurahi ni uhuru wao kwa nini polisi iwaonye wasifurahi kama sio UDIKTETA KITU GANI BASI.........???
hakuna yeyote aloathirika na mabomu hayo kwani mabomu hayo yalirushwa kwa karibu nyuzi 85 na hivyo moshi kuishia angani. Hata hivyo vijana hao walibakia katika njia kuu baada ya kutoka mbio na baadae walirejea barabarani na kubadili njia kurudia kule wanakotoka.
Pemba
kwa taarifa nilopata hivi punde ni kuwa bado kuna makundi makubwa ya vijana ambayo yanakuja yakitokea maeneo ya Wete na Mkoani ya kisherehekea ushindi wa chama cha wananchi CUF. Nitazidi kukujuvya kipi kinaendelea katika eneo hili la Chake Chake kadiri ya uwezo wangu.

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment