Thursday, October 15, 2015

NCHINI ZANZIBAR MAALIM SEIF KUZINDUWA KUIFANYA NCHI YA ZANZIBAR KUWA SINGAPERI YA AFRIKA MASHARIKI


Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wafuasi wa chama cha CUF katika viwanja vya jimbo la Mkwajuni.

 Mwenyekiti wa Timu ya ushindi wa CUF Nassor Ahmed Mazrui, akiwahutubia wafuasi wa Chama cha CUF katika viwanja vya Mkwajuni.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa timu ya Ushindi CUF Ismail Jussa Ladhu, akionesha karatasi ya mfano ya kura ya urais wa Zanzibar yenye wagombea 14 wa Urais.

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhi kadi kwa mmoja kati ya vijana 39 wa CCM walio kikata chama cha CCM jimbo la Mkwajuni na kujiunga na chama cha CUF kupata mamlaka kamili ya nchi yao ya Zanzibar

 Wafuasi na wapenzi wa chama cha CUF wakifuatilia mkutano huo.

Wafuasi na wapenzi wa chama cha CUF wakifuatilia mkutano huo.

Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema anakusudia kuuzindua rasmi mpango wake wa kuifanya nchi ya Zanzibar kuwa Singapore ya Afrika Mashariki mwishoni mwa wiki hii. Amesema anapozungumzia mpango huo huwa hafanyi utani bali anazungumza akiwa na mikakati maalum ya kuweza kuibadilisha nchi ya Zanzibar kufikia lengo hilo. Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar ametoa kauli hiyo wakati akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa Chama hicho katika viwanja vya Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja. Amesema tayari chama hicho kimeshapanga mikakati imara ya kuweza kuikomboa nchi ya Zanzibar kiuchumi katika kipindi kifupi kijacho iwapo atachaguliwa kuiongoza na kuwa Rais wa nchi ya Zanzibar.

Akizungumzia mafanikio ya safari yake ya kichama nchini Afrika ya Kusini, amesema alikutana na viongozi wa makampuni mbali mbali ya nchi hiyo ambao walikubali kushirikiana nae kuikomboa nchi ya Zanzibar kiuchumi iwapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi mkuu ujao. Kuhusu matarajio ya ushindi kwa chama hicho Maalim Seif amesema kina matarajio makubwa ya kupata ushindi na kuapa kuwa hakuna atakayeweza kuzuia mabadiliko hayo. Amesema wananchi wa nchi ya Zanzibar wameshajiweka tayari kuleta mabadiliko na kuwahimiza kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuweza kufikia malengo hayo. Ameishauri Tume ya uchaguzi ya nchi ya Zanzibar kujiandaa kutoa matokeo ya uchaguzi mapema, ili kuzuia vurugu zinazoweza kuepukika. “Inawezekana kabisa kutoa matokeo siku hiyo hiyo kwa majimbo 54 ya nchi ya Zanzibar. Naamini kuwa ikifika saa sita za usiku matokeo yote ya nchi ya Zanzibar yatakuwa yamekamilika, hivyo Tume wajitahidi wayatangaze ili wananchi wapate kutulia” alieleza.

Maalim Seif amesisitiza haja ya kuwepo kwa uchaguzi wa amani, na kuwataka vijana wa chama hicho wasikubali kuchokozeka na kupelekea kuvunjika kwa amani ambayo ni hazina kubwa kwa taifa. Kuhusu Masheikh wa Jumuiya ya Uamsho wanaoshikiliwa na nchi ya Tanganyika, Maalim Seif amesema siku zao za kukaa ndani sasa zinahesabika kwani iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa ya Zanzibar atawarejesha masheikh hao hapa nchini Zanzibar ndani ya kipindi cha wiki moja baada ya kuapishwa. Nae Naibu Katibu Mkuu wa CUF nchini Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema iwapo Maalim Seif atachaguliwa kuwa Rais wa ya Zanzibar, atayarejesha yale yote yaliyoahidiwa na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za elimu na afya bila ya malipo. Mjumbe wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Janeth Fussi akizungumza katika mkutano huo amesema Maalim Seif anatosha na anavyo vigezo vyote vya kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi ya Zanzibar. Katika mkutano huo jumla ya vijana 39 wa jimbo la Mkwajuni kutoka chama cha CCM wamejiunga na Chama Cha Wananchi CUF na kukabidhiwa rasmi kadi za chama cha CUF baada ya kumkabidhi mgombea huyo wa Urais kadi zao.

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment