Wednesday, October 7, 2015

NCHINI ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD ATAVIUNDA UPYA VIKOSI VYA SMZ NA VITENDA KAZI NA KUIMARISHA MASLAHI YAO ENDAPO ATAPATA RIDHA YA WANANCHI KUWA RAIS WA NCHI YA ZANZIBAR


  Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya chama cha CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimkabidhi kadi ya CUF mmoja kati ya wanachama wapya waliojiunga na Chama hicho wakitokea CCM kutoka majimbo ya Kwahani na Shaurimoyo.

Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya chama cha CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wafuasi wa chama cha CUF katika viwanja vya Mkele unguja nchini Zanzibar.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa Timu ya Ushindi chama cha CUF Ismail Jussa Ladhu akiwahutubia wafuasi wa chama cha CUF katika viwanja vya Mkele nchini Zanzibar.

 Bi. Fat-hiya Salim akitoa salamu za wanawake katika mkutano wa kampeni za CUF uliofanyika viwanja vya Mkele.

Wafuasi wa chama cha CUF wakimsikiliza mgombea wao wa Urais Mhe Maalim Seif Shariff Hamad katika viwanja vya Mkele nchini Zanzibar

Wafuasi wa chama cha CUF wakimsikiliza mgombea wao wa Urais Mhe Maalim Seif Shariff Hamad katika viwanja vya Mkele nchini Zanzibar.

Wafuasi wachama cha  CUF wakiwa makini kusikiliza kampeni za mgombea Urais Mhe Maalim Seif Shariff Hamad katika viwanja vya Mkele nchini Zanzibar. 

Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya chama cha CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa nchi ya Zanzibar ataviunda upya vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuvipatia vitendea kazi na kuimarisha maslahi yao. Amesema vikosi hivyo viliundwa kwa malengo maalum lakini bado havijatimiza  malengo yake kutokana na mazingira duni ya kazi zao, jambo ambalo amesema katika uongozi wake atavijengea mazingira bora ili vifanye kazi kwa ufanisi. Maalim Seif Shariff Hamad ameeleza hayo katika viwanja vya Mkele mjini nchini Zanzibar, wakati akihutubia mkutano wa kampeni kwa ajili ya majimbo ya Kwahani na Shaurimoyo.

Amesema vikosi vyote vikiwemo KMKM, JKU, KVZ, Zimamoto na Chuo Cha Mafunzo, vitapatiwa vitendea kazi vya kisasa pamoja na kurekebisha mishahara na maposho zao, ili viweze kulingana na vikosi vya Muungano. Akizungumzia kikosi cha KMKM, Maalim Seif  Shariff Hamad amesema atakibadilisha jina na kukiita kikosi cha ulinzi wa bahari, na kukipatia zana zote zinazohitajika katika utendaji wao, ili kiweze kufuatilia pia usalama wa wananchi wanapokuwa baharini. Kuhusu Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Maalim Seif amesema mbali ya kuliwekea maslahi bora na vitendea kazi vya kisasa, pia ataliwekea mazingira ya kutoa utaalamu wa fani mbali mbali kwa vijana, ili watakapomaliza mafunzo yao waweze kujiajiri.

Amefahamisha kuwa kikosi cha zimamoto na uokozi kwa upande wake kitapatiwa zana za kutosha za uokozi pamoja na magari ya kuzimia moto ili kuweza kukabiliana vyema na majanga yanapotokea. Mapema akitoa salamu za  wanawake wa majimbo hayo, Bi Fat-hiya Salim, amewashauri wanawake kumchagua Maalim Seif Shariff Hamad ili aweze kutatua changamoto zinazowakabili zikiwemo huduma za afya.Amesema kwa muda mrefu wanawake wamekuwa wakihangaikia huduma hizo huku wakikabiliwa na mazingira magumu ya kimaisha, na kwamba iwapo watamchagua Maalim Seif Shariff Hamad ataweza kutatua changamoto hizo kwa kupatiwa huduma hizo bila ya malipo.Nae kijana Othmani Haji amesema bado vijana wengi wanashindwa kujitokeza hadharani kutokana na kuwaogopa wazazi wao ambao hawajataka kubadilika, lakini watakipigia kura chama cha CUF.

Ameelezea kufurahishwa na jinsi vijana wa majimbo hayo walivyohamasika kukiunga mkono Chama hicho na kutetea maslahi ya nchi yao, baada ya kutembelea barza saba za chama hicho katika majimbo hayo. Katika mkutano huo Maalim Seif Shariff Hamad amekabidhi kadi kwa wanachama wapya 26 kutoka majimbo ya Kwahani na Shaurimoyo ambao wamekihama Chama Cha Mapinduzi na kujiunga na chama cha CUF. Chama cha CUF kimesimamisha kampeni zake kupisha sherehe za sikukuu ya Eid El-Hajj zinazoanza tarehe 24/09/2015, ambapo amesema baada ya hapo kitatangaza maslahi kamili ya wafanyakazi na vikosi vya SMZ. ni habari iliyo toka kabla ya eid el hajji ila nimeiona nimuhimu sana.

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment