Tuesday, October 20, 2015

NCHINI ZANZIBAR-MAMBO YALIKUWA HIVI BUBUBU MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD ATAWEKA MAZINGIRA BORA KWA WAFANYA BIASHARA WAKUBWA NA WADOGO BILA YA KUWASAHAU JUWA KALI WATAKUWA NA MAKAZI MAZURI YA KUFANYA BIASHARA ZAO


 Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wafuasi wa Chama hicho cha CUF katika viwanja vya Kwageji Bububu.

Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wafuasi wa Chama hicho cha CUF katika viwanja vya Kwageji Bububu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Timu ya Ushindi CUF, Ismail Jussa Ladhu, akihutubia kwenye mkutano huo.


Wafuasi wa chama cha CUF wakisikiliza na kushangilia hotuba ya mgombea Urais wa Chama hicho cha CUF katika viwanja vya Kwageji Bububu.

Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameahidi kuweka mazingira bora kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa  nchi ya Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao. Akiwahutubia wafuasi wa Chama hicho cha CUF katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Kwageji Bububu, Maalim Seif amesema atarekebisha mfumo wa ushuru katika bandari ili kuepusha wafanyabiashara kulipa ushuru mara mbili wanaposafirisha mizigo yao kuelekea bandari ya jiji la Dar es Salaam huko nhini Tanganyika. Amesema hali hiyo imekuwa ikiwadhoofisha wafanyabiashara wa nchi ya Zanzibar, jambo amesema ataliwekea utaratibu mzuri, ili wafanyabiashara waweze kuendesha shughuli zao bila ya usumbufu.

Akizungumzia wafanyabiashara wadogo wadogo wakiwemo wale wa Jua kali, Maalim Seif amesema atawaekea mazingira mazuri kuweza kufanya shuguli zao. Amesema chini ya uongozi wake iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa nchi ya Zanzibar atahakikisha kuwa wafanyabiashara hao hawanyanyaswi, na watawekewa maeneo maalum ya kufanya biashara zao, na kwamba hakutokuwa na ulipaji wa kodi zisizotambulika katika maeneo yao. Aidha ameahidi kuanzisha benki ya uwekezaji, ili kukuza mitaji ya wafanyabiashara wadogo wadogo. Nae afisa uchaguzi wa CUF Bw. Muhene Said Rashid, amewataka wanachama hao kuweka utaratibu mzuri wa kuwasaidia wasioweza kupiga kura wakiwemo wagonjwa, wazee na wenye ulemavu,  ili kila aliyejiandikisha aweze kupiga kura kwa mgombea anayemtaka. Aidha amewataka kuelimishana juu ya namna ya upigaji kura, ili kuepuka uharibifu wa kura na kupiga kura kwa usahihi.

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment