Wednesday, October 7, 2015

NCHINI ZANZIBAR MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA CCM SHEIN AKIENDELEA NA KAMPENI NA KUHUTUBIA WANANCHI WA NUNGWI.


Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi Shein akihutubia mkutano kampeni katika mji mdogo wa Nungwi katika mkoa wa Kaskazini Unguja nchini Zanzibar na kuwataka wananchi kukichagua chama hicho kwa kuwa ndicho kinachothamini na kinachotekeleza malengo ya Mapinduzi ya mwaka 1964.
Aliwaambia wananchi waliohudhuria mkutano huo kuwa wanapaswa kuichagua CCM kwani ndicho chama chenye uwezo na kimeonesha mfano wa utekelezaji wa malengo ya Mapinduzi na ahadi za Rais wa kwanza wa Zanzibar hayati Mzee Abeid Amani Karume.(( mzee karume kajenga majumba ya michezani wewe umejenga mnara ndio umetekeleza sasa watu wanaishi kwenye minara...?))

“Mapinduzi ndiyo yaliyoweka msingi wa usawa na kuondosha ubaguzi ambao uliwanyima haki na kuwakandamiza wananchi walio wengi wa Zanzibar” Shein alieleza.((wabaguzi wakubwa wanafunzi wangapi mumewafelisha kisa wapemba,wafanyakazi wangape wamefukuzwa kazi kisa wapemba,vitambulisha zanzibar ID ni kwa kila mwananchi mapaka leo kama sio mkereketwa hupewi,paspoti ni haki ya kila rai hamuwapi mpaka mtu awe mwana maskani n.k ))
Katika mnasaba huo alisema kuwa Mapinduzi yalileta usawa na kujenga mazingira ya kuijenga nchi yetu kwa ushirikiano na kwa umoja wetu na kwa maslahi yetu wote. Mgombea huyo wa CCM alisema Zanzibar ni maarufu ulimwenguni kote tokea karme nyingi zilizopita lakini umaarufu huo hautakuwa na manufaa kwetu endapo hatutaweza kulinda na kuienzi amani na utulivu uliopo.Katika kipindi kijacho aliahidi kuimarisha huduma za jamii ikiwemo elimu, afya, umeme na maji pamoja na miundombinu ya barabara ili kukidhi mahitaji makubwa ya huduma hizo kutokana na mji huo kupanuka sana kutokana na shughuli za biashara ya utalii.

(( Hivi wewe umesoma kweli au unaupumbavu katika elimu yako umekuwa mpumbavu badala ya kuwa mwerevu miaka mitano imemalizika ulikuwa ukiuza majengo ya serekali na kusema wewe ni mwenyewe unauza chako kisha ukajenga mnara wako kisonge sasa ati watu wakupe miaka mengine mitani ndio uwape.......kuimarisha huduma za jamii ikiwemo elimu, afya, umeme na maji pamoja na miundombinu ya barabara ili kukidhi mahitaji makubwa ya huduma hizo kutokana na mji huo kupanuka sana kutokana na shughuli za biashara ya utalii.inaonyesha wazi huna nia jemaa ila nia yako iko kwa sababu ya watali na sio wananchi Mzanzibari atakae kupigia kura wewe atakuwa amerengwa.))
“Tutaimarisha huduma za umeme kwa kuweka transfoma kubwa yenye KVA 200 katika mji mpya ulioko Ras Nungwi itakayoweza kuhudumia wateja wengi na kwa uhakika zaidi” Dk. Shein alisema na kuongeza kuwa mji huo mdogo utawekewa taa za barabarani hadi Kivunge.((kasome historia watu walikuwa na umeme barabarani kabla ya london U.K.nchi hii sio ya kutiwa umeme wabarabarani leo na wewe kujifanya kama umefanya jambo kubwa wakati hayo yote yalikuwa yawe tayari yashafanywa na sasa tuko mbali lakini wapi CCM mafisadi na kujaza matumbo yenu na mahawara wenu na watoto wenu wa kharamu ndio munalolijuwa mda mtaupata wapi wakuleta maendeleo na nyinyi mko bizi kuiba na kujitajirisha na familia zenu...?))

Shein aliwaeleza wananchi hao kuwa biashara ya utalii ndio inayoipatia Zanzibar fedha nyingi za kigeni hivyo lengo la Serikali katika miaka mitano ijayo ni kuongeza idadi ya watalii wanoitembelea Zanzibar ifikie 500,000 ifikapo 2020 kutoka 300,000 hivi sasa huku jitihada zikielekezwa katika kuimarisha uwezo wa wananchi kitaaluma wa kuweza kuhudumia sekta hiyo. 
Aliwaeleza wananchi hao kuwa kupanua haraka kwa mji Nungwi ni uthibitisho kuwa Nungwi inaendelea kusonga mbele kwa kujenga majengo mengi na hoteli nyingi za kitalii.
Shein aliahidi atakapochaguliwa tena Serikali yake itawajengea uwezo wavuvi nchini kwa kuwapatia boti zenye ukubwa wa kati na kubwa ili waweze kuvua kwa uhakika na kupata mapato makubwa zaidi.Kwa upande wa kilimo cha mwani, Shein alisema ataiamarisha masoko la mwani kwa kutafuta masoko mapya ya zao hilo ili wakulima waweze kupata bei nzuri na kufaidi jasho lao. 
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment