Wednesday, October 21, 2015

NCHINI ZANZIBAR MKUTANO WA KUFUNGA KAMPENI WA CHAMA CHA CUF TIBIRINZI,PEMBAMGOMBEA Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha wananchi CUF Mhe: Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wanachama na wafuasi wa chama cha wananchi CUF katika mkutano wa kufunga kampeni kisiwani Pemba uliofanyika viwanja vya Tibirinzi.

Mgombea Uwakilishi wa jimbo la Malindi, Mhe Ismail Jussa akimwaga sera na kuwanasihi wafuasi wa chama cha CUF na wananchi wote kwa ujumla kuwapigia kura viongozi wao katika mkutano kufunga kampeni katika viwanja vya Tibirinzi Pemba.

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Maji Mkongwe, Mhe Sanya akiwanasihi wafuasi wa chama cha wananchi CUF na wananchi wote walio jitokeza katika mkutano huo kuwapigia kura viongozi wao katika mkutano kufunga kampeni katika viwanja vya Tibirinzi Pemba.
Watoa huduma ya kwanza wakimbeba mmoja wa waliohudhuria Mkutano wa chama cha wananchi CUF baada ya kuzimia kwa wingi wa watu

Wapenzi na wafuasi wa chama cha wananchi CUF na wananchi wote kwa ujumla waliohudhuria mkutano wa kufunga kampeni katika viwanja vya Tibirinzi Pemba.
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment