Tuesday, October 13, 2015

NCHINI ZANZIBAR MKUTANO WA KAMPENI WA CCM UWANJA WA MISUKA MAHONDA JIMBO LA DONGE


Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Taifa (NEC) Balozi Seif Iddi ambaye ni balozi mdogo wa nchi ya Tanganyika ishie nchini Zanzibar akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakati alipowasili katika uwanja wa Misuka katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM katika jimbo la Donge mkoa wa Kaskazini Unguja nchini Zanzibar.


 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum Haji Omar Kheir akiwasalimia wananchi na wanachama wa Jimbo la Donge wilaya ya Kaskazini B Unguja wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo uwanja wa Misuka Mahonda.


 Aliyekuwa Balozi  Umoja wa Afrika nchini Marekani Mama Amina Salum Ali lipi kawafanyia Wazanzibari kwa kuwa Balozi Umoja wa Afrika nchini Marekani...? tonge ishakwisha sasa anakuja kuomba tonge kisha hamumsiki tena mpaka baada ya ya miaka mitano. akiwasalimia Maelfu ya Wananchi na Wanachama wa CCM Jimbo la Donge Wilaya ya Kaskazini B Unguja katika  mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo uwanja wa Misuka Mahonda,ambao mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Shein.

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban akitoa ufafanuzi kuhusu suala la Mafuta kwa wananchi wa Jimbo la Donge katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi zilizofanyika leo katika uwanja wa Misuka Mahonda Wilaya ya Kaskazini B Unguja.


Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Shein akiwasalimia wananchi na wanaCCM wakati alipozungumza nao katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM  uliofanyika leo katika uwanja wa Misuka Mahonda,Wilaya ya Kaskazini B Mkoa wa Kaskazini Unguja  Jimbo la Donge, katika mwendelezo wa Mikutano mbalimbali  ya hadhara katika Mikoa ya Unguja na Pemba.KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment