Tuesday, October 20, 2015

NCHINI ZANZIBAR-MKUTANO WA KAMPENI ZA CHAMA CHA WANANCHI CUF JIMBO LA NUNGWI WAFANYIKA KATIKA FUKWE ZA BAHARI YA NUNGWI JINSI WATU WALIVYOJITOKEZA KWA WINGI


Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya chama cha CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhiwa jahazi na wazee wa Nungwi kwenye mkutano wa chama hicho uliofanyika katika fukwe za Nungwi baada ya viwanja vya sokoni Nungwi kuwa vidogo kwa umati wa watu ulivyokuwa mkubwa.

Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya chama cha CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wafuasi wa chama hicho cha wananchi CUF katika fukwe za Nungwi baada ya viwanja vya sokoni Nungwi kuwa vidogo.

Wafuasi wa chama cha wananchi CUF walivyojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika fukwe za Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja amini usiamni ndio hali ilivyo hivi.

Wafuasi wa chama cha wananchi CUF walivyojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika fukwe za bahari za Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Wafuasi wa chama cha wananchi CUF walivyomiminika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika fukwe za bahari ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Wafuasi wa chama cha wananchi CUF walivyojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika fukwe za bahari ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Chama Cha Wananchi CUF, kimelazimika kufanya mkutano wake wa hadhara katika fukwe za Nungwi, baada ya kiwanja cha Sokoni Nungwi kuonekana kuwa kidogo kutokana na idadi kubwa ya wanachama waliojitokeza kwenye mkutano huo.Katika mkutano huo wa kampeni Jimbo la Nungwi, mgeni rasmi alikuwa Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad. Akizungumza katika mkutano huo, Maalim Seif amesema hakuna sababu kwa Chama hicho kukosa ushindi katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 mwezi huu kutokana na kuungwa mkono na wanachama wengi katika maeneo yote ya nchi ya Zanzibar. Ameelezea kufurahishwa na jinsi wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja walivyohamasika kukiunga mkono Chama hicho, na kwamba huo ni ushahidi tosha wa kukiweka chama hicho madarakani.

Amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa nchi ya Zanzibar, atashughulikia migogoro ya ardhi inayojitokeza katika Mkoa huo, baada ya maeneo kadhaa ya wananchi kupewa wawekezaji bila ya utaratibu unaokubalika. Aidha amerejea kauli yake ya kuwarejesha nchi Zanzibar Masheikh wa Jumuiya ya Uamsho wanaoshikiliwa nchi ya Tanganyika, wiki moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa nchi ya Zanzibar na kwamba kesi yao itasikilizwa katika Mahakama ya nchi ya Zanzibar. Amemshauri Rais wa Zanzibar kuwadhibiti viongozi wa CCM wenye dhamira ya kuleta vurugu nchini, ili uchaguzi ujao ufanyike katika hali ya amani na usalama. Nae Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo nchini Zanzibar Bw. Salum Mwalim, amewataka mawakala kuwa makini katika kusimamia kura za wagombea wao.

Amesema vyama vinavyounda Umoja wa UKAWA havitomvumilia wakala atakayefanya uzembe katika usimamizi wa kura, na kwamba atakayebainika atawajibishwa. Kabla ya Mkutano huo Maalim Seif alitembelea na kufungua barza mbali mbali za Chama hicho ikiwemo barza ya New Singapore katika kijiji cha Bwereu Kitogani, na kuelezea kufarajika kwake kutokana na namna vijana walivyojipanga kukipatia chama hicho ushindi katika uchaguzi ujao. Wazee wa Nungwi kwa upande wao wamemkabidhi jahazi Maalim Seif, ili aweze kuliongoza hadi kufikia kupatikana kwa mamlaka kamili ya nchi ya Zanzibar.

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment