Wednesday, October 7, 2015

NCHINI ZANZIBAR MKUTANO WA VYAMA VINAVYOUNDA UKAWA WAWI,CHAKECHAKE PEMBA


MGOMBEA urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF Mhe: Maalim Seif Sharif Hamad akivishwa koja, kabla ya kuzungumza na mamia ya wanachama wa vyama vinavyounda UKAWA, uliofanyika Ditia Jimbo la Wawi wilaya ya Chake chake Pemba.

MJUMBE wa baraza kuu taifa la chama cha CHADEMA Janeth Madadi Fussi, akitoa salamu zake kwa mamia ya wanachama wa vyama vinavyounda UKAWA na chama cha CUF, kwenye mkutano uliofanyika Ditia, Jimbo la Wawi wilaya ya Chake chake Pemba, na kuhutubiwa na mgombea urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya chama cha CUF maalim Seif Sharif Hamad.

KADA wa chama cha wananchi CUF bwana Sanya akizungumza kwenye mkutano wa kuwanadi wagombea wa Majimbo ya Chake chake na Wawi na wadi zake, uliofanyika uwanja wa Ditia Jimbo la Wawi na kuhutubiwa na mgombea urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho, maalim Seif Sharif Hamad.

 MGOMBEA urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya chama cha  CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akimnadi mgombea Udiwani wa wadi ya Tibirinzi Mohamed Hafidh Ngwidi, kabla ya kuzungumza na wanachama wa chama hicho, kwenye mkutano uliofanyika Ditia Jimbo la Wawi.

 MGOMBEA urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya chama cha CUF maalims Seif Sharif Hamad, akimnadi mgombea Ubunge Jimbo la Chake chake Yussuf Kaiza Makame, kabla ya kuzungumza na wanachama wa chama hicho, kwenye mkutano uliofanyika Ditia Jimbo la Wawi.

MGOMBEA urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha wananchi CUF Mhe: maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wanachamawa chama cha CUF na vyama vinavyounga umoja wa UKAWA, kwenye mkutano wa kuwanadi wagombea wa nafasi mbali mbali wa majimbo ya Wawi na Chake chake, mkutano huo ulifanyika Ditia Jimbo la Wawi.

WANACHAMA wa chama cha CUF na wengine wanaounda UKAWA, wakifuatilia hutuba ya mgombea urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya chama cha CUF maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza kwenye mkutano wa kuwanadi wagombea wa majimbo ya Chake chake na Wawi pamoja na wadi zake
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment