Wednesday, October 21, 2015

NCHINI ZANZIBAR SHEIN AJA NA MPYA YA KUIFANYA ZANZIBAR KUWA KAMA DUBAI MIAKA 50 CCM IMESHINDWA MIAKA 5 SHEIN UMESHINDWA KUIFANYA ZANZIBAR DUBAI MNAMDANGANYA NANI....???
Nchini Zanzibar. Mgombea urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Shein amesema akichaguliwa atavifanya visiwa hivyo vya nchi ya Zanzibar kuwa mji wa kisasa wenye hoteli za nyota tano, viwanda na uwanja wa kimataifa wa mpira. Akihutubia wana wa CCM na wafuasi wa chama hicho walio baki kwenye mkutano wake wa 25 wa kampeni za uchaguzi uliofanyika katika Jimbo la Dimani, Mkoa wa Mjini Magharibi, Shein alisema nchi ya Zanzibar itafanya na miji mikubwa duniani kama Dubai. Alisema tayari kuna eneo maalumu kwa ajili ya ujenzi huo ambalo limeshatengwa katika eneo la Fumba na kwamba kiwanda cha kisasa cha kuzalisha maziwa cha Azam kimeshaanza kazi. Alisema katika eneo hilo, pia utajengwa uwanja wa mpira wa kimataifa utakaokuwa na uwezo wa kuchukua watu 45,000. “Mji wa Fumba utakuwa eneo huru la uwekezaji, yatajengwa majengo yenye zaidi ya ghorofa 20 kwa ajili ya makazi na wanaofanya kazi hii ni wawekezaji kwa kushirikiana na Serikali.
“Mradi huo utasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa Wazanzibari, wasikudanganyeni wapinzani kwa ahadi hewa, ninachokisema ni mipango ya Serikali inatolewa na rais wengine waongo,” alisema. Alisema Serikali inaingia makubaliano kampuni mbalimbali nchi kuhusiana na miradi hiyo akawataka wananchi wamchague ili aiendeleze. Akiuzungumzia Mji Mkongwe, alisema Serikali itaendelea kuwatumia wawekezaji kwa ajili ya kuyafanyia ukarabati majengo ya Mji Mkongwe ili yaweze kuendeleza historia na kuingizia mapato kupitia utalii. “Tutalinda historia ya Zanzibar kwa kuboresha majengo ya Mji Mkongwe bila kuathiri mwonekano wake ili kuboresha sekta ya utalii,” alisema. Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Balozi Seif Ali Iddi alisema maendeleo yaliyopatikana Zanzibar yameletwa na CCM hivyo akawataka wananchi kukichagua chama hicho ili kuendeleza mambo yaliyobaki. Kwa upande wake, Katibu wa Oganaizesheni ya CCM Taifa, Dk Mohamed Seif Khatib aliwataka wananchi waipe kura CCM ili iweze kudumisha Muungano. Alisema kamwe Wazanzibar wasifanye uchaguzi huu kwa majaribio, bali wakichague chama chenye rekodi ya kudumisha amani na mshikamano.
Tunawauliza hawa CCM miaka 50 na ushaiya wameshindwa kuifanya Zanzibar kuwa na miji mikubwa kama Dubai wataweza sasa miaka mitano ijayo wanawadanganya nani..? wanasema majumba ya mji mkongwe watayajenga kwa nini hawakuyajenga miaka yote hiyo 50 na ushaiya na hata hii miaka mitano iliyo pita kwa nini hamukuyajenga...? badala yake Shein ulikuwa ukiuza majengo na kisha ukisema kwenye vyombo vya habari kuwa mtu akiuza chake analaumiwa vipi au ushasahau Shein...? kuhusu kufanya Zanzibar iwe kama Dubai Shein miaka mitano umeka madaraka kwanini hukuifanya iwe Dubai....? badala yake miaka mitano umeipoteza kujenga mnara wa kifisadi ndio Dubai yako au sio pale mnarani....? umeme umewashinda mpaka leo bado mnapiga magoti kwa nchi ya Tanganyika mkiwakera wanazima kwisha jeuri yenu maji mpaka leo hamjawapa wananchi maji ya uhakika bomba moja kijiji kizima ndi maendeleo hayo....?
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment