Wednesday, October 21, 2015

NCHINI ZANZIBAR UFUNGAJI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI KWA CHAMA CHA CCM JIMBO LA KIJITO UPELE


Balozi Seif akimnadi kwa wapiga kura mgombea nafasi ya Ubunge kupitia chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Kijito Upele Mh. Shamsi Vuai Nahodha.


Balozi Seif akimnadi kwa wanachama wa ccm na Wananchi Mgombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Kijito Upele kupitia CCM Nd. Ali Suleiman Shihata.


Mmoja wa Waangalizi wa Uchaguzi Nchini nchini Zanzibar akiwajibika kuchukuwa matukio mbali mbali kwenye kampeni za uchaguzi Jimbo la Kijito Upele zilizofanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Taveta Magirisi Wilaya ya Magharibi”B”. mkutano wa CCMMwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi nchini Zanzibar Balozi Mkazi alisema kwamba kauli za Viongozi wa Upinzani za kuleta ubaguzi ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa ((Tanzania)) ni ufisadi unaofaa kukemewa na ((Watanzania)) wote wapenda amani na Umoja. Alisema ((Watanzania)) ambao tayari wameshachanganya damu kwa zaidi ya karne sasa na hatimae Umoja wao kurasimishwa rasmi kupitia Muungano wa April 26 Mwaka 1964 hawatakuwa tayari kuona kasumba za kusababisha ubaguzi kati ya ((Watanzania Bara)) na Wazanzibari zinaendelezwa wakati huu. Balozi Mkazi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM alisema hayo wakati akifunga rasmi Mikutano ya Kampeni ya Uchaguzi ya  Chama cha Mapinduzi Jimbo la Kijito Upele hapo  kwenye uwanja wa Michezo wa Taveta Magirisi Wilaya ya Magharibi “B”. Alisema mchakato wa kutafuta Katiba Mpya ya ((Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania)) uliojumuisha Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba kutoka vyama vyote vya Kisiasa Nchini ((Tanzania)) umeshuhudiwa na Wananchi wote jinsi kambi ya Upinzani ilivyosusia na kuamua kutoka nje ya Bunge hilo.

Balozi Mkazi huyo alifahamisha kwamba kitendo hicho kimethibitisha wazi kwamba upinzani bado mbali ya kuwa hauna uwezo wa kuongoza Dola ya ((Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania))  lakini pia unaonyesha wazi kwamba hauko tayari kupewa dhamana ya kuwahudumia ((Watanzania.)) Aliwaomba Wananchi na kuwasisitiza kuwa  wakati umefika kwao katika kuuhukumu upande wa Upinzani uliounda umoja wa Ukawa kwa kuunyima kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwishoni mwa Wiki hii katika nafasi zote za Uongozi kuanzia Udiwani, Wabunge, Wawakilishi, Urais wa nchi ya Zanzibar na Urais wa ((Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.)) “Ile siku yetu ya kuwahukumu wale wenzetu wa vyama vya siasa waliounda Ukawa umewadia na lazima tuwakatae hadharani kwa kutowapa kura hata moja katika nafasi zote za Uongozi  ifikapo Jumapili “. Alisema Balozi Mkazi huyo. Akizungumzia suala la Amani Balozi Mkazi alisema Serikali pamoja na Wananchi wote wapenda amani wanahitaji kuiona nchi inaendelea kubakia katika misingi  hiyo itakayowawezesha waendelee na shughuli zao za kimaisha mara tu baada ya uchaguzi Mkuu.

Balozi Mkazi akiendelea kusema katika mkutano huo kuwa vyombo vya dola vitakuwa makini katika kuwachukulia hatua za kisheria watu walioamua kutumiwa katika kufanya vurugu na akawaonya vijana watakaokubali kutumiwa katika uzembe huo. Balozi Seif aliwaonya na kuwatanabahisha wazazi kuwaasa vijana wao kujiepusha na mtego huo ambao mara nyingi wahusika wakuu pamoja na familia zao wanakuwa mbali mara tu baada ya kupanga mipango hiyo miovu. Aliwathibitishia Wananchi wenye asili ya Tanganyika wanaoishi hapa Zanzibar katika Maeneo na mitaa mbali mbali kwamba  kwamba  waendelee kuishi kwa amani na utulivu licha ya vitisho vilivyoanza kutolewa na baadhi ya Viongozi wa Upande wa Upinzani. Mjumbe  huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM aliwaomba Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi wote kwenda kupiga kura ifikapo Tarehe 25 kwa kuwachagua Viongozi wanaowakubali kutokana na Sera zao na kurejea nyumbani.

Alisema mtego unaoandaliwa na baadhi ya Viongozi wa Kisiasa kwa kuyatumia makundi ya wafuasi wa vyama vyao wa kutaka kubakia kwenye maeneo ya kupiga kura kwa madai ya kulinda kura wawawachie wenyewe shari yao itakayokuja wadhuru wenyewe. Akimkaribisha mgeni rasmi katika Mkutano huo wa Kampeni ya uchaguzi ya Jimbo la Kijito Upele Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi Ndugu Yussuf Moh’d Yussuf alisema ushindi wa CCM uko wazi kutokana na Viongozi wa Upinzani  kuanza kuchanganyikiwa katika Mikutano yao ya Kampeni iliyojaa matusi na kashfa. Nd. Yussuf aliwataka Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wajiandae kusherehekea ushindi wao kwa amani na utulivu kwa vile utekelezaji mkubwa wa ilani na Sera za CCM mwaka 201 -2015 umevunja rekondi ya ufanisi katika uimarishaji wa miradi ya kiuchumi, Kijamii pamoja na Maendeleo. Mwenyekiti huyo wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi aliwanasihi Wanachama wa Chama cha Wananchi { CUF } kujiepusha mapema na ushawishi unaoandaliwa na Viongozi wao wa kuwaagiza wajiweke tayari kwa kufanya .vurugu baada ya kushindwa katika uchaguzi Mkuu unaoonyesha dalili zote.

Katika Mkutano huo wa ufungaji wa Kampeni ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi Jimbo la Kijito Upele  Balozi Mkazi aliwanadi wagombea nafasi mbali mbali za Uongozi wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi. Wagombea hao ni Nd. Shamsi Vuai Nahodha Nafasi ya Ubunge, Nd. Ali Suleiman Shihata  nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, Nd. Saleh Yahya Saleh  nafsi ya Udiwani Wadi ya Kijito Upele, na Nd.Saleh Juma Kinana  Udiwani Wadi ya Meli Nne. Wakiomba kura kwa Wana CCM na Wananchi wa Jimbo hilo la Kijito Upele Wagombea hao wameahidi kusimamia vyema Sera na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015 – 2020 ambayo wana uwezo nayo katika kuwaletea maendeleo Wananchi wa Jimbo hilo la Kijito Upele.

Mh. Shamsi Vuai Nahodha anayewania nafasi ya Ubunge Jimbo la Kijito Upele alisema katika kukabiliana na usumbufu wa huduma ya maji safi na salama Wakipewa ridhaa ya kuingia madarakani kazi yao ya mwanzo ni kuchimba Visima Vinne vitakavyoondoa tatizo la huduma za maji safi na salama katika wadi na shahia za Jimbo hilo.

Mh. Shamsi alisema suala la usafiri kwa wanafunzi wa Jimbo hilo utapewa kipaumbele na Uongozi wao kwa kununua Mabasi Manne yatakayotoa huduma za usafi wanafunzi wa Jimbo hilo wa kwenda na kurudi Maskulini.Naye Mh. Ali Suleiman Shihata anayewania nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi aliahidi kutoa shilingi Milioni  Mia Moja  taslim { 100,000,000/-} endapo watampa ridhaa  ndani ya kipindi cha miezi Minne  mara tuu baada ya kuchaguliwa kwao. Fedha hizo zitaelekezwa katika kuviimarisha Vikundi vya ushirikia, Vikoba pamoja na saccos za Wananchi walioamua kujikusanya pamoja na kuunda vikundi hivyo lengo likiwa ni kujikwamua na ukali wa maisha na kupunguza umaskini miongoni mwa Jamii.

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment