Saturday, October 24, 2015

WASIA WA NDUGU ZETU WA ((UAMSHO)) WALIOKO NDANI


Mwana Familia
Kawaida kila week hupewa siku moja ya kuweza kuonana na mdogo wetu ambae yuko ndani kwa tuhuma za Kesi ya Ugaidi ( Uamsho) mara nyingi tukionana nae ilikua tunaweza kupata muda angalau wa dakika 20 kuweza kuzungumza na wana familia hata kama mbele yetu husimamiwa na Askari wa magereza lakini tunazungumza sana yale mambo yanayo husiana na yeye hali yake na kumuliza hali za wenzake walomo ndani.
Lakini hali ya jana ilitushangaza sana visitors kutokana na ulinzi mkali ulio kuwepo na hawakutaka kuturuhusu sote wana familia kwenda waliruhusu mtu moja tu kwenda na wengine mbakie , mimi nilipata bahati hio kwa vile ni kaka mshukiwa na nilingia na kwenda kumuona na kwa bahati yule askari wa Magereza alie tusimamia anafahamiana na mdogo wangu na akamuomba atupe faraha kidogo kuna mambo ya kifamilia tunataka kuzungumza muhimu.
Alikubali na akaondoka kidogo , kikubwa alichonambia nikusema hali ikoje huko uraiani...??? sisi humu ndani tuna matumaini makubwa In Shaa Allah kwa Uwezo wa M/mungu tukatako na mambo yakabadilika lakini uhakika nikua hali sio mzuru humu na wengi wetu ni wagonjwa na kama unavyo jua kifungo ni gereza na huna uhuru wala husaminiki na hasa gereza zetu hizi za kiafrica na kosa tulilofungiwa ni chuki tu zakisiasa, lakini sisi tunamtegemea Allah zaidi na nyiyi huko nje musitusaliti .
Mimi nikamuliza kusaliti vipi akasema kuipigia kura CCM nisawa na kutusaliti na sisi humu tulimo na yoyote atakaye fanya hivyo basi sisi tunaomba madua makubwa makubwa yakuweza kumshtakia M/mungu na dhulma zote tunazo fanyiwa kwahio ikiwa mtu yoyote atatusaliti kwa njia hii au nyingine basi na yeye kachangia kutukandamiza na atakua miongoni mwahao waliokua wameiwacha haki na kuingia katika batli.KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment