Friday, November 13, 2015

CCM ZANZIBAR IMESHINDWA VIBAYA VIONGOZI WA CCM HAWATAKI KUONDOKA MADARAKANI MAANA HAWAJUWI WATAWALISHA VIPI MAHAWARA WAO NA WATOTO WAO WALIO ZA NA MAHAWARA NJE YA DOWA KAZI IPO

11046516_10153084924781459_1465526352091690252_n
m
HAIJAWAHI kutokea serikali za wafadhili wa jamhuri kushikilia jambo wasiloliamini. Haijawahi kutokea, hata kama laweza kuwa na maslahi makubwa ya nchi zao.Mara nyingi hawa Wazungu, wakilishikilia jambo, wanauhakika na wanachokisema. Wanayo hoja na haibishaniki kiakili, labda kimazingaombwe.Sasa unapolitazama suala la mgogoro wa kipuuzi wa uchaguzi wa nchi ya Zanzibar, hupati shaka Wazungu wanauhakika na wanachoshikilia kusema kwamba “hawaioni hoja ya msingi kuitisha uchaguzi mpya hapa nchini Zanzibar.”Hawaioni kisheria na wala kimaadili. Wataionaje hoja wakati mpaka uchaguzi unafutwa mchana wa Oktoba 28, mezani hakukuwa na lalamiko hata moja la CCM....?? Kwa sababu hiyo basi, Marekani, Uingereza, Canada, Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola, si wapuuzi kama wale walioitia nchi ya Zanzibar katika shimo kwa sababu za kukidhi maslahi ya kihafidhina na maradhi walio nayo ya BT Bora Tumbo.John Kerry, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, anamwambia Dk. John Magufuli, rais mpya wa Tanganyika ((Tanzania,)) kwamba ushirikiano kati ya nchi zao utakuwa mzuri zaidi ukishughulikiwa ipasavyo mgogoro wa uchaguzi wa nchi ya Zanzibar.Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya nchini, naye anakumbusha hayohayo – hakuna hoja hata moja ya kuhalalisha kuitishwa kwa uchaguzi mwingine nchini Zanzibar baada ya ule uliofanyika Oktoba 25 na kuelezwa na wote hao kuwa ulikuwa uchaguzi mzuri kuliko wa 2010.Kwa kushikilia hoja hii – ya kutoiona sababu yoyote ya kisheria wala kimaadili ya kufanywa uchaguzi mwingine hapa nchini Zanzibar – Wazungu wanaamini, kwa watu wenye akili timamu huo ndio msimamo wa kibinaadamu.
Wazanzibari wameshafanya uamuzi wao. Wameshasema mwanasiasa gani wanamtaka awe kiongozi wao mpya. Ni nani tena anayetaka kubadilisha uamuzi wao huu...? ikiwa si ujahili unao wasumbuwa ukichanganyika na Udikteta wa kiaina Ndio kadhia inayoendelea kuitafuna nchi ya Zanzibar, nchi muhimu sana Afrika Mashariki, Afrika nzima, kidunia na ambayo ni sehemu muhimu pia ya Jamhuri ya Muungano feki wa ((Tanzania.)) Nchi inayosifika kwa watu wakarimu, wastaarabu, watulivu, watendakazi stadi, na wapenda dini sana.Hili halina shida hata kidogo. Wagombea walioshiriki uchaguzi wa nchini Zanzibar wanalijua vizuri. Wanajua uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu, na waangalizi na Tume ya uchaguzi ya nchi ya Zanzibar yenyewe, waliridhika na kiwango cha usimamizi wakisema kimeimarika kutoka ilivyokuwa mwaka 2010.Ukizungumza na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wenye akili nzuri na wanaojali zaidi nchi kuliko maslahi ya chama chao, wanakuambia wazi, “uchaguzi umefanyika na Wazanzibari wameamua wanachokitaka.”Bali unapowauliza sasa kama hata nanyi mnaamini hivi, mnawaeleza viongozi wenu wakubwa kwamba watambue na kukubali uamuzi wa wananchi na kuondoa kikwazo cha kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo...? Wanasema “ah unajua kila mtu anafikiri kwa akili yake, wengine tunamjua Mola aliyetuumba na ndiye tunayemuabudu, wengine wana mambo yao.”Swadakta. Kumbe ni kweli kama ninavyokuwa naamini katika viongozi wakubwa wa CCM, hiki chama kinachogomea matokeo ya kushindwa uchaguzi kwa kubeza uamuzi wa Wazanzibari, wamesahau wameumbwa na Mola huyu Allah.Tunayemuabudu wengi wetu hapa nchini Zanzibar na Tanganyika, siye wanayemuabudu wao. Wana Mungu wao. Useme vipi sasa kama wameshikilia kisichoshikika na kusababisha kuitumbukiza nchi katika mgogoro wa kipuuzi.Viongozi wa CCM wanaendelea kudhani kwamba shida zao binafsi na familia zao, na rafiki zao wakiwemo hawara zao na watoto wao walio zaa nje ya dowa zao, zitatatuka tu kwa kuendelea kuitawala nchi ya Zanzibar kwa lazima japo kuwa wananchi washamuwa kuwa hawawataki tena.
Wameifanya siasa mtaji wa maisha yao. Wanazeekea humo, wengine wakishindwa hata kuwekeza miradi kwa maisha ya nje ya siasa. Au wamewekeza ila walafi wa kutupwa, kwao nje ya utawala; ni mauti na madhila.Angalia, wakati wanajadiliana na wale wanaowakaba wasiongoze nchi ya Zanzibar, tena wakisikitika eti amani ya nchi imewekwa rehani, nje ya hapo, wanaeneza propaganda kuwa “tunajiandaa na uchaguzi mpya.”Lakini angalia vingine. Baada ya kikao cha viongozi wakubwa wa siasa za nchi ya Zanzibar – Shein anayetaka kubakia Ikulu, marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Amani Abeid Karume; Balozi Mkazi na Maalim Seif Shariff Hamad anayepigania haki yake na ya Wazanzibari kwa kura zao walizo piga ili Maalim Seif kuongoza nchi ya Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF) – wameharakia Makunduchi kuwaeleza wasaidizi wao kuwa “mupokee kwamba tumepoteza madaraka.”Watu wa namna hii wanapewa jina linalowastahiki hasa – wanafiki. Adhabu ya unafiki ni mbaya isiyomithilika mbele ya Mola muumba. Shida ni kuwa wa kwao hawa viongozi wahafidhina wa CCM, siye tunayemuabudu sisi.Wanajua hawana hoja. Wanalazimisha tu hoja zilizoshindwa mbele ya wanaadamu. Si kisheria wala kimantiki, hawana hoja.Waliyaeleza malalamiko wanayopigia chapuo nje ya utaratibu, wakaambiwa “mbona hapana hoja hapa.” Wakaishia.Bali wanaendelea kulalamika; tena wanaeneza propaganda nyepesi kwa watu wao wakiwemo vijana walioonekana wenye akili ya kileo, ila wakijijengea historia ya ovyo ya kufikiri pasina kufikiria.Mpaka juzi wanatuma makada walalamike. Wanajua hawana malalamiko yenye maana kwa sheria na taratibu, wanayashika na kuwatuma hao wayashike. Tatizo ni kwamba wanawashikiza kibubusa. Jamani, hawa wenzetu ni shida!!! Wanalalamikia kuibwa kura zao tano, tuseme 25, kisiwani Pemba. Kwani hesabu ya kura inaonesha wamepitwa kwa ngapi...? Ni hizo tano au 25; wakipewa, wameshinda urais...? Watu wa ajabu na hatari hawa CCM wa nchi ya Zanzibar.Kwa sababu maslahi yao ni maslahi ya wenzao wa Tanganyika, na chama chao CCM, basi nao hao bukheri khamsa ishirini (25) wanawasaidia kubeba propaganda nyepesi. Wanasikilikana wakishikilia vitu vya ovyo. Masikini roho zao, zimejaa khiyana (choyo).
Wamemkabasa Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti (kwa kweli si heshima tena kumuita hivyo bora ‘kiongozi’), wakamshikisha maneno ayatamke, alipoyatamka tu, yeye na wao wameitia shimoni nchi ya Zanzibar.Hawaeleweki popote duniani. Hawaeleweki kwao hapa nchini Zanzibar, wanaulizwa kwenye familia zao, wanahojiwa na wanachama wao, wanaoneshwa njia sahihi na Wazungu waliofadhili uchaguzi wote, sasa wanasakamwa na umma na dunia warudishe akili zao za kibinaadamu. Mara ndiwo, mara watupu akilini.Siwatukani kusema hivi. Unawaitaje watu wazima, viongozi wakubwa wa chama kinachojulikana duniani, na wenye dhamana, wanaoshinikiza Maalim Seif akamatwe ashitakiwe eti amevunja sheria kwa kujitangaza mshindi wa urais...?Tuseme katenda hivyo, adhabu yake si CCM kupiga kelele, si Jecha kufuta uchaguzi, si kuwaweka roho juu Wazanzibari na Watanganyika. Hata kidogo. Akamatwe Maalim Seif, bali Tume itangaze kura za mwisho, ijulikane.Akili ya kawaida inatambua kwamba Tume ingemsuta Maalim Seif kwa kuendelea na kazi yake kwa mujibu wa utaratibu. Wakaikamilisha na kutangaza matokeo.Si wangetangaza walichokipata kule mwishoni...? Na wangetangaza Shein amepata, wangekuwa wamemsuta Maalim Seif, si basi. Ni kwanini Tume wakwepe wajibu wao wa kikatiba..? Hivi Jecha amejificha sio...? Ili iwe nini...? Kwa nini hakuna tangazo la serikali kuhusu kilichotokea na kitakachokuja..? Kwanini hapatikani; Mkurugenzi wa Uchaguzi hataki kusema kitu, Shein hataki kusema hadharani. Ni kwanini lakini...? Kama wote hao hawataki kutimiza wajibu wao, maana yake nini..? Ni moja tu – wameshindwa wajibu, na hawaitakii mema nchi ya Zanzibar na Tanganyika. Kwa hivyo, nini adhabu yao...? na shein mwenyewe sio rais tena yopo yopo tu kama kilua kilicho anguka mtini masikini weeeee.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment