Friday, November 20, 2015

MAANDAMANO YA WAZANZIBARI WAISHIO NCHINI UINGEREZA YAFANYIKA NA KUTAKA RAISI ALIYE SHINDA UCHAGUZI NCHINI ZANZIBAR ATANGAZWE





12247082_455166178000825_8745307794412665492_n

Wawakilishi wa Zawa UK wakiingia 10 Downing Street kukabidhi barua kwa Waziri Mkuu Bwana David Cameroon kuhusiana na sakata la Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar. Pichani ni Bwana Rashid Ali, Bi Ghariba Said

8

4

9

5

3

2



6

12227082_10205370980297892_5516912819446149797_n

Nchini Uingereza Wazanzibari wanaoishi nchini Uingereza leo wamefanya maandamano wakidai haki yao na kwa Wazanzibari kwa ujumla ya kutangazwa ushindi wa Chama Cha Wananchi (CUF) katika uchaguzi mkuu nchini Zanzibar uliofanyika Octoba 25 mwaka huu.Maandamano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Zanzibar Welfare Association (ZAWA) ambapo Wazanzibari hao wametoka maeneo mbali mbali katika miji yao na kukusanyika katika eneo Downing Street kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron na uongozi huo kukabidhi barua yao yenye malalamiko kutaka suala la nchi yao ya Zanzibar lishughulikiwe.Maandamano hayo yamefanyika kwa lengo la kuongeza shindikizo kwa mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa ((Tanzania)) au Wakoloni Weusi Tanganyika kuchukua hatua za haraka ya kuhakikisha Tume ya Uchaguzi ya nchini Zanzibar (ZEC) inakamilisha kazi ya kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.Uchaguzi wa nchi ya Zanzibar umekwamishwa na uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Zanzibar, Jecha Salum Jecha Octoba 28 alipotangaza kufuta uchaguzi huo wote kwa madai kwamba umekumbwa na matatizo mbali mbali sote tunajuwa ni ukereketwa na kunywa maji ya bendera ya CCM ndio kulimfanya achukuwe uamuzi huo ulio kinyume cha Sheria za nchi ya Zanzibar na katiba ya nchi ya Zanzibar.
Uamuzi huo wa kufuta matokeo umepigwa na Chama Cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) kwa kuwa hauna ugumu,uwezo kisheria ambapo Mwenyekiti wa tume hiyo hana mamlaka ya kufuta uchaguzi ambao tayari ulishakamilika na matokeo yake kuanza kutangazwa.Wakati jecha akitoa tangazo la kufuta matokeo bila ya kushauriana na tume yake alikuwa tayari ameshatangaza matokeo ya kura za urais za majimbo 31 kati ya 54 ya Zanzibar pia washindi wa nafasi za uwakilishi na udiwani katika majimbo hayo walishatangazwa na walishakabidhiwa vyeti vyao.Barua hiyo iliyowasilishwa na Rashid Ali ambaye kiongozi wa ZAWA wamewasilisha barua hiyo wakiamini kwamba suala la nchi ya Zanzibar litashughulikiwa ili wananchi wa Zanzibar waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida.Mwakilishi wa ZAWA, Hassan Khamis alisema wameamua kupeleka barua kwenye ofisi za waziri Mkuu wakiamini suala hilo litashughulikiwa ikiwa pamoja na serikali ya ((Tanzania)) Wakoloni Weusi Tanganyika kuchukua hatua madhubuti na za haraka katika kushughulikia suala hilo ambalo limewaweka wazanzibari roho juu.“Sisi kama Wazanzibari tumeshachoka na nduguzetu nyumbani ndio kabisa wamechoka na hali iliyopo sasa huko nyumbani kwetu ambao kuna jamaa zetu na wazee wetu wanahitaji kuendelea na maisha yao hivyo kuna kila sababu ya kumalizwa mgogoro uliopo ili waendeleaa na maisha yao sasa hivi maisha yamekuwa magumu, vitu havinunuliki khofu imetanda majeshi yamejaa na hali ya khofu ndio imekuwa kubwa kwa wananchi hawajui saa ngapi kutazuka nini” alisema Khamis.
Wakizungumza kwa njia ya simu baadhi ya wanawake walioshiriki maandamano hayo wamesema wanaiombea dua nchi yao ya Zanzibar ili mgogoro na mkwamo wa kisiasa umalizike ili wananchi waweze kuishi kwa amani kwani suala la kuishi kwa khofu linawatia huzuni hasa wao ambao wapo nje ya nchi.“Tunaumia tukisikia ndugu zetu wa Zanzibar wana mgogoro mwengine uliotokana na uchaguzi kwa sababu ni miaka mingi kulikuwa na hali kama hiyo miaka mitano nyuma kukatafutwa Maridhiano lakini sasa tunarejea nyuma miaka 15 iliyopita, haipendezi na pia inatutia sisi wasiwasi ambao tupo mbali na ndugu zetu” alisema mmoja wa wanawake walioandamana.Khamis alisema wamekabidhi barua na imepokewa ambapo wameahidiwa kwamba barua yao itafanyiwa kazi pamoja na kuonana na baadhi ya viongozi wengine wa serikali ili kupeleka malalamiko yao yafanyiwe kazi haraka.Wazanzibari hao waliovalia nguo rangi nyekundu na buluu na nyeupe huku wengine wakiwa wamebeba mabango yenye maandishi mbali mbali na picha za Mgombea Urais wa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad wameonekana wakiwa na furaha wakati wa maandamano hayo.Hii ni mara ya kwanza tokea kumalizika kwa uchaguzi wa nchi ya Zanzibar kufanyika kwa maandamano kama hayo nchini Uingereza ambapo baadhi ya wananchi wanaoishi Marekani nao wameandaa maandamano yao ambayo yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo.“ tutafanya maandamano kuitaka Serikali ya Marekani kuingilia kati na kuweka shindikizo kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa ((Tanzania)) ili mshindi aliyeshinda atangazwe na serikali ya umoja wa kitaifa iundwe wazanzibari washirikiane wajenge nchi yao” alisema mmoja wa wazanzibari anayeishi Marekani.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment