Saturday, November 14, 2015

MASULTANI WEUSI TANGANYIKA NDIO TATIZO KUU LA NCHI YA ZANZIBAR KUWA TETE


Leo hii nichukue nafasi hii kuwaeleza Watanganyika na Wazanzibari popote pale walipo kwamba nchini Zanzibar hakuna tatizo la uchaguzi bali kinachoendelea nchini Zanzibar ni viongozi wa Tanganyika Masultani Weusi kuendelea kuitawala nchi ya Zanzibar kimabavu huku wakijua fika kwamba ulimwengu huu hilo limeshapitiwa na wakati. Pia ningependa Watanganyika na wasio Watanganyika kuelewa kwamba Watanganyika yaani Wananchi wa kawaida hawana tatizo na Wazanzibari na hawapendi kuona Wazanzibari wanateseka kwa ajili ya kuhalalisha Maslahi ya watu wachache kisiasa kuendelea kutawala kimabavu katika nchi ya Zanzibar. Siku zote huwezi kuficha ukweli, Takribani viongozi wote wa Serikali ya C.C.M ambayo inatawala katika nchi hizi zetu yani Tanganyika wamejengeka na chuki zidi ya Wananchi wa Wazanzibar tofauti na Wazanzibar walio wengi wanao wachukulia Watanganyika kama ndugu zetu wa damu. Nianze kwa mifano hai, Muasisi wa Muungano huu feki Mwalim Nyerere yeye binafsi alikuwa akichukia uwepo wa nchi ya Zanzibar, matamshi yake na hotuba zake zipo na hili halijifichi.Pia waliomfuata akina Mzee Ali Hassan walifuata nyayo hizo hizo hadi hii leo unawaona viongozi wa Watanganyika akina Mkapa na wenzake wanavyoishupalia na kuididimiza nchi ya Zanzibar hili lipo wazi kila mtu anajua. Ukiangalia kauli na maelezo ya Viongozi wa C.C.M nchini Tanganyika kwa mtu yeyote mwenye akili yake timamu na anaependa kutaka kujua ukweli halisi atakubaliana na mimi kwamba tumefika hapa tulipo kutokana na wenzetu kutokuwa na nia njema kwenye Muungano huu feki.Tujikumbushe hotuba ya Waziri Lukuvi alioitoa kwenye waumini wa kanisa nchini Tanganyika,hotuba ile inaonesha ni jinsi gani Wakuu wa nchi ya Tanganyika wanavyoichukulia nchi ya Zanzibar kama wao ndio wamiliki wa nchi hii ya Zanzibar, na Wazanzibari wenyewe hawana haki. Baada ya hotuba ile hakuna hata kiongozi mmoja alietoa maelezo kupinga zana ile ya kibaguzi na ya kishenzi wote wameufyata.
Nchi zote duniani zinaongozwa kwa mujibu wa sheria na taratibu ambazo Watu wenyewe wamejipangia na kukubaliana.Sasa unapokuja hapa nchini Tanganyika na nchi ya Zanzibar unakuta mambo ni tofauti kabisa, sheria ni kwa yale mambo ambayo watawala wanayafurahia tu,hapa utakuta sheria yeyote ambayo inawatukuza na kuutukuza utawala wao hizo ndio zifuatwe lakini zile nyengine zinazowapa Wanyonge haki yao hizo hazina maana, hivi tujiulize nchi ya Tanzania na nchi ya Zanzibar zinaelekea wapi....?? Hivi kweli Wazanzibari hawana haki ya kujitawala wenyewe....?? Hivi nchi ya Tanganyika kujifanya ndie baba katika Nyumba ya nchi ya Zanzibar ni halali huku sote tukiwa Wanaume....?? Tumeshuhudia maamuzi yote muhimu tokea chama kimoja yanafanywa na viongozi wa nchi ya Tanganyika tulifikiria baada ya ukiritimba wa chama kimoja kumalizika, hivi sasa kutakuwa na mabadiliko kwa vile mifumo ya kiongozi na utawala imebadilika lakini la kusikitisha na kuhuzunisha ni kwamba tunashudia aibu na fedheha kwa Taifa hili.Iitakavyokuwa vyovyote Viongozi Watanganyike waelewe kwamba Wazanzibari hawataweza kukubali kuwa nchi yao ya Zanzibar kuwa Mkoa,wilaya au kata moja katika nchi yao ya Tanganyika hilo wasahau mpaka tone la mwisho la damu ya Mzanzibar halisi.Haya yote yanayotokea hapa nchini Zanzibar sio bahati mbaya ni matukio ambayo yamepikwa na kuratibiwa na Serikali ya Tanganyika na kushuhulikiwa vyema na vibaraka wao waliopo hapa nchini Zanzibar kina Mr na Mrs BT. Hivi niwaulize umma lakini sitaki jibu, jiulize wewe binafsi hivi maelezo haya nitakayo yaeleza hapo chini yatakupa picha gani kama kweli wewe ni mpenda haki!!!! Naamini jibu utalipata mwenyewe kwani maelezo haya hayataki usomi bali yanataka mtu muelewa tu.Chama cha Mapinduzi kiko madarakani kwa muda mwingi sasa,Serikali zote zinazoongoza Tanganyika na Zanzibar ni zao.Tume imeundwa na Rais wa C.C.M na Mwenyekiti wake ni mkereketwa wa C.C.M, ukiwacha wajumbe wa wawili kutoka C.U.F wote ni C.C.M , Maofisa wote walioshuhulikia uchaguzi ukiwacha mawakala wa vyama vya siasa vengine ni C.C.M.Sasa tujiulize C.C.M wameibiwa kura vipi mpaka matokeo halali ya uchaguzi yafutwe......?? Ni dhahiri kwamba C.C.M imeshindwa hapa nchini Zanzibar hili halitaki tochi kuangaza. Kinachofanywa na C.C.M ni usanii tena sio wa siasa bali ule wa Bongo fleva maana usanii wa kisiasa una taratibu zake na huzingatia matakwa ya sheria.Tumeshuhudia Baadhi ya Wazanzibari walio wengi wakikoseshwa kuandikishwa na kunyimwa haki yao ya msingi,tumeshuhudia watoto wadogo na baadhi ya watu ambao sio Wazanzibari wakiandikishwa kupiga kura hapa nchini Zanzibar,Masheha,wakuu wa Wilaya/Mikoa wote wa chama Tawala wakiisadia kuiweka tena Serikali madarakani lakini pia la ajabu Jeshi la Taifa pamoja na Polisi pia wametumika kuisaidia C.C.M Lakini imeshindwa na nguvu ya Wananchi .Sasa ikiwa demokrasia ya kweli inapuuzwa kwa maslahi ya kikundi fulani cha watu hili halitowezekana lazima tuwe wakweli hapa kitakachofuata ni machafuko kwenye Nchi, huu ndio ukweli wenyewe,Watanganyika na Wazanzibari munaelekea wapi...??
Uchaguzi wa nchi ya Zanzibar umepata baraka zote za kuingizwa katika matukio ya dunia ya maajabu, kwani mwenye akili timamu haya yanayotendeka hapa nchini Zanzibar kwa amri ya Viongozi wa Masultani Weusi wa Tanganyika katika Nchi zenye ustaarabu uliotukuka hayawezi kufanyika. Hakuna mantiki yeyote wala sheria inayompa uwezo Mwenyekiti wa Tume ZEC kufuta matokeo ya uchaguzi wa nchi ya Zanzibar tena kwa kujificha.Hivi alishindwa vipi kutoa tamko lile mbele ya kadamnasi ya watu kama kweli alikuwa na nia njema....?? ukweli utabakia pale pale kwamba C.C.M ndie mchawi wa Wazanzibari. Mwenyekiti alifanya yale alioyafanya baada ya kupata Baraka zote kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano feki wa Tanganyika Kikwete na Serekali yake.Ushahidi wa hayo ni kwamba Kikwete ndio Amir Mkuu wa jeshi, kabla ya Mwenyekiti kutoa Tangazo la kufuta uchaguzi Jeshi lilimwagwa na vifaru nchini Zanzibar kuonesha dhahiri kwamba Serikali ya Wakoloni Weusi Tanganyika ndio iko nyuma ya pazia.Haiwezekani kufanyika uchaguzi na kuona vifaru na mitutu ya bunduki kwenye mistari na vituo vya kupigia kura huku ofisi zatume zikilindwa kama vile kumetangazwa hali ya hatari nchini .Hivi ZEC ni mbumbumbu kiasi gani kushindwa siku kuhesabu kura laki tano...?? MAAJABU ZEC ZANZIBAR!!! Haya yote yanatokea kwa sababu ya utashi wa Viongozi wa Mkoloni Mweusi Tanganyika hawapendi kuona Wazanzibari wakijiongoza wenyewe. Sababu ambazo mwenyekiti wa ZEC amezitoa yeye peke yake ni za kijinga na kipumbavu ambazo kwa jamii yenye Wasomi kauli hizi haziwezi kusikilizwa hata dakika moja wachilia mbali kuzifuata na kuzitekeleza. Zimekosa mvuto,hata mtoto mdogo hawezi kuamini ujinga kama ule. Nimefuatilia chaguzi zetu tokea mfumo wa vyama vingi kuanza C.C.M haijawahi kushinda jimbo lolote Kisiwani PEMBA tokea uchaguzi wa mwanzo 1995,sasa iweje leo hii waje na tamko eti wameibiwa kura hivi ni vichekesho la kushangaza ni kuona baadhi ya viongozi wakubwa na Wasomi wanaamini upumbavu huu na kuwataka baadhi ya watu kukubali utumbo wa aina hiyo, hili halitowezekana kama munavichwa vya samaki ni nyinyi sio wananchi wa Zanzibar .
Niwatahadharishe tu viongozi wa nchi ya Tanganyika akina Sita Lukuvi,Malecele na wengineo ambao ni wengi wenye mawazo chanya kama hayo kwamba kwa hapa Wazanzibari walipofikia hilo hawatolikubali na mjitayarishe kwa mapambano kwani sasa inaonekana dhahiri kwamba kunahitajika njia mbadala baada ya kushindwa kwa njia hizi za demokrasia.Uvumilivu una mwisho wake,unapofika pahala ukaona kwamba utu wako hauthaminiwi na kupuuzwa lazima utafute njia nyenginezo lakini sio kukubali kudhalilishwa. Kulikuwa na haja gani ya kuleta mfumo wa demokrasia wa vyama vingi na huku munaelewa kwamba nyinyi hampo tayari kiushindani.....?? Munafurahia kwa haya yanayotokea hapa nchini Zanzibar kwa utashi wenu lakini ni vyema mukaelewa kwamba mwisho wa siku haya yote yatakuja kwa Wananchi wa Tanganyika vile vile.Ikiwa munaona utawala wa mabavu na magoli ya mkono ni vyema kwenu, basi umma utafika usiku watayapinga hayo na huo utawala wenu wa kiimla utamaliza.Watanganyika na Wazanzibari wanahitaji yalio bora sio chuki na ubaguzi na uongozi usio kikomo. Maendeleo hayawezi kuja kwa kupindisha haki ya mmoja na kumpa asiestahiki.Mwisho sina budi kuwataka wale wote wapenda amani na demokrasia ya kweli kuwaunga mkono ndugu zao wa Kizanzibari ili na wao waweze kutumia utu wao kumchagua kiongozi wanaemtaka na kuondokana na Mkoloni wa mtu Mweusi Tanganyika mwenzao baada ya ule wa mtu Mweupe uliopita.Alieshinda uchaguzi apewe haki yake.Dhulma haiwezi kuleta amani wala maendeleo mwisho wa siku sote tutakuwa waathirika.
HAKI ITAPATIKANA ZANZIBAR

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment