Wednesday, November 25, 2015

RAISI WA KENYA UHURU KENYATTA AMEWATIMUWA MAWAZIRI WOTE WENYE KASHFA ZA UFISADI JE MAGUFULI UTAWATIMUWA WENYE KASHFA ZA ESCROW,EPA,RICHMOND NA OPERATION TOKOMEZA NA KUWAPELEKA MAHAKAMANI....???


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na kuwapiga chini mawaziri wote ambao wizara zao zinakumbwa na kashfa za ufisadi. Uamuzi wa Rais Kenyatta umekuja siku moja baada ya kutangaza ufisadi kama tishio la usalama wa kitaifa huku akiazimia kufanya mabadiliko makubwa kwenye ofisi ya Rais hivi karibuni.Katika mabadiliko hayo, Kenyatta ameongeza pia idadi ya wizara kutoka 16 hadi 20 na kuongeza idara mpya chini ya wizara hiyo, kutoka idara 26 hadi 41 kwa kile alichoeleza kuwa ni kusaidia wizara kutekeleza majukumu yao bora zaidi.

Baadhi ya mawaziri walikuwa tayari wamekwisha jiondoa kwenye wizara zao kwa tuhuma za ufisadi huku wengine wakiwa na kesi za kujibu mahakamani.Hivi karibuni, Waziri wa Ugatuzi, Anne Waiguru alikuwa wa mwisho kujiondoa kwenye wizara akiwa na kashfa zilizopata umaarufu zaidi kwa kipindi cha hivi karibuni za kununua kalamu moja kwa shilingi zaidi ya 200,000 za nchini Tanganyika.Hata hivyo, Uhuru Kenyatta hakuwa na budi ya kuvunja baraza lake na kuunda upya kwa kuwa katiba ya nchi hiyo inataka idadi ya mawaziri isiwe chini ya 14. Baada ya Waiguru kujiuzulu nafasi ya uwaziri, baraza la mawaziri lilibaki na mawaziri 13 pekee.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment