Thursday, December 31, 2015

ALIPANGALO M.MUNGU KATU BINADAMU HATAWEZA KULIBADILISHA

Mgogoro+Zanzibar+Photo

Katika hali isiyo ya kawaida kuanzia leo ,wakati wowote Maalim Seif Shariff Hamad kutangazwa RASMI aka official kuwa mshindi wa Uchaguzi uliofanyika tarehe 25/10/2015 katika ngazi ya uraisi.
Kikao kilichomalizika cha CCM ambacho kimewapasha wahafidhina wa chama hicho kuyapokea matokeo yatakayotangazwa rasmi na Wakuu wa nchi ambao wamekuwa wakikutana chini ya aliekuwa Raisi wa nchi ya Zanzibar wa awamu iliyopita.
Habari zilizovuja ni kuwa hakuna hali isipokuwa matokeo ya Uchaguzi yaendelee kutangazwa na mshindi au chama kilichoshinda kipewe ushindi wake,zaidi ilikuwa haitajwi kuwa Maalim Seif Shariff Hamad kashinda bali chama kilichoshinda.
Katika mazungumzo hayo UZANZIBARI KWANZA ndio ulioongoza majadiliano hayo na zaidi ilipoonekana CCM wa nchi ya Tanganyika wamekaa kimya ,na kila wanaemsikia ambae ni kutoka CCM ya Tanganyika anasema Wazanzibari watayamaliza wenyewe chachu ambayo imeonekana kuwatenga CCM wahafidhina Mr na Mrs wenye maradhi ya BT wa nchini Zanzibar na kama kitanuka CCM wa nchini Zanzibar ndio watakao husishwa wakati wenzao wa nchi ya Tanganyika wakijitenga na kuwaruka na kuendelea kuja nchi yao kwa furaha kabisa na rais wao ambaye ameleta matumaini makubwa kwa wananchi wanyonge kujione kuwa mara hii wamepata rais mwenye kuleta maendeleo kwa wote,habari za kuondoka wanajeshi wenye sare za Tanganyika walio jazwa hapa nchi Zanzibar na Kikwete ,kumezidi kuonyesha dalili za kuwa CCM na nchi ya Tanganyika kujitenga kwa lolote,na kuonekana wataegemea kauli wanayoitumia kila kona ya Dunia kuwa WaZanzibari watayamaliza wenyewe nchini kwao.
Katika CCM walioshiriki kikao hicho hata wale waliokuwa wakisema sana na kuulinda uamuzi wa Jecha wamekataa kubebeshwa lawama iwapo wananchi watapambana na kutokea maafa ,wa kwanza kuruka kiunzi hicho ni mkuu wa kikao ambae alisema hayupo tayari kuwa mhusika wa machafuko,hayo walipeana vidonge baada ya kukutana chemba wahusika watupu wanaoonekana ni kutoka CCM wakishauriana ili kuwa na uamuzi wa pamoja.Hali iliyosababisha wengine kupwaya na kubaki na hoja zisizo na mashiko.
Kwa ufupi mambo mazuri yameshaiva.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment