Thursday, December 3, 2015

ISMAIL JUSSA LADHU NIWASAIDIE WAZANZIBARI WENZANGU


Ismail Jussa
Baada ya kupata maswali mengi, leo nimeona kidogo niwasaidie ndugu zangu mnaouliza ni kwa nini uongozi wa CUF umekuwa kimya kuhusu mazungumzo yanayoendelea kati ya Maalim Seif Sharif Hamad na Dk. Ali Mohamed Shein ambayo pia yanawahusisha Dk. Amani Karume, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Balozi Seif Ali Iddi. Mazungumzo hayo yalianza Novemba 9 na mpaka sasa imeshafanyika mikutano mitano. Wengi wetu tunakosa uelewa wa mambo kama haya na tunadhani kwamba ni swali la mmoja kwenda kumueleza mwengine mtazamo wake na kisha kukubaliana. Ndiyo maana tunaona mikutano mitano ni mingi sana.Tunahoji kinajadiliwa nini kisichokwisha..??. Lakini wale wanaofuatilia mambo kama haya wanafahamu kwamba si mepesi kama yanavyofikiriwa. Mfano mzuri turejee mazungumzo kama haya nchini Kenya baada ya uchaguzi wa 2007. Wengine wanasema kwa nini Chama kisiwe kinatoa taarifa baada ya kila hatua ya mazungumzo. Lakini kwa wanaoelewa na kufuatilia mazungumzo kama haya pia wanajua kuwa taarifa za upande mmoja si utaratibu sahihi wa kutoa taarifa ya kinachoendelea, kwani huishia kuvuruga mazungumzo.
Tunapaswa tujue kwamba mazungumzo kama haya ambayo yanahusu madaraka (power) huwa yanafuatiliwa pembeni na makundi mengi yenye maslahi tofauti. Huwa yana dynamics zake na kuna watu wengi pembeni wenye maslahi yao ambao huwa na tamaa ya kupata au khofu ya kupoteza maslahi fulani kutokana na yale yatakayoamuliwa. Katika hali hiyo, ikiwa kila jambo litasemwa hapatakuwa na litakalokuwa. Wengine wanasema mbona viongozi wa CCM wanawapitia viongozi na wanachama wao kuwaelezea kwamba uchaguzi utarudiwa na kwamba wajiandae kwa uchaguzi huo. Kwa hili niwarudishe kwenye taarifa ya Balozi Seif Ali Iddi ya kujirudi na kukanusha kwamba hakuna makubaliano yaliyofikiwa kwamba uchaguzi urudiwe. Kwa hivyo, wacha viongozi wa CCM wapite na waseme wanayosema. Wanafanya hivyo kuwapa matumaini wafuasi wao.
Kama uamuzi ni huo, Balozi Seif Ali Iddi asingekanusha kauli yake mwenyewe. Lakini zaidi jiulizeni walitangaza kila mahala kwamba uchaguzi wao wa marudio utafanyika tarehe 13 Desemba, 2015. Zikiwa zimebakia siku 10 kufikia tarehe hiyo, kuna dalili ya uchaguzi hapa....?? Mwisho kabisa, nimalizie kwa kuwahakikishia Wazanzibari kwamba kiongozi wao mpendwa ambaye walimpa kura nyingi tarehe 25 Oktoba, 2015 Maalim Seif Sharif Hamad anajua anachokifanya na anajua thamani ya ushindi waliompa Wazanzibari. Hatetereki katika msimamo wake ambao ndiyo msimamo wa Jumuiya ya Kimataifa na wapenda haki na amani wote kwamba ufumbuzi wa haki na wa kikatiba na kisheria ni kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kukamilisha kazi ya kutangaza matokeo ya majimbo 23 yaliyobakia kati ya 54 na kumtangaza mshindi wa Urais wa Zanzibar. Baada ya hapo ifuate hatua ya kumuapisha Rais Mpya wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na kisha vyama vya CUF na CCM vishirikiane kuunda Serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa itakayoiongoza Zanzibar kwa miaka mitano ijayo (2015 – 2020).

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment