Thursday, December 3, 2015

KITUO CHA RADIO HITS FM NCHINI ZANZIBAR CHATIWA MOTO

UPO MKUU WA UPELELEZI NCHINI ZANZIBAR KITUO CHA RADIO HITS FM KISHATIWA MOTO MAKUNDI KAMA HAYA NCHI TANGANYIKA YAKIFANYA UHUNI WAO SIKU HIYO HIYO HUKAMATWA NA JINCHI KUBWA KAMA NINI HAPA VISIWANI WANAFANYA WATAKAVYO KISHA POLISI INADANGANYA WATU TUNAENDELEA NA UPELELEZI KISHA KIMYA SIMUSEME UKWELI TU KUWA NI WATOTO WENU WANAENDELEZA UHARAMIA NA USHENZI KESI NGAPI SASA MLIZO FANIKIWA KATIKA UPELELEZI WENU NA WANGAPI MUMEWAFIKISHA POLISI AU MAHAKAMANI.....??Kundi la Watu wanaojulikana na jeshi la polisi na hata wazanzibari pia wanawajuwa wanapoishi na njia wanazo pita ila wazanzibari na jeshi la polisi hawajamuuwa kuwashughulikia kwa sababu moja au nyengine hili kundi linapewa amri na mkuu katika wakuu wa serekali hapa nchini Zanzibar kuendesha uharamia wao na polisi kufurahia na kujitia hamnazo kama hawawajuwi wakati ni wao wao wakiwa na silaha wamevamia studio za kituo cha  redio Hits FM kilichopo Migombani mjini Unguja na kufanikiwa  kukichoma moto kwa kutumia mafuta yanayosadikiwa kuwa ni petroli. Akizungumza na Muandishi wetu msemaji wa kituo hicho Juma Ayoub Amohamed, alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 7:30, usiku wa kuamkia jana ambapo zaidi ya watu 15 waliweza kuvamia studio hiyo na kufanikiwa kuichoma moto. Alisema kuwa hadi sasa bado hawajajua nini chanzo cha kufanyiwa hivyo huku wakisema kuwa hakuna siku hata moja waliyopewa onyo na mtu, kundi au taasisi yeyote juu ya uendeshaji vipindi vyao.
“kiukweli hadi sasa tunashangaa hili kundi lilitokea wapi na nini chanzo chake ila kazi kubwa tumewachia Jeshi la Polisi ambao wanaendelea na uchunguzi wao wa kisheria”alisema Juma. Hata hivyo alisema kuwa makadirio ya awali juu ya tukio hilo ni zaidi ya shilingi milioni 40, ambapo hesabu rasm itajulikana baada ya kufanyika kwa uhakiki. Akisimulia mkasa wa tukio hilo Ali Abdallah mfanyakazi wa zamu ambaye alikuwamo kituoni hapo wakati wa tukio hilo alisema kuwa alikuwa anaendelea na uendeshaji wa vipindi mara akasikia sauti za watu wakiwa ndani ya studio hiyo. Alisema kuwa watu hao ambao walikuwa zaidi ya 15 wakiwa wamejifunika uso na kumuamuru anyanyuke na kutoka nje ili wafanye wanachokitaka. Alisema kuwa mara baada ya taarifa yao hiyo mfanyakazi huyo alisita kidogo, na mmoja wao akamsogelea na kuanza kumpiga kwa mabapa ya panga na kumyanyua na kumfunga kitambaa cha uso na kumtoa nje kijeshi. “Waliponambia nitoke nje nilisita kidogo nao walinichukua kwa kamandi na kunipiga mabapa ya mapanga mwilini na kunifunga kitamba cha uso na kunitoa nje huku wakisema tunataka kufanya jambo humu ndani” alisema Abdallah. Hata hivyo alisema kuwa kutolewa kwake nje hakukuwa dawa kwa studio hiyo kwani mara baada ya muda mfupi walishuhudia moshi mkubwa ukiteketeza vifaa vyao vya studio.
Alisema kuwa huku moto huo ukiteketeza vifaa hivyo kundi hilo la watu liliweza kutoka nje na kuanza kuondoka, huku yeye na walinzi wa zamu wa studio wakiwa wamewekewa chini ya ulinzi na baadhi ya vijana wa kundi hilo .“Walipoondoka tu mimi na askari wetu tulijitahidi sana kutafuta watu wakutusaidi tulienda hadi katika nyumba ya Rais mstaafu Aboud Jumbe tukawaelezea wale askari waliokuwapo pale jinsi ya tukio letu nao walipiga simu kituoni kwao baada ya muda mfupi kikosi cha askari kikaja ila hawakufanikiwa kukuta hao wachomaji walikuwa wameshaondoka na gari lao”alisema Ali Ismail Mwinyi ambaye ni mwandishi wa habari kituo hapo alisema kuwa kwa upande wake alipopata habari hio aliweza kufika kituo kwao hapo na kushuhudia jinsi ya studio hio inavyoteketea kwa moto.Alisema kuwa tukio kwa ukweli limewasikitisha sana kutokana na hasa kosa lao kubwa la kufanyiwa hivyo hadi sasa bado hawalitambui huku akisisitiza kuwa kituo chao kinaendesha vipindi kwa kufuata taratibu za kisheria. Hili ni tukio la pili katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo miezi michache iliyopita watu kama hao waliokuwa na silaha walivamia kituo cha Coconut Fm na kuwatisha watangazaji watu hao hao ndio walikuwa wakiwatisha watu na kuwapiga wakati wa uwandikishwaji wa kupiga kura n.k je yule mkuu wa upelelezi anaye jidai kupeleleza makamishna wa uchaguzi na kutaka kuwabambikia kesi ili wawafunge jela kwa kushindwa chama cha CCM yuko wapi na upelelezi wake.....???

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment