Wednesday, December 9, 2015

MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD WEWE KWELI NI NAHODHA UNAE JUWA KUKIFIKISHA CHOMBO BANDARINI SALAMA


Na, b.ole
Sina budi kuchukua nafasi hii adhimu kuwapongezeni Wazanzibar wote wa Unguja na Pemba kutokana na kile kitendo chenu mulichokifanya tarehe 25 oct,2015 ambacho kilionesha kwa vitendo maamuzi ya walio wengi lakini pia kama hilo halitoshi ustahamilivu wenu pia umechupa mipaka na madaraja,sina budi kuwapongezeni kwa hilo.Ulimwengu umewafahamu kwamba Wazanzibar ni waungwana wa kupigiwa mfano katika ulimwengu huu wa mikasa na karaha.Kweli Maalim Seif ni Nahodha sio Bwege mara hii.
Pili nimpongeze kwa dhati sana Mh. Maalim Seif kwa ujasiri wake pamoja na kubobea kama Mwanasiasa na Mwanadiplomasia mahiri asiyeyumba.Wazanzibar wanabahati kupata kiongozi anaejiamini, mwenye kupenda raia wake na mwenye muono wa kuleta maendeleo katika Visiwa vya Zanzibar.Wazanzibar hawana budi kujivunia kwa hilo,sio uchochezi wala aibu leo hii kumuona Mzanzibar halisi anajivunia na kujinasibisha na kiongozi huyu.Naamini kuna wengi ambao sio Wazanzibar lakini ari na uchu wa Maendeleo alionao Kiongozi huyu Wanamkubali na kumzimia kutokana na uweledi wake na uchapaji kazi wake.
Ukitaka kumjua Kiongozi mweledi katika uwanja wa siasa basi moja kati ya alama zake ni kuwa mtu wa busara na maarifa na hasa kiongozi mwenyewe akijielewa kwamba wale anaoshindana nao ni hohehahe wasiojielewa. Maguvu na mieleka sio mbegu njema katika kufikia kule kwenye uwanja wa amani,upendo,utulivu na maendeleo ya kweli.Kitendo cha Maalim Seif kupigania haki ya Wazanzibar kwa njia ya amani ni mfano wa kuigwa na sio kwa Zanzibar tu bali hata duniani kote.Naamini kuna jamii zitakuja kujifunza kutoka kwa Kiongozi huyu na pia historia haitakuwa ngeni katika kuenzi jambo hili.
Kila zama hutokea Kiongozi katika jamii ambae kuletwa kwake ni kwa ajili ya kuwakomboa wanyonge wanaokandamizwa na utawala dhalimu na kibabe katika jamii inayohusika.Kwa Wazanzibar Maalim Seif ndio chaguo walilochaguliwa hawana budi kumpenda na kumuenzi kwani Kiongozi huyu ni tunu isio kwisha hamu kwa Wazanzibar.Natamani na mimi ningelikuwa Mzanzibar,naamini ningelijivunia na kijifurahisha sio kwakua ni Mzanzibar tu bali kuwa naongozwa na Kiongozi anaependa haki na usawa kwa wote na anaependeza kwa wengi.
Nimekuwa nikifuatilia siasa za Wazanzibar tokea nikiwa mdogo na kwa bahati mbaya sikufanikiwa kupata Elim kubwa lakini nimepata kujifunza mambo mengi katika jamii hii ya Wazanzibar ambapo kwa leo wametawanyika ulimwengu mzima.Siamini kwamba Wazanzibar wanafurahikia hilo lakini niseme tu kwamba malimwengu ndio yaliowasibu hadi kufikia katika hali hiyo.Zaidi nilichojifunza kwa Wazanzibar ambalo wao wenyewe hawalijui kwamba ndio liliwaponza hadi kufikia hatua hii waliyonayo ni UKARIMU wao na UPENDO usiomithilika.
Vitu hivi viwili ndio vilivyo wasababishia Wazanzibar kufikia hapa walipo. Tatizo lao kubwa ambalo Mababu na Mabibi zao waliyafanya ni kuwakaribisha Majirani zao kutokana na ukarimu na upendo wa jadi waliobarikiwa matokeo yake Majirani wale wakawageuka Wenyeji wao na kujifanya wao ndio wenye hati miliki na mamlaka ya Wazanzibar na hapa ndipo lilipozaliwa lile kundi linalojulikana kama Wahafidhina ambao kwa leo ndio wanao wayumbisha Wazanzibar halisi. Naomba kwa wale Wazanzibar halisi wafanye utafiti juu ya hili halafu watueleze ukweli juu ya akina nani Zanzibar wamewafikisha hapa walipo Wazanzibar leo hii.Jibu liko wazi kwamba wakuja ndio tatizo la Wazanzibar na hili haliwezi kufichwa katika jamii ya Wazanzibar.
Wakati nikitafakari haya ndio kwanza napata kufumbua macho nakuona mwangaza wa asubuhi na jua likichomoza huku nikiwa taabani ndani ya chombo,siamini macho yangu kuona kwamba Nahodha alietegemewa Maalim Seif amewafikisha Wazanzibar nangani, nahisi kama vile niko ndotoni,siamini ! sina budi kutoa hongera nyingi kwake pamoja na mabaharia wake,ama kweli wewe ni Nahodha, hongera baba Seif kazi yako imekwisha kalafati waachie wengine roho za Wazanzibar zimeshasalimika na kiza kinene cha bahari,kilichobakia baba piga makasia maji sasa ni ya mafuti chaza Wazanzibar watavuwa wenyewe tando umeshawatia.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment