Friday, December 4, 2015

NI BALAA NCHINI TANGANYIKA VIGOGO WA TRA WAKUTWA NA MAMILLIONI NDANI YA NYUMBA ZAO WENGI SASA WALALA HOTELINI AU GEASTI ILI NYUMBA ZAO ZISIJULIKANE


Siku  chache baada ya kigogo mmoja wa Mamlaka ya Mapato Tanganyika (TRA), kubainika kumiliki nyumba 73, wafanyakazi wengine wa mamlaka hiyo wamekutwa na mamilioni ya shilingi waliyoficha majumbani mwao.aibu,balaa na tama baya walio nayo. Taarifa kutoka ndani ya TRA zinapasha kuwa tangu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awasimamishe kazi maofisa kadhaa wa mamlaka hiyo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na kitengo cha uchunguzi cha mamlaka hiyo, hivi sasa wapo kwenye msako wa kubaini ukwasi wa wafanyakazi wake. Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, juzi maofisa wa kitengo cha uchunguzi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, walifika katika eneo la Tegeta Salasala wilayani Kinondoni na kuvamia nyumba mbili za wafanyakazi wa mamlaka hiyo. Katika nyumba hizo, wafanyakazi hao kila mmoja alikutwa na kiasi kikubwa cha fedha ndani kuliko kiwango cha mshahara anaolipwa. majambazi mikubwa inahujumu uchuma tu.

“Walivamiwa wafanyakazi wawili (majina yanahifadhiwa au hapa Zanzibar tunasema majina kapuni),ambapo katika kila nyumba zilikutwa fedha nyingi. Kwa mtu wa kwanza zilikutwa Sh milioni 200 na yule wa jirani yake pia alikuwa na zaidi ya shilingi milioni 150. “Tangu kuanza kwa msako huu wafanyakazi wengi wamekuwa hawana amani kabisa, na hata wengine wanasema wazi kama wangekuwa na uwekezaji wa nje ya nchi wangeondoka kabisa nchini,” 

kilisema chanzo cha gazeti hilo maana washajuwa kuwa sasa rushwa haitafanyika tena na wao mchezo wao au maisha yao ni rushwa game na kunyonya wanyonge.
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wafanyakazi hivi sasa wamelazimika kuzikimbia nyumba zao na kuishia kulala hotelini huku wakienda kazini wakiwa na hofu.Hivi karibuni, vyombo vya habari viliripoti kuwa Kamishna wa Forodha wa TRA, Tiagi Masamaki, aliyesimamishwa kazi pamoja na vigogo wengine wa mamlaka hiyo kutokana na upotevu wa kontena 349 zenye thamani ya Sh bilioni 80, amebainika kumiliki nyumba 73 mtu moja tu huyo atii anamiliki nyumba 73 hebu tumulize kwa mshahara upi na mshahara huo anao lipwa ni kwa dola,euro,pound au shillingi za Tanganyika mpaka akaweza kumiliki nyumba 73......???

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment