Sunday, December 27, 2015

SAFARI ZA KUIDAI NCHI YA ZANZIBAR 1963 LACENSTER.SAFARI ZA KUIDAI NCHI YA ZANZIBAR 2015 KWA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA MASULTANI WEUSI ZIMEANZA












 huzuni kubwa Ni msiba mkuu lakini kila jambo lina mwisho wake na mwisho wa huu ni Wazanzibari wapewe haki yao ya kumchaguwa kiongozi walio mtaka na kumpigia kura ambaye ni Maalim Seif Shariff Hamad sote tunalijiwa hilo hakuna cha mgogoro wa kisiasa wala mkwamo wa kisiasa kilichopo ni kuwa kikundi cha majambazi,walafi,waroho wa madaraka,wabaguzi,wenye xhuki binafsi,wauwaji,mara hii M,Mungu kawaumbuwa na kila walipangalo M,Mungu anazidi kuwaumbuwa na kufedheheka kuwa bado wanataka kuka madarakani hata ikiwa ni kuuwa Wazanzibari wote ila wao lazima wabaki madarakani maskini wamesahau kama haya ni maisha ya kupita tu Mzee karume yuko wapi...? Abdurahamani Babu yuko wapi....? John Okello yuko wapi...? Mzee Thabiti Kombo yuko wapi....? Nyerere yuko wapi...? Hitler yuko wapi...? na wengine wengi sana wako wapi leo hii hata kutajwa hawatajwi tena itakuwa nyinyi.......???

Kabla ya 1963. Wakitoka Karume , Shamte , Ali Muhsin , Hasnu Makame na hata Babu…. Wote kiguu na njia kwenda Lancester UK kudai “Uhuru” wa nchi yetu ya Zanzibar kutoka Uingereza. Muda walipoteza mpaka wakafanikiwa……Zanzibar ikafurahi sasa wapo Huru. Yakaja Mapinduzi na Muungano Feki sasa tanga 64 tunapigishwa safari za Dodoma na Dar kwa Mkoloni Mweusi Tanganyika. Alianza Karume mwenyewe kwenda kuramba miguu Akauliwa wakatuwekea Jumbe. Nae japo ni Gavana lakini ni Muislam na kaoa huku yule akawa anataka kupata maslahi ya wajukuu zake akaambiwa 1+1 = 3. Akawekwa kifungoni Kigamboni tuli mpaka Kazeekeya Kigamboni.

Wakaja kina Seif nao yakawafika ya kuwafika, Salmin naye alijaribu kutikisa kibiriti ..kikamuwakia mwenyewe Akaja Bilal kafanya zogo akaambiwa nyamaza wakampeleka Dodoma mpaka kazeekea huko kimya Akaja Karumu mdogo naye yalomkuta kuzomewa na kuchorwa na wabara wa Kisonge katika ubao wa kisonge na mengine mengi, Walikuja kina shamsi vuai na wengine wakaambiwa hapa tutampa Shein..Amri ya Dodoma kwisha wakaufyata. Sasa haya Juzi tena Seif Kashinda tena kwa kishindo kikubwa amri haijatoka nani apewe kwani Shein imani yake inamsuta kukubali kuijitangaza kakataa sasa Jecha akaambiwa koma kumtangaza Seif …unawajua Dodoma wewe...? Kalikoroga sasa ajificha kila kona laana kwake..

Sasa cha kusikitisha safari zimeanza tena ..lakini hizi si za Lacenster kudai kwa Muingereza hizi za Dodoma na Dar kwa Mkoloni Mweusi Tanganyika kuomba kwa mabwana zetu wapya Makaburu Weusi hawa Tanganyika…Kaanza seif iddi...Akafata seif sharif...Sasa zamu ya shein.
Hii si bure …tuna utandu wa ubongo unazuia kufikiri kama watu huru..tupo muflis….dhambi kuu mara nyingi laana huja kwa wote…na ndo yatupatayo hivi sasa,

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

1 comment:

  1. CCM mutakoma mukilazimisha kurejewa kwa uchaguzi, itakuwa ni historia yenye kukumbukwa kwa muda mrefu. Na wewe mkoloni Tanganyika tosheka na kwako Mungu kawapeni ardhi na raslimali za kutosha kama lazima mutuchukulie nchi yetu ya Zanzibar jitayarisheni na hiyo Tanganyika kukunyanganyeni shwain

    ReplyDelete