Tuesday, December 1, 2015

SHEIKH PONDA ISSA PONDA AMEACHIWA HURU ALHAMDULILAHI

Katibu Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa serikali
Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Morogoro imemwachia huru kiongozi wa taasisi na jumuiya za kiislam nchini sheikh ponda issa ponda baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyofunguliwa mahakamani hapo dhidi yake.Sheikh ponda aliachiwa huru na Hakimu mkazi mfawidhi Mary Moyo baada ya kukaa rumande kwa zaidi ya miaka miwili kutokana na kile kilichoelezwa kuwa dhamana yake ilizuiwa na mkurugenzi wa mashtaka DPP kwa maslahi ya taifa.
Akizungumza mara baada ya kuachiwa huru sheikh Ponda alisema kuwa anaishukuru mahakama kwa kutenda haki japo kuwa imechelewa na kwamba amekaa rumande tangu siku aliyokamatwa kutokana na dhamana yake kuzuiwa.Katika kesi hiyo iliyovuta watu wengi wakiwemo waumini wa dini ya kiislamu sheikh ponda alikabiliwa na mashtaka mawili ambayo atii ni kutoa maneno yenye kuumiza imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa ambayo alidaiwa kuyatenda agosti 10 mwaka 2013 katika viwanja vya shule ya msingi kiwanja cha ndege manispaa ya morogoro.
Upande wa mashtaka katika kesi hiyo uliwakilishwa na wakili wa serikali mwandamizi Bernard Kongola, Sunday Hyera, na George Mbalassa wakati upande wa utetezi uliongozwa na wakili Juma Nasoro, Abubakar Salim na Batheromeo Tarimo.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment