Thursday, December 31, 2015

ALIPANGALO M.MUNGU KATU BINADAMU HATAWEZA KULIBADILISHA

Mgogoro+Zanzibar+Photo

Katika hali isiyo ya kawaida kuanzia leo ,wakati wowote Maalim Seif Shariff Hamad kutangazwa RASMI aka official kuwa mshindi wa Uchaguzi uliofanyika tarehe 25/10/2015 katika ngazi ya uraisi.
Kikao kilichomalizika cha CCM ambacho kimewapasha wahafidhina wa chama hicho kuyapokea matokeo yatakayotangazwa rasmi na Wakuu wa nchi ambao wamekuwa wakikutana chini ya aliekuwa Raisi wa nchi ya Zanzibar wa awamu iliyopita.
Habari zilizovuja ni kuwa hakuna hali isipokuwa matokeo ya Uchaguzi yaendelee kutangazwa na mshindi au chama kilichoshinda kipewe ushindi wake,zaidi ilikuwa haitajwi kuwa Maalim Seif Shariff Hamad kashinda bali chama kilichoshinda.
Katika mazungumzo hayo UZANZIBARI KWANZA ndio ulioongoza majadiliano hayo na zaidi ilipoonekana CCM wa nchi ya Tanganyika wamekaa kimya ,na kila wanaemsikia ambae ni kutoka CCM ya Tanganyika anasema Wazanzibari watayamaliza wenyewe chachu ambayo imeonekana kuwatenga CCM wahafidhina Mr na Mrs wenye maradhi ya BT wa nchini Zanzibar na kama kitanuka CCM wa nchini Zanzibar ndio watakao husishwa wakati wenzao wa nchi ya Tanganyika wakijitenga na kuwaruka na kuendelea kuja nchi yao kwa furaha kabisa na rais wao ambaye ameleta matumaini makubwa kwa wananchi wanyonge kujione kuwa mara hii wamepata rais mwenye kuleta maendeleo kwa wote,habari za kuondoka wanajeshi wenye sare za Tanganyika walio jazwa hapa nchi Zanzibar na Kikwete ,kumezidi kuonyesha dalili za kuwa CCM na nchi ya Tanganyika kujitenga kwa lolote,na kuonekana wataegemea kauli wanayoitumia kila kona ya Dunia kuwa WaZanzibari watayamaliza wenyewe nchini kwao.
Katika CCM walioshiriki kikao hicho hata wale waliokuwa wakisema sana na kuulinda uamuzi wa Jecha wamekataa kubebeshwa lawama iwapo wananchi watapambana na kutokea maafa ,wa kwanza kuruka kiunzi hicho ni mkuu wa kikao ambae alisema hayupo tayari kuwa mhusika wa machafuko,hayo walipeana vidonge baada ya kukutana chemba wahusika watupu wanaoonekana ni kutoka CCM wakishauriana ili kuwa na uamuzi wa pamoja.Hali iliyosababisha wengine kupwaya na kubaki na hoja zisizo na mashiko.
Kwa ufupi mambo mazuri yameshaiva.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Sunday, December 27, 2015

SAFARI ZA KUIDAI NCHI YA ZANZIBAR 1963 LACENSTER.SAFARI ZA KUIDAI NCHI YA ZANZIBAR 2015 KWA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA MASULTANI WEUSI ZIMEANZA

 huzuni kubwa Ni msiba mkuu lakini kila jambo lina mwisho wake na mwisho wa huu ni Wazanzibari wapewe haki yao ya kumchaguwa kiongozi walio mtaka na kumpigia kura ambaye ni Maalim Seif Shariff Hamad sote tunalijiwa hilo hakuna cha mgogoro wa kisiasa wala mkwamo wa kisiasa kilichopo ni kuwa kikundi cha majambazi,walafi,waroho wa madaraka,wabaguzi,wenye xhuki binafsi,wauwaji,mara hii M,Mungu kawaumbuwa na kila walipangalo M,Mungu anazidi kuwaumbuwa na kufedheheka kuwa bado wanataka kuka madarakani hata ikiwa ni kuuwa Wazanzibari wote ila wao lazima wabaki madarakani maskini wamesahau kama haya ni maisha ya kupita tu Mzee karume yuko wapi...? Abdurahamani Babu yuko wapi....? John Okello yuko wapi...? Mzee Thabiti Kombo yuko wapi....? Nyerere yuko wapi...? Hitler yuko wapi...? na wengine wengi sana wako wapi leo hii hata kutajwa hawatajwi tena itakuwa nyinyi.......???

Kabla ya 1963. Wakitoka Karume , Shamte , Ali Muhsin , Hasnu Makame na hata Babu…. Wote kiguu na njia kwenda Lancester UK kudai “Uhuru” wa nchi yetu ya Zanzibar kutoka Uingereza. Muda walipoteza mpaka wakafanikiwa……Zanzibar ikafurahi sasa wapo Huru. Yakaja Mapinduzi na Muungano Feki sasa tanga 64 tunapigishwa safari za Dodoma na Dar kwa Mkoloni Mweusi Tanganyika. Alianza Karume mwenyewe kwenda kuramba miguu Akauliwa wakatuwekea Jumbe. Nae japo ni Gavana lakini ni Muislam na kaoa huku yule akawa anataka kupata maslahi ya wajukuu zake akaambiwa 1+1 = 3. Akawekwa kifungoni Kigamboni tuli mpaka Kazeekeya Kigamboni.

Wakaja kina Seif nao yakawafika ya kuwafika, Salmin naye alijaribu kutikisa kibiriti ..kikamuwakia mwenyewe Akaja Bilal kafanya zogo akaambiwa nyamaza wakampeleka Dodoma mpaka kazeekea huko kimya Akaja Karumu mdogo naye yalomkuta kuzomewa na kuchorwa na wabara wa Kisonge katika ubao wa kisonge na mengine mengi, Walikuja kina shamsi vuai na wengine wakaambiwa hapa tutampa Shein..Amri ya Dodoma kwisha wakaufyata. Sasa haya Juzi tena Seif Kashinda tena kwa kishindo kikubwa amri haijatoka nani apewe kwani Shein imani yake inamsuta kukubali kuijitangaza kakataa sasa Jecha akaambiwa koma kumtangaza Seif …unawajua Dodoma wewe...? Kalikoroga sasa ajificha kila kona laana kwake..

Sasa cha kusikitisha safari zimeanza tena ..lakini hizi si za Lacenster kudai kwa Muingereza hizi za Dodoma na Dar kwa Mkoloni Mweusi Tanganyika kuomba kwa mabwana zetu wapya Makaburu Weusi hawa Tanganyika…Kaanza seif iddi...Akafata seif sharif...Sasa zamu ya shein.
Hii si bure …tuna utandu wa ubongo unazuia kufikiri kama watu huru..tupo muflis….dhambi kuu mara nyingi laana huja kwa wote…na ndo yatupatayo hivi sasa,

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Wednesday, December 23, 2015

PASPOTI YA ZANZIBAR KABLA YA KUPINDULIWA NA KUTAWALIWA NA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA HII HAPA

WAKO WAPI WANAO SEMA ZANZIBAR SIO NCHI WAKO WAPI WANAOSEMA ZANZIBAR HAIJAWAHI KUWA NA PASPOTI.....??
TULIKUWA HIVI DAH SIO MCHEZO
LEO ZANZIBAR TUMEFIKISHWA HAPA NA CCM OYEEEE CCM OYEEE CCM OYEEEE
LEO TUNA HILI LA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Sunday, December 20, 2015

NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI UTALII NA MICHEZO NCHINI ZANZIBAR BIHINDI AIKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO TIMU YA ZANZIBAR BEACH SOKA

Kiongozi wa Timu ya Zanzibar Beach Soka Ali Shariff (Adof) akitowa shukrani kwa Uongozi wa Wizara ya Michezo hapa nchini Zanzibar kwa msaada huo na kuitaka Wizara na Baraza la Michezo hapa nchini Zanzibar kuitilia nguvu Michezo ya Beach Soka Zanzibar ili kuukuza mchezo huo hapa nchini Zanzibar, Timu ya Beach Soka inashiriki Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Nchini Kenya michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika Wiki Hii Nchini Kenya

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii Michezo nchini Zanzibar Mhe Bihindi Hamad akizungumza na Wanamichezo wa Mchezo wa Mpira wa Ufukweni Zanzibar (Beach Soka) wakati wa kuwakabidhi Vifaa vya Michezo kwa Uongozi wa Timu hiyo katika ukumbi wa VIP Amaan nchini Zanzibar. 

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe Bihindi Hamad akimkabidhi Vifaa vya mchezo wa Soka la Ufukweni (Beach Soka ) Kiongozio wa Timu hiyo Ali Shariff (Adof) kwa ajili ya timu yake kuweza kushiriki vizuri katika michuano hiyo ya Afrika Mashariki inayofanyika Nchini Kenya makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa VIP Uwanja wa Amaan nchini Zanzibar.katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini Zanzibar Sharifa Khamis (Shery)

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo nchini Zanzibar Mhe Bihindi Hamad akiendelea kumkabidhi Vifaa vya mchezo wa Soka la Ufukweni (Beach Soka ) Kiongozio wa Timu hiyo Ali Shariff (Adof) kwa ajili ya timu yake kuweza kushiriki vizuri katika michuano hiyo ya Afrika Mashariki inayofanyika Nchini Kenya.

Kiongozi wa Timu ya Zanzibar Beach Soka Ali Shariff Adof akitowa shukrani 

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

CCM MAA MR NA MRS WENYE MARADHI YA BT WAKERWA NA NCHI YA MAREKANI KUZUI MABILLIONI

KABURINI KUNA KASHESHE NA KIYAMA KUNA NI BALAA Mhhha

Wakati Chama cha Mapinduzi kinapinga uamuzi wa Marekani wa kusitisha msaada kwa nchi ya Zanzibar na Tanganyika wa tilioni 1.5 kutokana na kufutwa kwa matokeo ya Uchauzio Mkuu wa  nchi ya Zanzibar lakini kura hizo hizo za wabunge na raisi wa Tanganyika wakazikubali na kumupisha Pombe Magufuli, Chama cha Wananchi CUF kimeunga mkono uamuzi huo na kutaka mshindi wa urais aliye shinda nchini Zanzibar atangazwe na kuapishwa ili kuondoa vikwazo vya kiuchumi. Msimamo huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama cha Wananchi (CUF),  Ismail Jussa Ladhu jana alipokuwa akizungumzia uamuzi wa Marekani kuzuia fedha za MCC hadi muafaka wa uchaguzi utakapopatiwa ufumbuzi pamoja na kuondoa sheria kandamizi ya makossa ya mitandao. Jussa alisema hakuna njia ya kunusuru Zanzibar ((Tanzania)) Tanganyika kuwekewa vikwazo vya kiuchumi ikiwemo kunyimwa misaada zaidi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar kukubali kukamilisha uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu. Aidha alisema kuwa uamuzi wa Marekani wa kuzuia msaada unatoa fundisho kubwa kwa nchi nyigine kuheshimu mashariti ya kunufaika na fedha za MCC ikiwemo kulinda misingi ya Demokrasia na Utawala bora.
Jussa alisema matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa nchi ya Zanzibar yalifutwa kwa ubabe na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar baada ya kuona CCM wapo katika hatari ya kuanguka lakini hakuna kifungu cha Katiba kinachompa uwezo huo. Alisema msimamo wa CUF utaendelea kubakia palepale pamoja na kufanyika kwa mazungumzo ya kutafuta muafaka wa uchaguzi, ZEC warudi kazini wakamilishe kuhakiki na kutangaza matokeo na mshindi wa uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu. Alisema kuwa kuna kikundi cha watu wachache nchini Zanzibar ndiyo hawataki kuona mabadiliko yakitokea ya kiutawala hapa nchini Zanzibar licha ya CCM kushindwa kufikia malengo ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu.“Kuna kikundi cha watu Zanzibar hakitaki kuona mabadiliko ya kiutawala kwa maslahi yao binafsi licha ya CCM kuanguka katika uchaguzi wa Oktoba 25 Mwaka huu,”alisema Jussa. Alisema kuwa kadhia ya uchaguzi wa nchi ya Zanzibar imesababisha madhara makubwa ikiwemo wananchi kuishi katika mazingira ya wasiwasi pamoja na kupanda kwa gharama za maisha visiwani humo. Jussa alisema hakuna sababu kwa Viongozi wa CCM kuwa na wasiwasi wa kupoteza vyeo wakati marekebisho ya kumi ya Katiba ya nchi ya Zanzibar yameweka mfumo mzuri wa kuunda serikali ya pamoja na wao kunufaika kama CUF ilivyonufaka baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Aidha, alisema CUF haiko tayari kuona Uchaguzi Mkuu unarudiwa hapa nchini Zanzibar kwa malengo ya kuibeba CCM licha ya kuanguka katika uchaguzi wa awali Visiwani humo. Naibu Katibu Mkuu wa CCM nchini Zanzibar Vuai Ali Vuai, alisema kuwa haikuwa mwafaka kwa Marekani kuzuia msaada huo wakati Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ilikuwa na hoja za msingi za kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 Mwaka huu. Alisema kuwa uchaguzi wa Oktoba 25 Mwaka huu ulipoteza sifa za kuwa uchaguzi huru na wa haki baada ya kutawaliwa na vitendo vya udaganyifu kinyume na misingi ya demokrasia na utawala bora. Alisema hana wasiwasi na Marekani kuwa hawajapata taarifa na vielelezo vya kuharibika kwa uchaguzi wa Zanzibar na iwapo watapata taarifa hizo watakubaliana na uamuzi wa ZEC wa kufuta matokeo ya uchaguzi huo. Alisema  uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya udaganyifu ikiwemo idadi ya wapiga kura kuzidi watu waliosajiliwa katika daftari la wapiga kura wa kudumu pamoja na mawalaka wa vyama kupigwa na kufukuzwa katika vituo vya kazi. “Ufumbuzi wa migogoro sio kuzuia misaada kwa sababu unawaumiza hadi watu wasiokuwa na hatia, cha muhimu ni  kutafuta njia ya mufaka za kuondoa matatizo.”alisema Vuai ali vuai Mr BT.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

PROFESA MUHUNGO AWAMBIYA TENASCO WASHUSHE BEI YA UMEME

Nchini Tanganyika Bei ya umeme inatarajia kushuka wakati wowote kuanzia sasa baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (pichani )kuliagiza Shirika la Umeme (Tanesco), kushusha gharama za nishati hiyo.Katika hatua nyingine, Waziri huyo amefuta likizo za wafanyakazi wa shirika hilo ili  washughulikie tatizo la umeme nchini huku akisisitiza kuwa hataki kusikia kukatika katika kwa umeme kila saa.Profesa Muhongo alitoa maagizo hayo  jana jijini Dar es Salaam hapa nchini Tanganyika wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mtambo wa kuzalisha umeme wa Tegeta Gas Plant, ambapo alikwenda kwa ajili ya kukagua mitambo hiyo ili kuona kama yote inafanyakazi maana kila mara unasikia mitambo michakavu ndio maana umeme unakatika katika lakini alipofika mambo tafauti mitambo iko sawa kabisa ila tu ni ushenzi wa wafanya kazi wa Tanesco.Akitoa maelezo ya mtambo huo, Meneja Mohamed Kisiwa alisema wana mitambo mitano na wana uwezo wa kuzalisha Megawati 42 kila saa.

Alisema gharama ya uzalishaji umeme kwa uniti moja ni Sh. 90 na wamekuwa wakiuza kwa Sh. 180 hadi 187 lakini sio kweli maana watu wanauziwa mpaka 300 ila hapa wanajaribu kumdanganya profesa Muhungo kuwa ati wauza 180 mpaka 187.Profesa Muhungo alisema kwa maelezo ya meneja  huyo, inaonyesha umeme wanaozalisha wanapata faida mara mbili hivyo alisema kuna uwezekano mkubwa wa kushusha  gharama za umeme.Aliagiza maofisa wa wizara yake na wa shirika la Tanesco wakutane leo ili wajue umeme huo utashushwa kwa kiwango gani.“Utauzaje umeme mara mbili ya gharama za uzalishaji,  tunataka kuwapunguzia wananchi bei ya umeme  na kwenye mkutano wetu wa kesho (leo) tutajadili  kupunguza bei ya umeme..haya mahesabu hayajakaa sawa maana unazalisha uniti moja kwa Sh. 90 na kuuza kwa Sh. 180 tutajadiliana mpunguze,” alisema profesa Muhungo.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Thursday, December 17, 2015

BARUA YA WAZI KWA POMBE MAGUFULI-ALLY SALEH MBUNGE WA JIMBO LA MALINDI NCHINI ZANZIBAR

ally
Barua ya Wazi kwa Rais Magufuli. By Hon Ally Saleh. Member of the Union Parliament (Malindi Constituency)
Mheshimiwa
Amiri Jeshi Mkuu
Ikulu, Dar es salaam
Asssalam alaykum,
Natumai hujambo na familia na unaendelea na kazi kama msemo wako wa HAPA KAZI TU ulivyo. Inshallah Mungu atakupa afya na uzima uendelee. Pili nakupongeza kwa kuchagua Baraza la Mawaziri ambalo litafanya kazi na wewe, na sisi kama Wabunge kwa faida ya taifa.
Ingawaje hata hivyo, sikubaliani na wewe juu ya baadhi ya teuzi zako, kama vile kuwanyima fursa ya kutosha Wazanzibari na kuonekana Baraza lako kuwa ni la Tanzania Bara zaidi na kutufanya wadogo zaidi na wanyonge zaidi ndani ya Muungano.
Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu, hata hivyo nilotaka kukuandikia leo ni kuhusiana na hali ya usalama hapa kwetu Zanzibar na tishio la kutokuwepo Amani ambapo naamini wasaidizi wako watakuwa wamekuarifu, lakini nakuandikia nikiwa Mbunge wa Malindi kwa tukio lilotokea usiku wa juzi Jumamosi.
Tukio hilo la kuvunjwa vunjwa barza ya wana CUF katika eneo la Michenzani, Mjini Unguja kwa hakika ni muendelezo wa matukio mengi yanayofanywa na watu wanaoitwa wasiojulikana na ambayo yalishamiri sana wakati wa uchaguzi lakini hata baada ya uchaguzi yamekuwa yakiendelea.
Watu waliosemwa wakitumia magari rasmi ya Vikosi vya Zanzibar na wakiwa na silaha walifika eneo hilo usiku mkubwa na kufunga njia na kisha wakifanya ukhabithi huo, na Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu sehemu hiyo ni mita mia tatu tu kutoka Kituo cha Polisi cha Madema.
Tunajiuliza kwa nini tukio hilo lifanywe usiku kama ni zoezi la kawaida la kusafisha mji? Na hilo tunajua kuwa lilitanguliwa na siku chache nyuma gari moja iliyopita na kutangaza kwa bomba kuwa sehemu hiyo ivunjwe, bila ya kuonyeshwa amri halali ya kufanya hivyo.
Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu, sehemu hiyo maarufu huitwa Commonwealth na hadi leo haijaripotiwa kuwa na kitendo chochote kile cha ukosefu wa Amani tokea ilipoanzishwa.
Mita 100 tu upande wa pili kuna ile inayoitwa Maskani Mama ya Kisonge ambayo hiyo haiguswi wala haiulizwi na Polisi yoyote yule. Tokea kuanzishwa kwake hadi leo imekuwa na ubao unaoitwa Sauti ya Kisonge ambao umekuwa na matusi na kejeli kwa viongozi na hasa viongozi wa upinzani.
Ubao huo umekuwa ukichochea fujo, kutoa lugha ya kibaguzi na mara nyingi imekuwa ni chanzo cha kuzusha hamasa za kisiasa hapa Zanzibar, lakini inalindwa utafikiri ni taasisi rasmi ya kiserikali.
Siku chache nyuma, watu wasiojulikana wakiwa na silaha pia walivamia studio ya Hits FM wakati wa usiku na kuichoma moto na kutia hasara kubwa. Lakini hasara kubwa zaidi ni kuzima sauti za watu na kukaba uhuru wa maoni na kujieleza.
Wakati wa Kampeni makundi hayo pia yalitishia Amani ya wana habari kwa kumpiga mwana habari mmoja na kuvamia kituo cha radio cha Coconut FM mchana kweup wakiwa na silaha kama marungu, mapanga, msemeno wa kukatia miti na bunduki.
Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu, sitaki nikuchoshe kwa mlolongo wa matukio ya makundi hayo katika kupiga watu, kuvunja na kuchoma sehemu kadhaa, lakini nataka nikuhakikishie kuwa hakuna sauti yoyote ya kukemea iliotoka kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kwa uhakika Rais wa Zanzibar wakati huo, Dk. Ali Muhammed Shein alisema “ hana habari”; Waziri wa Vikosi wakati huo Haji Omar Kheir alisema “ hakuna ukweli” na Polisi walisema “hawajawaona watu kama hao.”
Dhamana ya usalama wa nchi nzima ni yako wewe. Sitaki niamini kuwa tuna utawala ulioshindwa (failed state) kwa sababu ya Zanzibar ambapo makundi haramu yanafanya yanavyotaka na hakuna wa kuwauliza. Hakunonekani kuna nia ya kisiasa wala ya kiutendaji kwa wasaidizi wako wa Zanzibar kulikabili na kulimaliza jambo hili.
Hakuna nia hizo kwa sababu makundi hayo wameyaunda wao kwa faida zao za kisiasa. Ila naamini katika picha kubwa ya taifa makundi haya yanaharibu sifa yako na yanajuburi ( challenge) mamlaka yako.
Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu, kuendelea kwa vitendo hivi hapana shaka kutashusha Imani ya wananchi kwa vyombo vyetu vya ulinzi vikiwemo Polisi na Jeshi la Wananchi na vikiwa chini yako. Na kushuka kwa imani hiyo kuna maana kuelekea kwenye fujo na vurugu (riot na anarchy).
Kanuni ya kuonewa inasema wazi kuwa anaeonewa hataonewa siku zote maana iko siku atasema basi na atajitetea hata katika hali yake ya udhaifu kuonesha msimamo wake na makundi haya yameonea sana watu wa Chama cha Wananchi CUF na nina hofu ya wanaononewa kusema wamechoka.
Wakati bado tumo kwenye kutafuta njia ya kutoka kwenye mkwamo ambao pia unatokana na ukweli kuwa Chama cha Mapinduzi hakina na hakijawahi kuwa na nia ya kutoa nchi kwa njia za kidemokrasia, matukio kama haya yana nia ya kuzidi kukwamisha kupatikana suluhu.
Haikubaliki kabisa, raia kuonewa, kunyanyaswa ndani ya mipaka yao, tena wafanye hao wa uonevu wakiwa ni wale waliopewa dhamana ya kuwalinda. Au kama wanaofanya hivyo sio wao, kufumba macho wenye nia hiyo chafu wakitekeleza dhamira mbovu.
Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu, naamini si kuwa kadhia zote hizi hazijafika mezani huko Magogoni jumba kuu, lakini pengine ushauri ulitolewa kuwa hili ni jambo la kupita na dogo tu. Lakini napenda kusema kama cheche huzaa moto na dogo huzaa kubwa.
Sina haki ya kukushauri kama hujaniuliza ushauri wangu kwa heshima yako, lakini napenda kusema hili lisimamie mwenyewe utake kujua undani utandu na ukoko. Kisha ulishikia fimbo limalizwe na wanaohusika kuliwachia wachukuliwe hatua.
Zanzibar leo imekuwa eneo la khofu. Khofu ya mchana ambapo katika malindo yanayofanywa na askari wa JWTZ wananchi wamekuwa wakipigwa mchura wanafanya makossa na usiku makundi mengine yakifanya hujuma na kutishia maisha na Amani. Tushukuru Mungu kuwa mpaka leo hakuna maisha yaliopotea.
Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu, ya Burundi, ya Burkina faso, ya Ivory Coast na kwengine tusiyaone yako mbali. Siku hizi tuna nafasi ya kujifunza mambo haraka na kuyazuia na naamini utalifanyia kazi hili ili nchi mshirika wa Muungano watu wake wafaidi uhuru wao wa kila kitu na isiwe kujikunyata.
Nashukuru na Mungu akubariki katika kazi na maisha yako.
Mwandishi wa Makala hii ni mshairi, mchambuzi wa siasa, mtunzi wa vitabu, mwanasheria na Mbunge wa Jimbo la Malindi.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

SPIKA WA BUNGE LA NCHI YA TANGANYIKA YUKO NCHINI INDIA KWA MATIBABU YALE YALE VIONGOZI WAKIUMWA NJE YA NCHI RAI KUFENI

Spika wa Bunge la nchi ya Tanganyika, Job Ndugai tayari asha anza kufunguwa listi za kuwa mgonjwa na yupo India kwa matibabu cheza na thulma weee. Katibu wa Bunge la nchi ya Tanganyika, Dk Thomas Kashililah alisema jana kuwa Ndugai yuko nje ya nchi kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake bila ya kusema amekwenda nchi gani wala ugonjwa unaomsumbua.

“Ni kweli Spika yupo nje, lakini alikwenda kwa ajili ya kufanya uchunguzi tu, siyo kwamba anaumwa sana, hapana ila hii ni mara ya pili kwenda kufanya uchunguzi huo. Hata ukitaka kuzungumza naye mpigie simu mtazungumza naye maana hali yake inaendelea vizuri na yuko salama,” alisema Dk Kashilila.

Balozi wa wao wa nchi ya Tanganyika nchini India, John Kijazi alipopigiwa simu ili kujua kama kiongozi huyo yuko huko, alisema:

“Ni kweli yuko hapa India kwa matibabu na anaendelea vizuri. Unaweza kumpigia wewe mwenyewe uzungumze naye.” Alisema Kijazi bila kuweka wazi kwamba yuko hospitali gani na nini hasa kinachomsumbua.

Ndugai hajaonekana hadharani, kwa muda mrefu, hata katika shughuli muhimu za kitaifa ambazo zimekuwa zikifanywa na Rais John Magufuli, hivyo kuacha maswali mengi kutoka kwa wapenda kuhalalisha haramu.Shughuli mojawapo ambayo Spika huyo hakuhudhuria ni ile ya kuapishwa mawaziri wapya au hayo majipu mapya Jumamosi iliyopita Ikulu, jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika. Naibu Spika, Dk Tulia Akson ndiye alihudhuria.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Wednesday, December 16, 2015

WANAUITA MGOGORO WA UCHAGUZI WA NCHI YA ZANZIBAR IMEKUWA NDIO BIASHARA KWA TV ZA NCHI YA TANGANYIKA NA KUTUCHEKA WAZANZIBARI KUWA NCHINI KWAO KUKO POA SISI TUNAENDELEA NA MIGOGORO

NCHINI TANGANYIKA PROF LIPUMBA NA KITILA WAZUNGUMZIA UCHAGUZI WA NCHI YA ZANZIBAR.  
WANAUITA MGOGORO WA UCHAGUZI WA NCHI YA ZANZIBAR WAKATI HAKUNA MGOGORO NA SOTE TUNAJUWA KUWA CCM IMESHINDU UCHAGUZI NA SHEIN WAO HAWATAKI KUKABITHI MADARAKA BASI LAKINI HAKUNA MGOGORO WOWOTE.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

MAHAKAMA YA RUFAA NCHINI TANGANYIKA M (TCM) IMETUPILIA MBALI OMBI LA RUFAA ILIYOKATWA NA MKURUGENZI WA MASHITAKA DPP

MAHAKAMA ya Rufaa ya nchi ya Tanganyika M (TCA), imetupilia mbali ombi la rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) la kupinga kupatiwa dhamana viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiisilamu (JUMIKI), kutokana na kukosa vigezo vya kisheria Lakini hata hivyo, pamoja na uamuzi huo mahakama hiyo imetoa nafasi maalumu kwa DPP kuwasilisha tena rufaa hiyo mahakamani hapo ndani ya siku 14.Uamuzi huo umetolewa na jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufaa, baada ya kusikiliza pingamizi za awali zilitolewa na wapinga rufaa hiyo kwa madai rufaa ya DPP juu yao imekiuka taratibu za kisheria.Katika maamuzi yake, Mahakama ya Rufaa ya M (TCA), ikiongozwa na Jaji Othman, Jaji Kimaro pamoja na Jaji Mussa imeungana na upande wa wapinga rufaa kwamba rufaa iliyowasilishwa na DPP imekiuka taratibu za kisheria kwa kukatwa nje ya wakati uliowekwa.Kutokana na kasoro hizo za kisheria zilizojitokeza katika ukataji huo wa rufaa, mahakama hiyo imeungana na upande wa wapinga rufaa na kuitupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na DPP mahakamani na kumtaka kuiwalisha tena ndani ya siku 14, endapo atashindwa sheria itachukua mkondo wake.Katika kikao kilichopita, wapinga rufaa hiyo kupitia Mawakili wao wa kujitegemea Abdalla Juma na Rajab Abdalla waliiomba mahakama itupilie mbali rufaa ya DPP dhidi ya wateja wake kwa madai imekatwa nje ya wakati.Mawakili hao walitoa hoja hizo wakati walipotoa pingamizi za awali ambapo Mawakili wa serikali kutoka ofisi ya DPP Raya Issa Mselem na Suleiman Haji, walidai rufaa hiyo ilikuwa ndani ya wakati na ilifuata vigezo vyote vya kisheria.Wakitetea hoja zao katika kikao hicho, Mawakili hao walidai Jaji wa Mahakama Kuu Fatma Hamid Mahmoud, hakulazimika kuwapatia dhamana wapinga rufaa hiyo kwa madai tayari walikuwa wameshatoa indhari (notice) mapema ya kutaka kukata rufaa Mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi huo.Walidai, kutokana na hali hiyo Jaji Fatma alitakiwa kuchukua uamuzi huo baada ya rufaa yao kusikilizwa pamoja na kutolewa uamuzi na Mahakama ya Rufaa na kuiomba mahakama ikubaliane na rufaa yao na kutupilia mbali pingamizi za awali za wapinga rufaa kwa madai hazina msingi wowote.Viongozi hao wa Jumuiya hiyo ya uamsho pamoja na wafuasi wao, walikatiwa rufaa na DPP kupinga uamuzi wa kupatiwa dhamana na Jaji Fatma Hamid ,Mahmoud kutokana ni haki yao ya kisheria na Kikatiba na kuzingatia kesi hiyo imekaa muda mrefu mahakamani bila ya kusikilizwa.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

VIDEO-WAZANZIBARI WAISHIYO NCHINI SWEDEN WAANDAMANA KUDAI MSHINDI ALIYE SHINDA UCHAGUZI ATAGANZWE MARA MOJA

MAANDAMANO YA WAZANZIBARI NCHINI SWEDEN

Taswira za Maandamano ya Wazanzibar Diasporan wa nchi Tanganyika,Zanzibar pamoja na wapenda amani na Demokrasia kote ulimwenguni. leo Jumatatu Wazanzibari waishio nchini Sweden na wapenda amani ya Demokrasia Dec 14, wameandamana huko Stockholm Sweden kwenye Parlament (Riksdag) kutaka Bunge na Serikali ya nchi hiyo kuibana Jamhuri ya Muungano feki wa Tanganyika ((Tanzania)) ili iheshimu maamuzi ya wananchi wa nchi ya Zanzibar waliyoyafanya kupitia Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

WAKUU WA CHAMA CHA CCM NCHINI ZANZIBAR WAMEELEWA SOMO TUNAWAPONGEZA KWA KUELEWA SOMO

IMG-20151214-WA0005

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Saturday, December 12, 2015

RAIS POMBE MAGUFULI HUU SI WAKATI WA KUJIPATIA MAADUI ZAIDI YA WALE WALIO KATIKA UONGOZI WA CCM AMBAO WANAKUSUBIRI KWA HAMU UFELI AU UJIKWAE WAKUCHEKE

Mhe. Magufuli aliwasili Zanzibar kwa lengo la kutambulishwa kwa wanachama wa CCM Zanzibar akiongozana na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan ambapo wote kwa pamoja walipata kuwasalimia wananchi wa Zanzibar kwenye viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar
KAMA kimya kinasema basi hichi kilichotanda miongoni mwa baadhi ya vigogo vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinasema mengi, tena kwa sauti kubwa. Hichi ni kimya chao kuhusu hatua ambazo Dkt. John Magufuli amejaaliwa kuzichukua katika kipindi cha siku thelathini ushei tangu aapishwe awe Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika kwa tiketi ya CCM. Hadi sasa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho ni Katibu wa Uenezi na Itikadi, Nape Nnauye, pekee aliyejitokeza akionekana kuwa yuko upande wa Magufuli. Nnauye, ambaye naye alichaguliwa mbunge kwa mara ya mwanzo katika uchaguzi uliopita, amejigamba kwa kusema kwamba Magufuli anachofanya ni kutekeleza atii ilani ya CCM. Juu ya hayo, hata naye pia amethubutu kuonya kwamba chama chake cha CCM kitaingilia kati endapo Magufuli atatenda mambo kinyume na chama hicho. Hilo ni onyo na tishio kwa Magufuli licha ya kuwa Nnauye hajawadhihirishia ni kwa njia gani chama cha CCM kitaingilia kati pindi akikikiuka chama chao. Jumapili hii iliyopita Ramadhan Madabida, mwenyekiti wa wenyeviti wa mikoa wa CCM alisema kwamba wenyeviti hao wanampongeza Magufuli kwa kasi yake ya kuwachukulia hatua watendaji wanaoshindwa kuyatekeleza majukumu yao. Wakuu wengine wa CCM wamejikunyata kama paka aliye rovyowa na maji ya mvua. Ama wamepigwa na muhuma kwa mshtuko walioupata, na wasioutarajia, kutoka kwa Magufuli. Kama si hivyo, basi wamepigwa na bumbuwazi na hawajui Magufuli ana mizungu gani mingine ambayo baadaye atawaonyesha Watanganyika na Wazanzibari haswa hao MaCCM walio zoe kula rushwa kwa miaka zaidi ya 50 sasa na ushaiyaa.
Ala kuli hali, hatua alizochukua mpaka sasa zimewatikisa walio karibu na hao vigogo na pia baadhi ya vigogo vyenyewe.
Sitoshangaa waathirika hao wakimwagia Magufuli maganda ya ndizi ili ateleze akiwa njiani kupigana na ufisadi, ubadhirifu pamoja na uzembe uliozagaa serikalini. Au huenda wakamwekea vizingiti ili ajikwae, wakitaraji kwamba ataanguka ili wamcheke na kumuumbuwa.Uzuri wa Magufuli ni kwamba yeye pamoja na waziri mkuu wake, Majaliwa Kassim Majaliwa, wanaonekana kuwa wanayajali maisha ya Rai wote kwa ujumla zaidi kuliko walivyo viongozi wengini wenye maradhi BT. Hilo halina shaka. Pili, wamekuwa wakichukua hatua bunifu, hatua tusizowahi kuziona zikichukuliwa na marais waliopita wa taifa hili baada ya Julius Nyerere. Tatu, kila moja ya hatua walizochukua ni kama yenye kumsuta au kumpiga kigongo Rais wa Awamu ya Nne, J Mrisho Kikwete. Tunaweza labda kuzimithilisha hatua hizo na yale maneno ya Nyerere dhidi ya uongozi wa Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi. Mwaka 1994, Nyerere aliandika kijitabu alichokiita “Uongozi Wetu na Hatima ya Tanganyika na Zanzibar”. Kijitabu hicho kilikuwa na mengi ya kuukaripia na kuukosoa uongozi wa serikali ya wakati huo iliyokuwa chini ya Mwinyi na Waziri Mkuu wake, John Malecela, pamoja na Katibu Mkuu wa CCM wa wakati huo, Horace Kolimba. Kwa vile Nyerere wa siku hizo hakuwa na madaraka serikalini hakuweza kufanya lolote ila kukemea. Magufuli mwenye madaraka serikali hana haja sana ya maneno. Kwa vile anao uwezo wa kikatiba wa kuchukua hatua basi amekemea kwa vitendo shabash.Wakati maneno ya Nyerere yalikuwa yakikinzana na uongozi wa aliyemfuatia kwenye madaraka, vitendo vya Magufuli vinakinzana na uongozi wa aliyemtangulia kwenye madaraka.Katika nchi nyingi Rais anayeondoka madarakani aghalabu hupendelea anayemrithi awe dhaifu kushinda yeye au asiwe mtu mwenye kung’ara kumpita yeye. Bahati mbaya tena nasema tena Bahati mbaya ya Kikwete ni kwamba amerithiwa kwenye madaraka na kiongozi anayeonekana kuwa mshupavu zaidi yake na ambaye, hadi sasa, kila hatua aliyoichukua imezidi kumnawirisha na kumfanya azidi kuwa kipenzi cha umma isipokuwa hapa juzi ameanza kulikoroga baada ya kumrudisha Profesa Sospeter Muhongo na Dk. Harison Mwakyembe katika madaraka watu wameanza kusema aha CCM ni CCM tu na rushwa haitakwisha kwa hiyo Magufuli anatakiwa awe makini zaidi kuliko alivyo fikiri kwani hao hao CCM ndio wamwanzo wao msuburi ajikwae ili wamzome kwa sababu washajuwa anapendwa na wananchi.
Kwa mujibu wa wananchi, Magufuli ni Rais mwenye kujiamini, mwenye uchungu na nchi yake na mwenye ari ya kizalendo. Hivyo ndivyo wamuonavyo wananchi. Zaidi ya hayo, wanaamini kwamba anajuwa anasema nini na anajuwa anafanya nini. Juu ya hayo yote, ameonyesha unyenyekevu kwa kusema, bila ya kubania, kwamba yuko tayari kujifunza asiyoyajuwa, kama alivyowaambia wafanya biashara aliokutana nao wiki iliyopita. Mara kwa mara amekuwa akisisitiza kwamba serikali iliyopo sasa ni serikali yake yeye John Pombe Magufuli. Haitaji kuwa ni ya CCM, ingawa ulimwengu mzima unajuwa kwamba yeye ndiye aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho. Tusisahau kwamba mara mbili tatu wakati wa kampeni ya uchaguzi wa urais alisikika akitamka hadharani kwamba CCM ni chama chenye wanafiki na kinachohitaji kusafishwa. Kwa kusema hayo akimaanisha kwamba hicho chama ni kichafu, yaani uongozi wake wa juu ni mchafu na akijuwa kwamba chanuka kwa wengi wa wananchi. Yote hayo yamewatia kiwewe wajionao kuwa ndio wenyewe wa kuiendesha nchi watakavyo kufanya watakavyo kwa kuwatesa wanyonge kwa kutumia madara yao sasa wameigiwa na kiwewe tafrani ndani ya nyoyo zao na roho zao hawapati usingizi tena, hata kama ni kwa kuzipinda sheria wao wako tayari. Ndio maana vigogo vya juu ndani ya CCM vimekaa kimya vikimkodolea macho tu Magufuli badala ya kumshajiisha katika bidii zake za kizalendo na kufurahi nae au hata kumuunga mkono hapa wako kimya wanatafakari. Tunayahifadhi majina ya wawili watatu, mmoja akiwa katika ngazi ya juu kabisa, ambao tunasikia kwamba faraghani wanamkebehi na hata kumcheka wakimfanya kuwa kama ni mwehu. Wanaikebehi kauli yake ya “kupasua majipu” na wanazifanyia dhihaka ahadi alizotoa.Ninazisikiliza hotuba zake, naiangalia ile iitwayo “lugha ya mwili” wake inavyosema na moyo unaridhika, unafarijika kwamba kweli huyu ni kiongozi mwenye kuyaweka mbele maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla na si ya chama chake au ya viongozi wa chama hicho walio zoea kuona kama hii nchi wamerithishwa kutoka kwa baba na babu zao na wengine wote ni watumwa wao.Huyu ni mtu ambaye unaamini kwamba atakifanya anachosema atakifanya kwa sababu unahisi ya kuwa anakikusudia kwa dhati yake. Haonyeshi kuwa na ajizi wala muhali.Magufuli ana sifa nyingine inayomzidishia haiba: anaweza kuyalainisha magumu kwa mizaha lakini katu si mcheka ovyo. Ukimsikiliza tu utajuwa kwamba kiongozi huyu hana mchezo. Hii ndiyo sababu inayowafanya wenye nguvu ndani ya CCM wawe wanamcha na kutafuta paa kujificha na makucha yao wameyarudisha ndani ya nyama zao za vidole wakisubiri wakati muafaka wamalize kiaina, wakati huohuo, kumchukia.Wameingiwa na wasiwasi mkubwa kwa sababu wanachelea asije akaamua kuyageukia na kuyafufua madudu yao waliyoyazika yakazikika. Kwa sasa hawawezi kumgusa kwani hagusiki kwa vile wananchi wengi wanamuunga mkono kwa hatua alizochukuwa.
Habari tunazozisikia ni kwamba wapinzani wake ndani ya uongozi wa CCM-Taifa wanaungwa mkono, chini kwa chini, na baadhi ya viongozi wa CCM-Zanzibar walio wahafidhina na wanaong’ang’ania madaraka kwa kukataa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar isiyatangaze matokeo yaliyosalia ya Uchaguzi Mkuu huko nchini Zanzibar. Pande la viongozi hao linaongozwa na Balozi Seif Ali Iddi,Vuai ali Vuai,Ameir Kificho,Nahodha N.K. na mpaka sasa hakuna hata mmojawao aliyejitokeza kuiunga mkono kasi ya Magufuli na hatua anazozichukuwa au hata kumpogeza wote kimya kama majini ya baharini. Pale ambapo kasi za Magufuli hazijaonekana bado ni katika kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa wa nchi ya Zanzibar. Mgogoro huo umesababishwa na hatua ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Firauni Jecha, kukataa kumaliza kuyatangaza matokeo yaliyosalia ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wa Urais wa nchi ya Zanzibar. Pamoja na hayo aliubatilisha uchaguzi Mkuu wa nchi ya Zanzibar isipokuwa ule wa wabunge na wa kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika huo hakubatilisha kuwachama kama ulivyo. Hatua hiyo imeipelekea Marekani kuonya kwamba itainyima Tanganyika msaada wa dola za Marekani milioni 472 lau mgogoro huo wa kisiasa wa nchi ya Zanzibar usipotanzuliwa. Marekani, pamoja na mataifa mengine yaliyo wafadhili wa Tanganyika, yanataka mgogoro huo umalizwe kwa kukamilisha zoezi la kutangaza matokeo yaliyoyabaki ya uchaguzi na kutangazwa kwa aliyeshinda urais wa nchi ya Zanzibar.Tuna taarifa kwamba Muungano wa Ulaya (EU) umekwishaanza kufikiria ni hatua gani za kiuchumi unazoweza kuchukuwa dhidi ya Tanganyika pindi ZEC isiporejelea zoezi la kutangaza matokeo ya uchaguzi wa nchi ya Zanzibar.Kasi ya Magufuli pia imepwaya kwa kutowaondosha nchini Zanzibar wanajeshi wa nchi ya Tanganyika waliopelekwa huko kutoka Tanganyika tangu siku za uchaguzi na aliyekuwa Rais wa nchi hiyo ya Tanganyika J.R.Kikwete na Kutawanywa wanajeshi hao mitaani na hili ni kuwatia watu hofu kubwa hasa kwa vile nchi ya Zanzibar haimo vitani wala hakuna hata fujo. Watu wanajiuliza kwa nini....?? au kunani.....??  Wanajeshi hao wametawanywa mitaani ilhali huko kwao nchini Tanganyika wanajeshi wameondoshwa mitaani baada ya kumalizika uchaguzi mkuu kwa nini iwe hivyo...??  Mwenye kuweza kuwatuliza wananchi wa Zanzibar kuhusu suala hilo ni yeye Magufuli akiwa Amiri Jeshi wa majeshi yote nchini kwa kuamrisha kwamba vikosi vilivyopelekwa nchini Zanzibar virudishwe huko nchini kwake Tanganyika. Asipochukuwa hatua za kuyatatua matatizo hayo ya nchi ya Zanzibar japo kuwa anaona ni nchi ndogo sana Magufuli atakuwa anajitafutia uhasama wa bure na wengi wa Wazanzibari wanaotaka utawala wa kisheria uheshimiwa kote ikiwa unahishimiwa nchini Tanganyika basi na nchini Zanzibar pia uheshimike sio nchini Tanganyika uheshimike nchini Zanzibar unaviringwaviringwa Magufuli atajiharibia jina lako la utendaji haki kwa wote. Huu si wakati wa kujipatia maadui zaidi ya wale walio katika uongozi wa CCM ambao wanakusubiri kwa hamu ufeli ili wakucheke na kukutukana. Hao viongozi wa CCM waliokaa kimya na wanaokerwa na miondoko yake ya uongozi ambayo ni miondoko iliyo safi sana mpaka wananchi wacheza mziki huu wa miondoko yako lakini hawa CCM hawana hila ila waendelee na kimya chao na labda waendelee pia kukuperemba Magufuli na kutamani ujikwae. Magufuli atafanya kosa kubwa akikipuuza kimya cha wasiomtakia yeye, na taifa, mema. Kimya chao ni cha shari na ni cha hatari. Ajue namna ya kupambana na wenye kimya hicho. Kwa sadfa, Nyerere alitanguliza kijitabu chake kilichoushambulia uongozi wa Mwinyi kwa shairi kuhusu ukimya lililoandikwa na malenga wa mwambao wa Kenya, Muyaka bin Haji Ghassany (1776-1840). Inafaa Magufuli ayakumbuke maneno ya ubeti wa mwanzo wa shairi hilo:
“Kimya mshindo mkuu, ndivyo wambavyo wavyele
Kimya chataka kumbuu, viunoni mtatile
Kimya msikidharau, nami sikidharawile
Kimya kina mambo mbele, tahadharini na kimya!”

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Friday, December 11, 2015

CCM UFISADI HAUTA KWISHA NGOOOooo POMBE MAGUFULI ANZA KUWARUDISHA MAJIPU KAZINI WALIO KULA MABILLIONI YA ESCROW

Saa chache baada ya rais wa nchi ya Tanganyika Pombe Magufuli kutangaza baraza lake la Mawaziri ambalo limekuwa baraza dogo kama alivyoahidi, aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) na mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu wamekosoa uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo na Dk. Harison Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe alikuwa waziri wa Uchukuzi katika serikali ya awamu ya nne na hivi sasa ameteuliwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria. Profesa Muhongo ambaye alijiuzulu kwa kashfa ya kuiba na kula Mabillioni ya Escrow katika serikali ya awamu ya nne, amerudishwa katika wizara ya Nishati na Madini. Profesa Lipumba amekosoa uteuzi wa profesa Muhongo kwa madai kuwa uteuzi wake umelitia doa baraza hilo.

“Kwa kitendo kama hiki, Pombe Magufuli amejiwekea dosari kutokana na uteuzi huu. Maana yake ni kuwa katika kashfa ile Profesa Muhongo hakuwa na hatia,” Profesa Lipumba aliliambia gazeti la Mwananchi.Profesa Lipumba aliongeza kuwa wananchi watapata ugumu kumuelewa Rais kutokana na ahadi zake kuwa atapambana na rushwa na ufisadi.

Naye Tundu Lissu aliliambia gazeti hilo kuwa uteuzi wa Dk. Harison Mwakyembe hakuwa sahihi kwa kuwa ndiye aliyekuwa waziri wa Uchukuzi na punde baada ya rais Magufuli kuingia ikulu, Mamlaka ya Bandari ikabainika kukumbwa na kashfa ya upotevu wa makontena.

“Juzi Rais Magufuli aliufumua uongozi wa Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kashfa, miongoni mwa waziri waliokuwa wakisimamia sekta hiyo ni Dk. Harrison Mwakyembe, eti leo amemrudhisha kundini...??” Lissu ananukuliwa.

Lissu aliongeza kuwa Muhongo pia hakufaa kuwa miongoni mwa mawaziri kwa kuwa alifukuzwa na Bunge kutokana na sakata la Escrow. Hata hivyo, Profesa Lipumba alimpongeza rais kwa kutekeleza ahadi yake ya kuunda baraza dogo kwa lengo la kubana matumizi.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

MJIHADHARI DUNGU ZETU MULIO NCHI ZA NJE AIRPORT YETU YA ZANZIBAR IMEINGIA MBONGE LA RUBA JIMAMA

Hivi karibuni nilipata taarifa kutoka kwa mtu wangu wa karibu kwamba kuna mzanzibari ambaye ni mkaazi wa UK alikamatwa airport Zanzibar na askari wa usalama pale airport askari huyo ni mwananamke ,tena ni mkorofi sana kwa taarifa nilizo pata, ameanza kutumiwa na wanaccm kuwatisha wazanzibari walioko nje.
Mkasa huyu mtu akifiwa na baba yake huko fuoni ,baada ya kupata taarifa na kuja Zanzibar kwa ajili ya msiba wa baba yake,ndio hali iliyo mtokea hapo airport Zanzibar, ndugu na jamaa zake wakafanya huku huku na kule ndio kutolewa madema.
Ninacho taka kusema ni kwamba mimi kama mzanzibari ninae ishi nje na kwa niaba yangu na familia yangu,na wanzanzibari wote ulimwenguni, kamwe hatutasita kuja nyumbani ,wakati wowte, na tunatuma salamu hapo usalama wa ccm kamba magereza yenu hatuogopi, na mukiendelea kuwanyanyasa wazanzabari na wasio wazanzibari tutawaandikia barua rasmi ubalozi wa uwengereza,canada na America na balozi nyingine wanajua nini cha kufanya, kama hamujui miaka ya nyuma nini kilitokea airport dar es salaam basi mtakipata na nyinyi.
Na mukiendelea na upumbavu wenu, tutashuka dar es salaam ,kwani visa tunalipa dola mia kila raia wa wa nje, ina maana ya kwamba fedha hizo titakwenda Tanganyika, sijui mutakua muna mkomoa nani zaidi ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar. Pia natoa tahadhari kwa yoyote atakae kumbana na unyanyasaji kama huu, wasiliana na ubalozi wa uk dar es salaam, pia tunawaomba mutoe taarifa kwa mwenyekiti wa ZAWA uk. Pia tutashirikiana na jumuiya nyengine za wazanzibari wanao ishi nje kama ZADIA ,na tutachukua hatua za kisheria, kwa kuwasiliana na balozi zilizopo  Tanganyika ((Tanzania))
Shukran

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Wednesday, December 9, 2015

MIAKA 52 YA UHURU WA NCHI YA ZANZIBAR

DECEMBER 10 1963 SIKU YA SHEREHE ZA UHURU WA NCHI YA ZANZIBAR

Kama ilivyo desturi ya hustoria kesho tarehe 10 December tunatimiza miaka 52 ya Uhuru wa nchi yetu ya Zanzibar.Mwaka 1963 Zanzibar ilipata uhuru wake kutoka kwa Mwingereza (Uingereza) chini ya utawala wa Sayyid Jamshid bin Abdalla bin Khalifa ambapo serikali yake ilikuwa ukiongozwa na Waziri Mkuu Sheikh Mohamed Shamte Hamad.Historia haufutiki hivyo kila Mzanzibar anayofursa ya kuisoma na kujifunza umuhimu wa siku hii. Pia ikiwezekana kuikumbuka.Kabla ya Uhuru Zanzibar ilikuwa na kipindi cha mpito, ambacho iliundwa serikali ya umoja wa kitaifa.Katika kipindi kifupi cha udumu wa serikali hii uliweza kufanya kadhaa na muhimu kwa nchi yetu, kama vile kuwa mwanachama wa UN, mwanachana wa Commonwealth, na taasisi nyengine za kimaitaifa.

Licha ya kuweko njama maalum ya kuifuta au kupotosha historia hii Wazalendo wa Zanzibar wataendelea kwa nguvu zote kuikumbuka na kuadhimisha kila ifikapo December 10, iwe ndani au nje ya Zanzibar.

Hongera Uhuru wa nchi ya Zanzibar