Wednesday, February 3, 2016

TAARIFA KWA UMMA ALHAD MUSSA NI LINI ULISEMA AU KUZUNGUMZIA KUHUSU MASHEIKH WALIO FUNGWA JELA KWA THULMA ZA SEREKALI YENU YA WAKOLONI WEUSI TANGANYIKA....??

TAARIFA KWA UMMA
IMETOLEWA LEO 02/02/2016
BAKWATA MKOA DAR HAINA MAMLAKA YA KUITAKA CUF KUINGIA KWENYE UCHAGUZI
ALHAD MUSSA ANASHUGHULISHWA ZAIDI NA DUNIA KULIKO KUSIMAMIA HAKI
NI VYEMA AKAJIFUNZA KWA VIONGOZI WA KIKRISTO KUHUSU ZANZIBAR
CUF - Chama cha Wananchi, tunasikisitishwa na kushangazwa na kauli ilitolewa leo na Alhad Mussa, kuunga Mkono ukiukwaji wa Demokrasia uliofanywa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) sio tu Kuna onyesha sura halisi ya Kiongozi huyo wa Kiroho Lakini pia kinamuonyesha jinsi asivyokua na khofu ya Kukabiliana na Mola wake kwa Matendo atendayo hapa Duniani au kwa kauli atowazo kama Kiongozi wa Dini. Cuf tumezoea kumsikia mara kadhaa akiwashauri Viongozi wa Kisiasa na Viongozi wenziwe wa Kiroho kwamba wasichanganye Dini na Siasa, Lakini leo ajabu kwetu kumuona Alhad Mussa sio tu akichanganya Lakini akichupa Mipaka na kuitaka Cuf ishiriki kwenye Uchaguzi. Bila Shaka Alhad Mussa ni Mwanachama wa CCM kama ambavyo aliwahi kujitambulisha kwenye moja ya Shughuli za Kiserikali zilizopambwa na kunogeshwa na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi. Kwakua umeshindwa kusimamia Maendeleo ya Jamii unayoiongoza, tunahakika Huku unapokuja Sasa hutapaweza. Hali ya Zanzibar kwa Sasa ni tete na si suala jepesi kama Vile kwenda Ofisi za Bakwata pale Kinondoni. CUF tunaipuza kauli yako kama tunavyopuuza Uchafu wowote ule utakao kwenye Majumba yetu. CUF inawapongeza Viongozi wa Dini ya Kikristo ambao wameshatoa kauli ya Kupinga Ubakwaji wa Demokrasia na Maamuzi ya Wazanzibar. Tuna mtaka Alhad Mussa ajifunze kupitia kwa Viongozi Hao wa Dini ya Kikristo ambao wameonyesha uadilifu Mkubwa kwa kukemea ubabaishaji unaofanywa na ZEC. Kama Hana cha kujifunza kutoka kwa Viongozi wenziwe wa Kiroho kama alivyo yeye, basi ajifunze kwa Makada wa CCM ambao wanaijua vizuri CCM zaidi yake, ambao ni Benard Membe, Joseph Butiku na Dr Salim Ahmed Salim. Hata hivyo katika ile dhana au ile nia ya Kushughulishwa zaidi na Dunia kuliko kazi ya kulingania Waumini wake kutenda Mema.
KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU 

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment