Friday, March 18, 2016

KUBAKA NA KUDHALILISHA WANAWAKE KIJINSIA NA KUTESA WATU NCHINI ZANZIBAR UNAENDELEA

PIX 4..
_40966312_sundayblood416ap
Katika hali isiyokua ya kawaida jana usiku vikosi vya SMZ viliendelea na kile kinachodaiwa kuwa maendelezo ya vitendo vya kuikandamiza demokrasia ya vyama vingi na uvunjivu wa haki za binaadamu katika maeneo mbali mbali ya visiwa vya Zanzibar.Kuna matukio kadhaa wa kadhaa ya upigaji, unyang’anyaji wa mali na ubakaji tayari yameshajitokeza katika visiwa vya Zanzibar.Jana usiku mnamo milango ya saa saba na nusu huko bububu katika nyumba ya bwana Kombo Hamad Salim ilivunjwa na vikosi vya sms kwa umaarufu mazombi na wakamchukua bwana kombo kwa kile walichodai anaenda kuhojiwa huku wakizichukua simu mbili moja ya mkewe bi sana na ya mtoto wao Aisha ili kuzichunguza. Wakati huo huo walimdhalilisha bi Sada kwa kumvua nguo na kumpitishia chumba cha bunduki katika sehem zake za siri mbele ya watoto wake.


Kuna taarifa pia iliripotiwa huko Mangapwani kwamba kulikua kuna kikao cha kahawa kwa bwana Francil Malali ambae ni mfuasi wa CHADEMA kwa kuvamiwa na kikosi cha kmkm waliokua wamesheheni silaha za moto kuvamia na kuwapiga zaidi ya wananchi 17 na kuwanyang’anya hadi viatu vyao na hatimae walimuendesha kichura mzee Mustafa mwenye umri wa miaka 59 hadi akazirai kwa kisingizio kwamba aliwajibu ujeuri.
Katika tukio jengine jana usiku maeneo ya Piki Pemba bibi Husna Muhammed mwenye umri wa miaka 32 alibakwana wanajeshi wawili wakati akihangaika kumtafutia mwanawe daktari alipokua akiumwa sana. Mama huyu alizingirwa na askari jeshi wa JWT na wakamchukua katika kambi yao na kumfanyie unyama huo.Huhohuko Pemba duru pia zinaripoti kwamba wanajehi jana walizungunga madrassa ya Kadiria ya Wete mnamo saa 12 za jioni na kuwapiga kwa mateke walimu na wanafunzi huku wakichanachana vitabu vya dini kwa walichodai kuwa wanawaandaa magaidi wa baadae.Bado tupo katika maeneo mbalimbali ya visiwa vya Zanzibar na tutawajuzi kinacho endelea.
KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment