Saturday, March 26, 2016

MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD AMEREJEA NCHINI ZANZIBAR

Siku chache baada ya Dikteta wa nchi ya Zanzibar Shein kuapishwa baada ya kushinda uchaguzi bandia aliyo pigiwa kura na majeshi na polisi na wahafidhina uliosusiwa na vyama vya upinzani na wananchi wote wa nchi ya Zanzibar kwani sio uchaguzi halali, Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amerejea nchini Zanzibar.Maalim Seif  Sharrif Hamad ambaye alikuwa mapumzikoni katika hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika kwa Wakoloni Weusi Tanganyika kwa takribani siku 17, jana alirejea nchini Zanzibar kuendelea na mapumziko yake.

Maalim Seif alilazwa katika Hospitali ya Hindu Mandal ya jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika kwa Wakoloni Weusi Tanganyika,mara baada ya kuruhusiwa March 8 mwaka huu alishauriwa na Daktari wake kupata mapumziko ya muda mrefu.Kurejea kwa Maalim Seif Sharrif Hamad nchini Zanzibar kunazidisha shauku na kiu ya baadhi ya Wazanzibari kutaka kusikia atakachokisema kiongozi huyo wa upinzani mwenye ushawishi mkubwa kwenye jamii.Maalim Seif Sharrif Hamad aliugua wakati Wazanzibari wakiwa katika mgumu kabisa wa kulazimishwa na Dikteta Shein wakubali kurudia uchaguzi mkuu uliofanyika March 20 lakini Wazanzibari wanajuwa wanataka nini wameweza kukata uchaguzi huo bandia na mwisho wake ulikuwa ni uchaguzi wa majeshi,polisi,wahafidhina na wenye maradhi ya BT.

KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment